Askari Polisi mstaafu, Saba Sita anafukuzana na kivuli cha mauti yake

Huyu askari mstaafu Kimaro a.k.a Saba Sita, anafukuzana na kivuli chake cha mauti.

Siyo rahisi kwa mila za kiafrika, kukikaribisha kifo kwa bashasha na kimipango kama huyu Saba Sita anavyofanya.
Msuti yake yamemkaa akilini kisawasawa na hafikirii kitu kingine cha maendeleo.
Huyu Saba Sita asingekuwa na muonekano wa afya, tungesema anaumwa, anatamani kufa.

Hisia zangu ni kwamba huyu Saba Sita kuna kitu kinamsumbua kiskili. Kuna mshali kacheza rafu wakati wa utumishi polisi.

Kuna harufu ya damu inamfukuzia.

Na ningetamani azamie kwenye bahari na mwili wake usionekane tuone lile jeneza na kaburi atawekwa nani..........kuna kitu kinamfuatiia huyo.
 
Kwa hiyo na anaeandika wosia mapema kabla ya kifo nae tumwone kachanganyikiwa? Kuna connection Gan kati ya mabaya aliyofanya mtu huko nyuma kusema yanamwandama Sasa hivi? Kuna uthibitisho wowote wa Hilo? Ama ni story tu.
Vipi kama ameamua kuwa tofauti sabab binafsi sioni tatizo lolote ni vle tu waswahili hamjazoea haya mambo mnaona eti ni mkosi, ukiulizwa nini maana ya mkosi na unafanyaje kaz huo mkosi unaweza kujibu?
Hata akifa baharini mwili usionekane si family yake itaweka hata nguo zake kweny jeneza na kuzika wabaki na Imani kwamba mzee tumemzika pale, kwani wanaochoma moto wafu si huwa wanazika majivu ya watu wao!
Acheni uswahili mambo hayapo hivo Tena, kama unajiweza andaa tu safari Yako mapema usisumbue watu. Wazee wetu wengine walinunua sanda wakaweka ndani. Fresh tu
 
Kifo kipo lakini sio cha kuchongea jeneza sababu mtu hujui utafia wapi. Kuna wale MV Bukoba meli ilizama wengine hadi leo hawajapatikana, kuna walioungua moto malory ya mafuta yalipolipuka miili ikaungua kiasi mtu.hatambuliwi, Ndege ya Malyasia ilipotea na abiria wote hadi leo miili yao haijawahi kupatikana irudi kuzikwa kwao

Sidhani kama ni sahihi kujijengea kaburi na jeneza sababu binadamu huwrzi jua kifo utakutana nacho wapi na kitakuwaje.
Ni matumizi mabaya ya pesa.
Aje huku msikitini kwetu tumsaidie kumpatia tiba.
 
Huyu ana matatatizo ya afya ya akili.Nduguze wamshauri aende hospitali ili aanze kupata tiba
Ni sahihi atafutiwe matibabu sababu hapo anawaza tu kufa aweza jiua.Ni kama kapoteza matumaini ya kuishi kabisa awaza siku gani ataondoka.Anaona dunia kama ni katili kwake isiyofaa kabisa kwa yeye kuishi.Kichwani kajaza hallucinations za dunia katili sana kwake.

Hiyo hali sio nzuri aweza jidhuru au kudhuru wengine atafutiwe tiba
 
Huyo nasikia aliua sana kipindi chake ,ilo jina la sabasita means ni NJUGU hizo alizokuwa anamiminia watu.
 
Kaua Sana kwa wale tuliokulia Moshi na Arusha tunamjua Sana ni katili Sana
 
Nilimsikia siku nyingi kuwa alikuwa kiboko ya majambazi lakini inasemekana alikuwa anawatanguliza hata some innocent suspects
 
Utayari ni jambo jema sana, naona afande Mstaafu Sabasita anaendeleza harakati zake za kujiweka tayari akisubiria sherehe ya umauti wake. Ya Mungu mengi si haba kuona uthubutu wa aina hio. Alishachimba Kaburi kutengeneza safi na sasa Jeneza liko tayari.

Kwa hayo machache karibu tumtie moyo na kuhamasisha wengine wafuate mkondo huo.

Ni hayo tu

Wadiz
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom