Askofu: Serikali ya Kikwete imejaa wababaishaji

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
Askofu wa dayosis ya Pare ya KKKT Charles Mjema, amesema ubabaishaji katika uendeshaji wa nchi unaofanywa na baadhi ya watendaji wakuu serikalini ndio unaoitafuna nchi kwa sasa.

Wakati Askifu Mjema akitoa kauli hiyo, Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Karanga wa KKKT mjini Moshi, Fred Njama amesema mkakati wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wa kufikia maisha bora kwa kila mtanzania unatia shaka kuliko matumanini.

Viongozi hao waandamizi wa KKKT walitoa kauli hizo mjini Moshi mwishoni mwa wiki iliyopita katika mkutano mkuu wa 14 wa usharika wa Karanga, uliopo Soweto ambapo mgeni rasmi alikua asjofu Mjema.

Kauli za viongozi hao zimekuja kipindi ambacho kuna mjadala mkali nchini kuhusu hali ngumu ya maisha inayotokana na kupanda gharama za mafuta, mgawo wa umeme na ongezeko la bei za bidhaa na huduma mbali mbali.

Source: Mwananchi
 
Kauli hii haina udini bali huo ndiyo ukweli mtupu. Serikali yote imejaa wababaishaji tu ndiyo sababu kubwa ya matatizo mbali mbali ambayo ni sugu na yanashindwa kutatuliwa mwaka nenda mwaka rudi.
 
ni kweli ubabaushaji ni mwingi sana...........tena sana
 
Serikali inavyojitetea kwamba kupanda kwa maisha kunachangiwa sana na kupanda kwa bie ya mafuta duniani, mbona haijawahi kutueleza kama imefanya jitihada za kuwapunguzia wananchi wake ugumu wa maisha kwa kuondoa kodi ya foroza kwenye mafuta achilia mbali VAT na kodi nyinginezo nyingi walizoweka kwenye hayo mafut?
Badala yake wanatupiga changa la macho kwa kuondoa ushuru wa forodha kwenye sukari ambayo kimsingi sukari siyo kisababishi kikuu cha ugumu wa maisha.
.
 
kweli ubabaishaji umezidi yaani kila sekta ni bala bla tu hakuna chochote cha mhimu kabisa.
2015 naona ni mbali sana sijui wanannchi watafika.
 
Askofu wa dayosis ya Pare ya KKKT Charles Mjema, amesema ubabaishaji katika uendeshaji wa nchi unaofanywa na baadhi ya watendaji wakuu serikalini ndio unaoitafuna nchi kwa sasa.

Wakati Askifu Mjema akitoa kauli hiyo, Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Karanga wa KKKT mjini Moshi, Fred Njama amesema mkakati wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wa kufikia maisha bora kwa kila mtanzania unatia shaka kuliko matumanini.

Viongozi hao waandamizi wa KKKT walitoa kauli hizo mjini Moshi mwishoni mwa wiki iliyopita katika mkutano mkuu wa 14 wa usharika wa Karanga, uliopo Soweto ambapo mgeni rasmi alikua asjofu Mjema.

Kauli za viongozi hao zimekuja kipindi ambacho kuna mjadala mkali nchini kuhusu hali ngumu ya maisha inayotokana na kupanda gharama za mafuta, mgawo wa umeme na ongezeko la bei za bidhaa na huduma mbali mbali.

Source: Mwananchi

Wavue majoho sasa waingie kwenye siasa sio kujificha katika joho la dini.

Kumbe wametokea kule chimboko la Chadema. lakini Prof Maghembe
 
ASKOFU wa Dayosisi ya Pare ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Charles Mjema amesema ubabaishaji katika uendeshaji wa nchi unaofanywa na baadhi ya watendaji wakuu serikalini, ndio unaoitafuna nchi kwa sasa.

Wakati Askofu Mjema akitoa kauli hiyo, Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Karanga wa KKKT mjini Moshi, Fred Njama amesema mkakati wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wa kufikia maisha bora kwa kila Mtanzania unatia mashaka kuliko matumaini.

Viongozi hao waandamizi wa KKKT walitoa kauli hizo mjini Moshi mwishoni mwa wiki iliyopita, katika mkutano mkuu wa 14 wa Usharika wa Karanga uliopo Soweto ambapo mgeni rasmi alikuwa Askofu Mjema.

Kauli za viongozi hao zimekuja kipindi ambacho kuna mjadala mkali nchini kuhusu hali ngumu ya maisha inayotokana na kupanda kwa gharama za mafuta, mgawo wa umeme na ngozeko la bei za bidhaa na huduma mbalimbali.

Miongoni mwa bidhaa zinazolalamikiwa kupanda bei kwa haraka ni sukari ambapo kilo moja inauzwa kati ya Sh2000/ - na 2200/- tofauti na bei ya awali ambapo bidhaa hiyo ilikuwa ikuzwa kati ya Sh1600/- na 1700/- kwa kilo moja.

Kadhalika suala la mgawo wa umeme ni tatizo kubwa hivi sasa kiasi cha kukwaza shughuli za uzalishaji na utoaji wa huduma huku Serikali ikitoa taarifa kwamba mgawo huo unaweza kumalizika rasmi mwezi Julai mwaka huu.

Jana Askofu Mjema alisema: “Yapo masuala mengi ya ubabaishaji Dowans na mikataba mibovu isiyo na maslahi na nchi… yapo mambo yanayokera mpaka tunajiuliza tunakwenda wapi….kila siku hali inazidi kuwa mbaya kuliko jana yake”.

Askofu huyo alitaja baadhi ya mambo yanayokera Watanzania kuwa ni pamoja na malipo ya Sh94 bilioni kwa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans, michakato ya kuuza ardhi ya wanyonge na kumilikisha migodi kwa wageni.

Bila kumtaja kiongozi yeyote aliyekuwa akimlenga katika hotuba yake hiyo, Askofu Mjema alieleza kushangazwa na kauli ya kiongozi mmoja wa serikali kwamba hamfahamu mmiliki wa Dowans wakati kampuni hiyo ina mikataba na serikali.

“Inakuwaje una mkataba naye mmefanyaje kazi naye halafu unasema humjui?…maana yake ni kwamba watendaji wake aliowaweka hawako makini…hivi kweli mtasema mna Makatibu Wakuu kweli?”alihoji Askofu Mjema.

Maisha ya Wanyonge
Askofu huyo alisema Kanisa limepewa mamlaka na Mungu kutetea wanyonge wa Tanzania wanaokandamizwa na kudhulumiwa na watafanya hivyo hata kama kwa kufanya hivyo itawagharimu maisha.

“Tumepewa mamlaka ya kusema ni lazima tuseme maana Mamlaka tuliyo nayo ni kutoka juu…hatuwezi kufumbia uonevu uendelee halafu tukasema sisi ni kanisa…wajibu wa Kanisa ni Sauti ya Wanyonge,”alisisitiza Askofu Mjema.

Kwa upande wake, Mchungaji Kiongozi Fred Njama alisema kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana, Wakristo walimuomba Mungu awape viongozi watakaokuwa watumishi wa Taifa la Tanzania na sio mabwana.

“Tuliomba tupate viongozi wenye macho ya rohoni yenye kuona maumivu ya watu wa Mungu…hata hivyo kwa miezi hii michache mkakati wa viongozi wa serikali kufikia matarajio ya wengi unatia mashaka kuliko matumaini,”alisema Njama.

Mchungaji Njama alisema badala yake maisha hivi sasa hayashikiki huku bei za bidhaa zikipanda mara dufu na masuala nyeti kama ya Dowans na mzaha wa majibu ya viongozi wa serikali vinatia shaka umakini wa Serikali.

“Inatia uchungu na kukatisha tamaa…kutokuwa makini kwa utendaji wa serikali na matukio ya kizembe kama yale ya kujirudia kwa milipuko ya mabomu ya Mbagala na baadae Gongolamboto yameleta maafa,”alisema.

Mchungaji Njama aliwaambia wajumbe wa mkutano huo wapatao 150 kuwa mateso kwa Yatima na Wajane na vijana kukosa ajira huku wawekezaji wa Nje wakifaidika na maliasili na Madini ya Watanzania ni mambo yanayokera.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Wachungaji wa Sharika mbalimbali za KKKT ambapo ilielezwa kuwa mapato ya usharika huo kwa mwaka 2010 yakiwa ni Sh168.2 Milioni kulinganisha na lengo la kupata sh147.4 Milioni.

CHANZO: MWANANCHI MACHI 7, 2011
 
Uchaguzi umeshapita na JK kashinda. Blah blah zimeshapitwa na wakati. Wakati umefika wa kufanya kazi ili kujenga Taifa.
 
ndio tunajenga taifa kwa kuwaeleza wale wanaokosea makosa yao-bila kuwaeleza ukweli hawa taifa haltajegwa
 
ASKOFU wa Dayosisi ya Pare ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Charles Mjema amesema ubabaishaji katika uendeshaji wa nchi unaofanywa na baadhi ya watendaji wakuu serikalini, ndio unaoitafuna nchi kwa sasa.

Wakati Askofu Mjema akitoa kauli hiyo, Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Karanga wa KKKT mjini Moshi, Fred Njama amesema mkakati wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wa kufikia maisha bora kwa kila Mtanzania unatia mashaka kuliko matumaini.

Viongozi hao waandamizi wa KKKT walitoa kauli hizo mjini Moshi mwishoni mwa wiki iliyopita, katika mkutano mkuu wa 14 wa Usharika wa Karanga uliopo Soweto ambapo mgeni rasmi alikuwa Askofu Mjema.

Kauli za viongozi hao zimekuja kipindi ambacho kuna mjadala mkali nchini kuhusu hali ngumu ya maisha inayotokana na kupanda kwa gharama za mafuta, mgawo wa umeme na ngozeko la bei za bidhaa na huduma mbalimbali.

Miongoni mwa bidhaa zinazolalamikiwa kupanda bei kwa haraka ni sukari ambapo kilo moja inauzwa kati ya Sh2000/ - na 2200/- tofauti na bei ya awali ambapo bidhaa hiyo ilikuwa ikuzwa kati ya Sh1600/- na 1700/- kwa kilo moja.

Kadhalika suala la mgawo wa umeme ni tatizo kubwa hivi sasa kiasi cha kukwaza shughuli za uzalishaji na utoaji wa huduma huku Serikali ikitoa taarifa kwamba mgawo huo unaweza kumalizika rasmi mwezi Julai mwaka huu.

Jana Askofu Mjema alisema: "Yapo masuala mengi ya ubabaishaji Dowans na mikataba mibovu isiyo na maslahi na nchi… yapo mambo yanayokera mpaka tunajiuliza tunakwenda wapi….kila siku hali inazidi kuwa mbaya kuliko jana yake".

Askofu huyo alitaja baadhi ya mambo yanayokera Watanzania kuwa ni pamoja na malipo ya Sh94 bilioni kwa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans, michakato ya kuuza ardhi ya wanyonge na kumilikisha migodi kwa wageni.

Bila kumtaja kiongozi yeyote aliyekuwa akimlenga katika hotuba yake hiyo, Askofu Mjema alieleza kushangazwa na kauli ya kiongozi mmoja wa serikali kwamba hamfahamu mmiliki wa Dowans wakati kampuni hiyo ina mikataba na serikali.

"Inakuwaje una mkataba naye mmefanyaje kazi naye halafu unasema humjui?…maana yake ni kwamba watendaji wake aliowaweka hawako
makini…hivi kweli mtasema mna Makatibu Wakuu kweli?"alihoji Askofu Mjema.

Maisha ya Wanyonge
Askofu huyo alisema Kanisa limepewa mamlaka na Mungu kutetea wanyonge wa Tanzania wanaokandamizwa na kudhulumiwa na watafanya hivyo hata kama kwa kufanya hivyo itawagharimu maisha.

"Tumepewa mamlaka ya kusema ni lazima tuseme maana Mamlaka tuliyo nayo ni kutoka juu…hatuwezi kufumbia uonevu uendelee halafu tukasema sisi ni kanisa…wajibu wa Kanisa ni Sauti ya Wanyonge,"alisisitiza Askofu Mjema.

Kwa upande wake, Mchungaji Kiongozi Fred Njama alisema kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana, Wakristo walimuomba Mungu awape viongozi watakaokuwa watumishi wa Taifa la Tanzania na sio mabwana.

"Tuliomba tupate viongozi wenye macho ya rohoni yenye kuona maumivu ya watu wa Mungu…hata hivyo kwa miezi hii michache mkakati wa viongozi wa serikali kufikia matarajio ya wengi unatia mashaka kuliko matumaini,"alisema Njama.

Mchungaji Njama alisema badala yake maisha hivi sasa hayashikiki huku bei za bidhaa zikipanda mara dufu na masuala nyeti kama ya Dowans na mzaha wa majibu ya viongozi wa serikali vinatia shaka umakini wa Serikali.

"Inatia uchungu na kukatisha tamaa…kutokuwa makini kwa utendaji wa serikali na matukio ya kizembe kama yale ya kujirudia kwa milipuko ya mabomu ya Mbagala na baadae Gongolamboto yameleta maafa,"alisema.

Mchungaji Njama aliwaambia wajumbe wa mkutano huo wapatao 150 kuwa mateso kwa Yatima na Wajane na vijana kukosa ajira huku wawekezaji wa Nje wakifaidika na maliasili na Madini ya Watanzania ni mambo yanayokera.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Wachungaji wa Sharika mbalimbali za KKKT ambapo ilielezwa kuwa mapato ya usharika huo kwa mwaka 2010 yakiwa ni Sh168.2 Milioni kulinganisha na lengo la kupata sh147.4 Milioni.

CHANZO: MWANANCHI MACHI 7, 2011

....tatizo wananchi bado tunawabeba hawa wezi,,,,,tusirudie tena kuficha hawa wezi kwa kuwapa kura!!!
 
Uchaguzi umeshapita na JK kashinda. Blah blah zimeshapitwa na wakati. Wakati umefika wa kufanya kazi ili kujenga Taifa.
hayo maneno kamwambie mkwere, aache ubabaishaji afanye kazi ya kujenga taifa hatukumuajiri kuwa vasco da gama!!
 
Nimemvulia kofia huyu Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya Pare. Mkwere apate hiyo salamu kama huwa anasoma Gazeti la MWANANCHI.
 
JK alipotezea...

Wataelewa tu.

Unafiki haulipi siku zote, kuna watu walihoroja kuwa uongozi wake hauna maana na hauna jema hata moja.

Tuliona viongozi wa dini wakichochea vurugu kisa kuchinja, unagombania kuchinja kwa kuvunja nyumba za ibada!
 
Back
Top Bottom