Askofu: JamiiForums pekee ndio wameripoti Waraka wa TEC kwa Weledi

S.M.P2503

JF-Expert Member
Nov 25, 2008
1,646
2,610
Toka kwa baba Askofu Almachius Vincent Rweyongeza wa Jimbo katoliki la Kayanga
Media zote Tanzania hajaripoti Waraka wa TEC isipokuwa ni mitadao ya kijamii pekee na JamiiForums pekee ndio wameripoti tena kwa weledi mkubwa, je waraka huo haukukidhi vigezo vya kuw ahabari kubwa? La hasha ulikidhi ila hajaripotiwa kwa kuwa huenda umezuiliwa usiripotiwe ili usiwafikie walio wengi, lakini hawakujua nguvu ya mitandao habari husambaa kwa haraka zaidi kuliko mainstreem.

Na nawaasa wakati wa uchaguzi mchague viongozi watakaofaa, uchaguzi uliopita ulikuwa na makosa mengi sasa mchague viongozi wanaoweza kuwatetea na kuongoza vyema, na nyie mtimize wajibu wenu, mnachagua viongozi wanaobadili sheria za nchi ili ziwafae, na mnapewa rushwa na kuchagua viongozi wasiofaa sasa mnaanza kutuuliza sisi tuwasemee kwa nini mnatusukumia sisi,

Sisi tumetimiza wajibu wetu na tuko tayari kufa ndio maana ya nguo nyekundu hizi, tuko tayari kufa kwani tutakuwa tumekufa pamoja na Kristo kwa kutimiza wajibu wetu tatizo litabaki kwenu mtimize wajibu wenu.

====

Mwananchi mmoja aliyemsema ni huyu;
IMG_20230821_052317_768.jpg

Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC) limetoa tamko kupinga mkataba wa bandari. Ni tamko lililosheheni hekima na uwezo wa juu wa akili. Maaskofu 37 wametia sahihi kupitisha tamko hilo. Tamko limechambua vipengele vyote vyenye kasoro na kuvitolea ufafanuzi.

Jambo la ajabu media zote kubwa (Main streams) hazijaripoti habari hiyo. Sio ITV, ETV, Channel Ten, Clouds, WachafuTV etc. Wameipotezea. Hata online streams ni JamiiForums pekee walioripoti kwa weledi. Wengine either hawajaripoti kabisa au wameripoti kinafiki.

Kwa mfano Mwananchi wameripoti eti TEC YAMUANGUKIA SAMIA. Huu ni uandishi wa kikasuku. Hakuna popote TEC ilipomuangukia Samia wala kumuinamia. Wamekosoa mkataba wa bandari na kutoa mapendekezo yao. Yapo yanayomhusu Samia na yapo yanyohusu bunge. Hakuna aliyeangukiwa.

Lakini kwanini media kubwa (main streams) hazijaipa uzito habari hii? Je haikukidhi vigezo vya kuwa habari kubwa? Jibu ni HAPANA. Habari hii imekidhi vigezo vyote muhimu vya kuifanya iwe habari kubwa kama vile Timeliness, Impact, Proximity, Prominence etc.

Sasa kwanini haijapewa uzito kwenye main streams? Jibu ni kwamba serikali inadaiwa kuzuia main steams zisiripoti. Hata #MillardAyo amepost akalazimishwa kufuta.

"Bichwa kubwa" anaamini kwa kufanya hivyo atazuia waraka huo usisambae. Imagine alivyo na kichwa kikubwa halafu ana akili ndogo hivi? Ni huzuni. Hajui kama waraka umeshasambaa na kila mtu anao. Hajui mitandao ya kijamii inasambaza habari haraka kuliko hizo main streams?

Halafu nyie watu wa media jitafakarini sana. Mnaruhusije "censorship" kwenye vyumba vyenu vya habari? Yani mtu anaamuaje hiki andika na hiki usiandike? Yeye ni nani? Kumbuka moja kati ya makosa makubwa sana kwenye taaluma ya habari ni kuruhusu censorship, especially inayofanywa na serikali maana ni kuua uhuru wenu na kuua taaluma.

Leo mnaelekezwa msiandike habari ya TEC. Kesho mtaambiwa msiandike za BAKWATA.

Keshokutwa mtaambiwa msiandike za kwenu hata mkinyanyaswa. Acheni kutumika kama "bazoka" ambayo ikiisha utamu inatemwa.

Simanieni taaluma. Ingekua TEC imetoa tamko la kuunga mkono bandari mngeandika kwa mbwembwe sana. Lakini kwa sababu wamepinga mnapotezea kama hamuoni. Acheni Unaa.

Habari zaidi, soma:
  1. Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
 
Safi sana.

Vyombo vikubwa vya habari Tanzania vimejawa na unafiki na vinaiogopa sana CCM.

Hata Maalim Seif alipofanyiwa uhuni na JECHA (huko aliko ahukumiwe anavyostahili) hakuna hata chombo kimoja kilichoripoti kadhia Ile.
Kwa hiyo wanatoa waraka ili utangazwe kwenye vyombo vya habari?

Si walisema usomwe kwenye parokia na jumuiya zao? Sasa mbona mapovu yanawatoka kutaka utangazwe kwenye vyombo vya habari?

Wanavipangia vyombo vya habari habari za kutangaza? Kwani ni lazima vyombo vya habari viutangaze huo waraka?

Hawa watu ni kama wamechanganyikiwa wezi wakubwa
 
Hakukataa bila ya sababu. Alisema ni yeye aliyeiambia Serikali kuwa Hela za Tegeta Escrow zimechotwa iwaje yeye ndiyo ashitakiwe?

Na mpaka Leo yupo huru mtaani. Kama ni mhalifu ni kwa nini yupo huru??
Alisema wapi? Alitoa hizo taarifa wapi? Weka uthibitisho
 
Wewe ulitaka watoe waraka unahusu nini ?

Ila suala la bandari ni maoni yao hivyo serikali haijalazimishwa ila inajilazimisha TEC wakubali 😆.

Sasa kufanya rejea kwenye mkataba ni jambo baya au kuwasikiliza raia ni vibaya.

Serikali ijifunze kumsikiliza na kumjali raia wake kwanza. Shida ni kuwa tuna viongozi wengi wenye ulafi

Vyovyote vile . Walikula pesa za escrow na wala hawakuwahi kutoa waraka pamoja na kelele za wananch
 
Wewe ulitaka watoe waraka unahusu nini ?

Ila suala la bandari ni maoni yao hivyo serikali haijalazimishwa ila inajilazimisha tec wakubali 😆.

Sasa kufanya rejea kwenye mkataba ni jambo baya au kuwasikiliza raia ni vibaya.

Serikali ijifunze kumsikiliza na kumjali raia wake kwanza. Shida ni kuwa tuna viongozi wengi wenye ulafi
Kama hoja ni mawazo ya wananchi kusikilizwa kwa nini hawakutoa waraka juu ya maoni ya wananchi kusikilizwa pale wananchi walipowalalamikia wenzao kula pesa za escrow?
 
Back
Top Bottom