Askofu Bagonza: JWTZ ni Jeshi la Wananchi, si Jeshi la Watawala wala Viongozi!

ecolizer baba

Member
Sep 29, 2010
88
310
HAPPY BIRTHDAY MWALIMU JKN.

Hayati Baba wa Taifa, leo 13/4/2019 angetimiza miaka 97 ya kuzaliwa. Alizaliwa tarehe ya leo mwaka 1922. Niandike jambo moja kama kumbukizi na kumuenzi.

Mwaka 1985, wakati anastaafu, alihojiwa na chombo kimoja cha habari. Akaulizwa ataje jambo moja lililomsikitisha sana katika utawala wake, na moja lililomfurahisha sana. Alifikiri kabla ya kujibu. Na baadaye alitaja maasi ya jeshi (KAR) ya mwaka 1964. Tukio hili lilimsikitisha sana.

Akifafanua, alisema tulikuwa na miaka 3 tangu tupate uhuru. Tuliupata uhuru kwa kuwatukana sana wakoloni na mabeberu na kutangaza kuwa tunataka kuwa huru na kujitawala. Tulitumia kila aina ya lugha kuonyesha ubaya wa waingereza na majeshi yao.

Jeshi lilipoasi, Mwalimu na wenzake walitoa amri kuwataka wanajeshi waweke silaha chini lakini wanajeshi waligoma.

Ndipo baada ya siku kadhaa, Mwalimu na wenzake walilazimika kuomba msaada wa meli ya kijeshi ya Waingereza iliyokuwa Pwani ya mahali fulani. Kamanda wa meli hiyo, akitumia kipaza sauti toka melini, alitoa amri kuwataka wanajeshi walioasi waweke silaha chini na kurudi kambini Kolito. Walitii. Hili lilimsikitisha sana Mwalimu. Kuona wanajeshi wake wanatii amri ya mkoloni na kukaidi amri ya kiongozi wao mzalendo.

Masikitiko ya Mwalimu ndicho kiini cha kuvunja jeshi la KAR na kuunda JWTZ. Katika kifupi hiki cha jina la jeshi letu jipya, Mwalimu alisema, alipenda sana neno "Wananchi".

Kwa fahari kubwa, Mwalimu alipokuwa akitaja kuwa jeshi letu tangu wakati huo ni jeshi la wananchi, alionekana kuwa na furaha kubwa.

Mwalimu alituachia jeshi la Wananchi. Si jeshi la viongozi, wala la vyama, wala la awamu, wala la mtu yeyote. Ni jeshi la Wananchi.

Tukio lilomfurahisha alilitaja. Si kusudi ya kumbukizi hii. Watakaopenda kulijua, wasubiri siku nyingine.

Utaendelea kuishi Mwalimu.

Happy Birthday Mwalimu wetu Asiyestaafu.

Imeandikwa na Askofu Benson Bagonza (PhD)
 
Huo ndiyo ukweli mchungu

Inashangaza kumwona Kamanda wetu Jenerali Mabeyo ameamua kumlinda Jiwe badala ya kuwalinda wananchi wa Tanzania, kama anavyotakiwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977
 
Hapo ndio ujiulize kama Baba wa Taifa pamoja na kuwa mzalendo wa kweli kwenye nchi yake alipinduliwa ije iwe kwa awa wavunja katiba,sheria, kuminya uhuru wa kujieleza ? Haichukui hata dakika moja kuwekwa chini ya ulinzi na sijui kama Rwanda anaweza Saidia chochote.

Sijui unaenda tena kwa unaowaita mabeberu kuwaomba msaada? !!
 
Anaandika bishop Benson Bagonza

HAPPY BIRTHDAY MWALIMU JKN.

Hayati Baba wa Taifa, leo 13/4/2019 anget imiza miaka 97 ya kuzaliwa. Alizaliwa tarehe ya leo mwaka 1922. Niandike jambo moja kama kumbukizi na kumuenzi.

Mwaka 1985, wakati anastaafu, alihojiwa na chombo kimoja cha habari. Akaulizwa ataje jambo moja lililomsikitisha sana katika utawala wake, na moja lililomfurahisha sana. Alifikiri kabla ya kujibu. Na baadaye alitaja maasi ya jeshi (KAR) ya mwaka 1964. Tukio hili lilimsikitisha sana.

Akifafanua, alisema tulikuwa na miaka 3 tangu tupate uhuru. Tuliupata uhuru kwa kuwatukana sana wakoloni na mabeberu na kutangaza kuwa tunataka kuwa huru na kujitawala. Tulitumia kila aina ya lugha kuonyesha ubaya wa waingereza na majeshi yao.

Jeshi lilipoasi, Mwalimu na wenzake walitoa amri kuwataka wanajeshi waweke silaha chini lakini wanajeshi waligoma.

Ndipo baada ya siku kadhaa, Mwalimu na wenzake walilazimika kuomba msaada wa meli ya kijeshi ya Waingereza iliyokuwa Pwani ya mahali fulani. Kamanda wa meli hiyo, akitumia kipaza sauti toka melini, alitoa amri kuwataka wanajeshi walioasi waweke silaha chini na kurudi kambini Kolito. Walitii. Hili lilimsikitisha sana Mwalimu. Kuona wanajeshi wake wanatii amri ya mkoloni na kukaidi amri ya kiongozi wao mzalendo.

Masikitiko ya Mwalimu ndicho kiini cha kuvunja jeshi la KAR na kuunda JWTZ. Katika kifupi hiki cha jina la jeshi letu jipya, Mwalimu alisema, alipenda sana neno "Wananchi".

Kwa fahari kubwa, Mwalimu alipokuwa akitaja kuwa jeshi letu tangu wakati huo ni jeshi la wananchi, alionekana kuwa na furaha kubwa.

Mwalimu alituachia jeshi la Wananchi. Si jeshi la viongozi, wala la vyama, wala la awamu, wala la mtu yeyote. Ni jeshi la Wananchi.

Tukio lilomfurahisha alilitaja. Si kusudi ya kumbukizi hii. Watakaopenda kulijua, wasubiri siku nyingine.

Utaendelea kuishi Mwalimu.

Happy Birthday Mwalimu wetu Asiyestaafu.

Cc:
1. Rais Magufuli
2. Jenerali Venance Mabeyo
 
Huo ndiyo ukweli mchungu

Inashangaza kumwona Kamanda wetu Jenerali Mabeyo ameamua kumlinda Jiwe badala ya kuwalinda wananchi wa Tanzania, kama anavyotakiwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977
Kivipi mkuu!!! Nyinyi mlitaka amkabe na kisu au mnatakaje makamanda!!!
 
Hapo ndio ujiulize kama Baba wa Taifa pamoja na kuwa mzalendo wa kweli kwenye nchi yake alipinduliwa ije iwe kwa awa wavunja katiba,sheria, kuminya uhuru wa kujieleza ? Haichukui hata dakika moja kuwekwa chini ya ulinzi na sijui kama Rwanda anaweza Saidia chochote.

Sijui unaenda tena kwa unaowaita mabeberu kuwaomba msaada? !!
Rejea sababu za jeshi kutaka kuasi miaka hiyo, jeshi limefanya hayo majaribio mara tatu.
 
Unaweza kuwa unaongea na baba yako humu,kuna siku yoyote umenote baba yako kukosea, je ulimsaidia kumlala mama yako!!!!

Simply kwa sababu nafasi ya baba haina mbadala.
Hahahaha! Sindano imegusa naves. Hii inaonyesha ndivyo ulivyoishi na wazazi wako kwa kumsaidia baba yako.
Unahisi na wengine walifanya ulivyofanya wewe.
Chuma hunoa chuma, na wewe yupo mwanao atakayekusaidi maana kwa akili hii uliyonayo inaonesha unakosea sana kutimiza Majukumu yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu sikukusudi kukuumiza.
Hahahaha! Sindano imegusa naves. Hii inaonyesha ndivyo ulivyoishi na wazazi wako kwa kumsaidia baba yako.
Unahisi na wengine walifanya ulivyofanya wewe.
Chuma hunoa chuma, na wewe yupo mwanao atakayekusaidi maana kwa akili hii uliyonayo inaonesha unakosea sana kutimiza Majukumu yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HAPPY BIRTHDAY MWALIMU JKN.

Hayati Baba wa Taifa, leo 13/4/2019 angetimiza miaka 97 ya kuzaliwa. Alizaliwa tarehe ya leo mwaka 1922. Niandike jambo moja kama kumbukizi na kumuenzi.

Mwaka 1985, wakati anastaafu, alihojiwa na chombo kimoja cha habari. Akaulizwa ataje jambo moja lililomsikitisha sana katika utawala wake, na moja lililomfurahisha sana. Alifikiri kabla ya kujibu. Na baadaye alitaja maasi ya jeshi (KAR) ya mwaka 1964. Tukio hili lilimsikitisha sana.

Akifafanua, alisema tulikuwa na miaka 3 tangu tupate uhuru. Tuliupata uhuru kwa kuwatukana sana wakoloni na mabeberu na kutangaza kuwa tunataka kuwa huru na kujitawala. Tulitumia kila aina ya lugha kuonyesha ubaya wa waingereza na majeshi yao.

Jeshi lilipoasi, Mwalimu na wenzake walitoa amri kuwataka wanajeshi waweke silaha chini lakini wanajeshi waligoma.

Ndipo baada ya siku kadhaa, Mwalimu na wenzake walilazimika kuomba msaada wa meli ya kijeshi ya Waingereza iliyokuwa Pwani ya mahali fulani. Kamanda wa meli hiyo, akitumia kipaza sauti toka melini, alitoa amri kuwataka wanajeshi walioasi waweke silaha chini na kurudi kambini Kolito. Walitii. Hili lilimsikitisha sana Mwalimu. Kuona wanajeshi wake wanatii amri ya mkoloni na kukaidi amri ya kiongozi wao mzalendo.

Masikitiko ya Mwalimu ndicho kiini cha kuvunja jeshi la KAR na kuunda JWTZ. Katika kifupi hiki cha jina la jeshi letu jipya, Mwalimu alisema, alipenda sana neno "Wananchi".

Kwa fahari kubwa, Mwalimu alipokuwa akitaja kuwa jeshi letu tangu wakati huo ni jeshi la wananchi, alionekana kuwa na furaha kubwa.

Mwalimu alituachia jeshi la Wananchi. Si jeshi la viongozi, wala la vyama, wala la awamu, wala la mtu yeyote. Ni jeshi la Wananchi.

Tukio lilomfurahisha alilitaja. Si kusudi ya kumbukizi hii. Watakaopenda kulijua, wasubiri siku nyingine.

Utaendelea kuishi Mwalimu.

Happy Birthday Mwalimu wetu Asiyestaafu.

Imeandikwa na Askofu Benson Bagonza (PhD)

I appreciate Mwamunyange,he was best and Smart than Mobeyo....
 
Back
Top Bottom