Abdulhalim
Platinum Member
- Jul 20, 2007
- 17,193
- 3,011
Ndugu yangu inawezekana kakobe akawa na nguvu ...lakini kwa kuwa yeye naye ni mwanadamu anaweza kutumia nguvu au ushawishi wake vibaya....hainiingii akilini kuona kakobe anapingana na serikali..bila sababu za msingi..
umeme unapita ndani ya hifadhi ya barabara ambayo inamilikiwa na TANROAD ..ambao wameshawapa kibali TANESCO...ndani ya hifadhi ya barabara ndipo panapohusu upanuzi wa barabara,mitaro,simu,gesi,umeme,maji etc...zote hizo ni huduma za jamii...ambazo ndugu kakobe hazipiti kwenye eneo la miliki yake....isitoshe hata mabango yake ameweka kwenye eneo la TANROADS tena bila kibali chochote...kimsingi kakobe hana haki yeyote pale zaidi nafikiri anazo hasira ....labda kwa kushindwa kuzuia kisheria wakati eneo lake lote la parking la kanisa alilojengaga barabarani lilipobomolewaga wakati wa kupisha upanuzi wa barabara ya Sam nujoma.........
serikali ya kikwete ina staha sana na huruma nadhani ...nafikiri angekuwa ni mkapa angembomolea kama alivomvunjia parking mwaka 2005.....na kakobe anautumia vibaya upole wa kikwete....
jambo lingine ambalo ni hatari kwa usalama ..linalotokea mara ya pili sasa ni la baadhi ya viongozi wa dini kama hawa kutumia misingi ya imani kuwachochea waumini wao kufanya jambo...tuliona wakati viongozi wa dini walipotumia imani kali ya kikristo kuingiza DECI na kuwafanya waamini kuwa DECI ni mkombozi aliyeletwa na YESU.....sasa kakobe anawafanya watu waache kulala makwao na wake zao au waume zao ...wanakesha wanaumwa na mbu kulinda eneo ambalo si la kwao kisheria ....nafikiri iikiendelea hivi badi anao uwezo wa kuwashawishi wajichome moto kama kibwetere[samahani kwa kufikia hapo]...lakini ndiko tunakoelekea kama tutaruhusu watu watumumie imani za waumini wau ..kuwatumikisha watakavyo!!!......
ni bora watu wa usalama wakawa makini na kuibuka kwa fundamenalism ...iwe kwenye christian everngelism au muslim ...zote ni sawa ...pamoja na kuwa ndugu zetu yao inatokuwa movements tofauti na ya wakristo ambayo mtu mmoja anaweza kuwakusanya watu kama mazoba na wakasahau kila kitu na kumfuata yeye....badala ya Mungu!!!
Unncecessary OVER-ANALYSIS na inalenga kupotosha ukweli. Suala la Waumini wa Kakobe kusimamia kile wanachokiamini ni sahihi kipimwe kwa hoja na sio hizi ad hominem. Vyombo husika vitalifanyia kazi hili suala kwa taratibu zilizopo. Haya mengine ni yenu na ni vyema mkadili nayo wenyewe kwenye vichwa vyenu.