Askofu Mwamakula: Polepole ametahadharisha tusipokuwa makini, Serikali inaweza 'kutekwa nyara' na kubaki kama 'mwanasesere'

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,029
Humphrey Polepole ameanza kujenga taasisi huru ya fikra! Hahitaji kiwanja cha kujengea taasisi hiyo wala hahitaji Wajumbe wa Bodi wa kuendesha kwani kichwa chake ndio Bodi yenyewe. Ameanza kutoa mihadhara kuhusu mustakabali wa nchi. Anatahadharisha kuwa tusipokuwa makini, Serikali inaweza 'kutekwa nyara' na kubaki kama 'mwanasesere'! Kwamba 'kikundi cha wahuni' wanaweza kuiteka nyara ikawa inaendeshwa na hicho kikundi!

Hizo ndizo fikra huru zenyewe! Lakini Polepole anasahau kuwa hata yeye alipokuwa Mwenezi na Msemaji wa Chama kinachoongoza Serikali, kuna watu walikuwa wanasema kama yeye anavyosema sasa! Watu wale waliokuwa na fikra huru wakati akina Polepole wameshika hatamu walipigwa; waliteswa; walitekwa; walibambikiwa Kesi za uchochezi, uhujumu uchumi na utakatishaji Fedha. Sisi Askofu tuliokuwa tukiwapazia sauti na kuwatetea watu hao tuliandamwa na hata kukiona cha moto.

Mwelezeni Mheshimiwa Humphrey Polepole kuwa sisi Askofu tunamkaribisha katika ulimwengu ulio huru ambao hauna dola ya kukutetea badala yake dola ndio iliyo na uhuru wa kukufanya cho chote kile! Kwa ujumla, katika ulimwengu huu hatuna kinga ye yote dhidi ya dola haijalishi tuna hadhi gani katika jamii! Huku ukitoa tu mawazo yaliyo tofauti na ya watawala au hata watu walio karibu na watawala, basi wewe unalo.

Jamii yetu huku ni kama ya wale wezee walioambiwa wakati Polepole yupo katika hatamu kuwa 'watatwangwatwangwa' na yule aliyekuwa Mkuu wa Mkoa ule aliozaliwa Mukwavinyika! Huku katika ulimwengu huu ulio huru, unaweza kulazwa mahabusu hata kwa kutetea watu haijalishi kama wewe ni Askofu au Profesa! Huku, Jeshi la Polisi halifuatu hata kanuni na Sheria za kukamata watuhimiwa! Huku, Askofu anaweza kufuatwa hata alfajiri katika faragha akiwa chumbani. Mwambieni Polepole kuwa asiwe na wasiwasi kwani akianza kufinywa kwa kusema ukweli na kutetea haki za wengine, sisi Askofu tutakuwa tayari kumpazia sauti. Mwambieni aungane na Askofu kuhamasisha upatikanaji wa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

7EF5BCCF-667C-42F0-AECF-E93DAC0709FB.jpeg
 
Raisi Samia kasema leo anataka matendo sio kelele za kwenye TV na Youtube. Huyu alifanya nini cha maana wakati wake zaidi ya kununua wagombea wa upinzani? Hiyo ndiyo sera za maendeleo?

Mdomo tu hakuna cha kuonyesha. Hebu tujiulize kabla ya siasa Polepole amewahi kufanya kazi gani kwenye sekta binafsi au shirika lolote la maana?
 
Wachumia tumbo hawa wakiwa uwanjani wanacheza ngoma basi hufumbia macho maovu yote ili tu wapate mkate wao wa kila siku. Japokuwa wanayaona maovu mengi na kuamua kuangalia pembeni wakati mwingi na wao huamua kushiriki katika maovu hayo ili kujitajirisha kwa njia haramu kwa kujua hakuna wa kugusa. Mwanakondoo ameshinda tumfuate!

Raisi Samia kasema leo anataka matendo sio kelele za kwenye TV na Youtube. Huyu alifanya nini cha maana wakati wake zaidi ya kununua wagombea wa upinzani? Hiyo ndiyo sera za maendeleo? Mdomo tu hakuna cha kuonyesha. Hebu tujiulize kabla ya siasa Polepole amewahi kufanya kazi gani kwenye sekta binafsi au shirika lolote la maana? !!
 
Wachumia tumbo hawa wakiwa uwanjani wanacheza ngoma basi hufumbia macho maovu yote ili tu wapate mkate wao wa kila siku. Japokuwa wanayaona maovu mengi na kuamua kuangalia pembeni wakati mwingi na wao huamua kushiriki katika maovu hayo ili kujitajirisha kwa njia haramu kwa kujua hakuna wa kugusa.
Mwanakondoo ameshinda tumfuate!
Ndio maana ya mtenda hutendwa,ama mwanakulitafuta mwana kulipata😂
 
Raisi Samia kasema leo anataka matendo sio kelele za kwenye TV na Youtube. Huyu alifanya nini cha maana wakati wake zaidi ya kununua wagombea wa upinzani? Hiyo ndiyo sera za maendeleo? Mdomo tu hakuna cha kuonyesha. Hebu tujiulize kabla ya siasa Polepole amewahi kufanya kazi gani kwenye sekta binafsi au shirika lolote la maana? !!
Lahaula kumbe alikuwa ananunua ?

Kwa fungu lipi mkuu ?
 
Tena huyo polepole mwambieni atulie tutamrarua hataamini Hawa ndio waliotumika kusema lisu kajipiga risasi mwenyewe pumbavu kabisa Malaya wa kisiasa wewe.
Mkuu siyo fair kabisa uliahidi utaniua kwa kuwaibia tv mwaka 1988 sasa inakuwaje unajipendekeza kumrarua Chakubanga kwanza wakati mimi uliniweka wa kwanza kwenye list yako ya kulipiza kisasi? Wewe unaonaona vizuri nikizidi kuendelea kuishi na uzee huu Figo haifankshen siwezi kugegeda.

Kamoooonn kill me now!
IMG_20210913_200339.jpg
 
Back
Top Bottom