fangfangjt
JF-Expert Member
- Apr 25, 2008
- 571
- 139
Askofu wa dayosis ya Pare ya KKKT Charles Mjema, amesema ubabaishaji katika uendeshaji wa nchi unaofanywa na baadhi ya watendaji wakuu serikalini ndio unaoitafuna nchi kwa sasa.
Wakati Askifu Mjema akitoa kauli hiyo, Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Karanga wa KKKT mjini Moshi, Fred Njama amesema mkakati wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wa kufikia maisha bora kwa kila mtanzania unatia shaka kuliko matumanini.
Viongozi hao waandamizi wa KKKT walitoa kauli hizo mjini Moshi mwishoni mwa wiki iliyopita katika mkutano mkuu wa 14 wa usharika wa Karanga, uliopo Soweto ambapo mgeni rasmi alikua asjofu Mjema.
Kauli za viongozi hao zimekuja kipindi ambacho kuna mjadala mkali nchini kuhusu hali ngumu ya maisha inayotokana na kupanda gharama za mafuta, mgawo wa umeme na ongezeko la bei za bidhaa na huduma mbali mbali.
Source: Mwananchi