Asingekuwepo "Kikwete rais" mimi ningepigia kura CCM

The Lamb

Member
Jan 31, 2013
33
1
Nakili kwamba mimi nilikuwa mwanachama hai wa CCM na mkereketwa hasa. leo nimebadilishia gear angani na kujiunga na UKAWA. Nina sababu nyingi lakini kwa leo ni hizi.

Kwanza: Nilikuwa na imani sana na Rais Kikwete kwamba angetukwamua katika umaskini huu, lakini yeye na CCM chama nilicho kipenda ameshindwa.

Pili: Mfumo wa uongozi na kanuni zake kukiukwa, leo hii wamewapuuza watu wakubwa kama Bilali,Pinda,Mwandosya na wengi tu kwa sababu tu ya Lowasa je kesho labda AMANI yetu kwa ajili ya CCM.

Tatu: kushindwa kabisa kusimamia uchumi wa nchi.

Nne: Amani ya nchi mimi nimegundua CCM inafanya juu chini kufanya udanganyifu wakati wa kupiga kura na matokeo yake ipo tayari kupora matokeo.

Sasa ili wasifanikiwe ni bora kura yangu iende UKAWA ili hata wakiiba zibaki za kutosha. Ewe mwana CCM geuka hiki chama sio tena cha wanyonge bali ni chama cha watu wachache kwa maslahi ya wachache.

KARIBU UKAWA.
 
Back
Top Bottom