Oh! Ninachotaka kueleza hapa ni hiki: Je, nani amesema Milingo ni mlei: Kanisa Katoliki au wachangiaji? Baadhi ya wachangiaji wanaweza wasiwe na uelewa wa kutosha wa 'theological' au 'canonical jagons' (technical issues) ndiyo maana nikaleta hiyo communique na article ya canon lawyer ili kuonesha Kanisa linasema nini kwa mtu kama Milingo.
Kanisa linasema 'validly ordained minister' hawezi kurudia tena ulei. Hata hivyo, kutokana na sababu fulanifulani kubwa (grave reasons) 'validly ordained minister' anaweza kuondolewa 'clerical status' - 'faculties', 'rights' na 'privileges' za daraja. Na hii inafanyika kwa namna mbili:
1) Mhusika mwenyewe kuomba aondolewe akieleza sababu kubwa (laicisation) au
2) Mamlaka husika kuona kwamba mhusika mwenyewe baada ya kuwa ameonywa kuhusu mambo kadhaa makubwa ambayo ni kinyume na kazi yake na mafundisho ya Kanisa na amekaidi, baada ya muda fulani kupita, huwa mamlaka husika zinatakiwa zimwondolee hiyo 'clerical status'.
Mfano wake ni archbishop Milingo. Hii ina maana kwamba: kuanzia siku ilipotangazwa, Milingo hana tena 'clerical status' na chochote atakachofanya, hatafanya kwa jina la Kanisa Katoliki na pia kuanzia siku hiyo Milingo hatakuwa mmoja wa maaskofu halali wa Kanisa Katoliki (those in active ministry) - hatakuwa na ofisi ya kiaskofu, kidaraja na wala hataweza kuhudumia jumuiya yoyote iliyo chini ya Kanisa katoliki kama askofu Mkatoliki.
Kwa Kiswahili rahisi, Milingo kwa sasa siyo tofauti na mlei (kwa vile hajafukuzwa kutoka kwenye Kanisa) bali kwa maana ya kuwa hana majukumu ya kidaraja/kiaskofu - i.e hana 'clerical status'. Pengine hapajapatikana msamiati mzuri wa kumwita mtu kama yeye, kwani kukosa 'clerical status' kwa lugha ya kawaida ni kuishi kama mlei anavyoishi.
Ila kwa kuzingatia 'valid ordanation' yake, katika hatari ya kufa, Milingo anaweza kutoa baadhi ya huduma za kipadre kwa wahitaji. Ukisoma Canon Law, utaona ni huduma gani anaweza kuzitoa katika hali kama hiyo.
Hivyo, katika kujadili kwetu pengine tungesema toka mwanzo tunajadili hoja hii kutoka upande gani: wa sheria za Kanisa au uelewa wa kawaida wa watu? Na nadhani hata hao wanaosema Milingo sasa ni mlei wanasemea katika 'context' ya kukosa 'clerical status' - yaani, kwamba kwa kawaida mtu asiye na 'clerical status' ni mlei. Sijui utakuwa umenielewa kwa hili au bado?
Kwa hiyo, Milingo hana tena 'clerical status' ndani ya Kanisa Katoliki!
Mkuu Magobe T,
Sikujua kwamba tuko pamoja. Natumaini hili limeeleweka kwa wengi. Heko JF kuwa thinkTank. Sasa tuje kwenye suala lingine la huyohuyo archbishop Millingo lenye utata kidogo.
Huyu Millingo si ndiye yuleyule ambaye tayari alishakuwa ametengwa au ex-communicated tangu 2006 yaani miaka mitatu iliyopita? Na hiyo ex-communication ndiyo adhabu kubwa kuliko zote. Kwamba chochote alichokifanya huko aliko tangu 2006 si cha Kanisa Katoliki wala kutambulika na kanisa hilo.
Leo tena miaka mitatu baadaye eti anaondolewa ukleri (clerical status) wakati tayari alishatengwa! Hiyo ina maana gani? Nini kimepungua au kuongezeka in terms of adhabu.
Kuna tofauti gani kati ya mapadri aliwapadrisha mwaka jana na atakaowapadrisha kuanzia sasa.
Je, si kwamba hii adhabu ya pili ni ndogo na haikutakiwa kuwepo? Afadhali wangeanza kumpa hii ya kumnyanga ukleri kama alivyonyang'anywa Privatus Karugendo halafu ndiyo ikaja ile kubwa ya kum-excommunicate?
Mkuu, naomba majibu yako maana najua utaniletea document ndefu kama kawaida yako na mimi ndiyo ninayoihitaji na sintachoka kuisoma. Inanisumbua sana akili hii kitu iliyofanyika kwa Millingo kwa mtizamo wangu huo.
Mkuu Magobe T, shusha darasa kali!