Asilimia kubwa ndugu huvunja ndoa za ndugu zao

Dejane

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
49,758
68,896
Tubadilike mtu akishaoa au akiolewa waacheni waishi maisha yao,watu wameoana tayari mshaenda kujazana kuishi hapo mara bibi,sijui shangazi, sijui shemeji, acheni wanandoa waishi kwa uhuru mnawabana, mara waletewe mtoto sijui wa nani walee, acheni wanandoa waishi wenyewe kusalimiana iwe mara moja moja na mtoe taarifa sio kwenda tu kama kwenu.

Ndugu mnachangia sana wanandoa kuachana kwa sababu mkishaenda kukaa mnaanza maneno na chokochoko. Watu wakioana waacheni waishi maisha Yao wapeni uhuru, wapeni nafasi.

Kina mama wengi wanavunja ndoa za watoto wao kwa kuingilia na kuanza kuwapangia wanandoa waishi namna gani, wazae watoto wangapi? Kina mama kuweni busy na maisha yenu maisha ya wanandoa hayawahusu nyie wabarikini inatosha sio kuanza kuchongoa midomo na wivu wivu usio na maana, eti kisa umemzaa kwa uchungu ndio umpangie maisha haitakiwi

Nimegundua ndoa nyingi huvunjika kisa ndugu,kwenda kujirundika kukaa kaa tu kwa watu wameoana
Tubadilike
 
Wakati wa uchumba mbona mnajifanya kuwapenda sana ndg wa mume? Hizo kanuni za kutobanwa mziainishe kabla ya kuolewa, acheni roho mbaya, maisha ya kiafrika ndo hayo, Kwanza ndg wa mume unakuwa na hakika hawezi kukuibia mume kwa asilimia nyingi
 
Mnatuchanganaya sasa elewekeni tuwaruhusu ndugu au tusiwaruhusu..?
Nataka kuoa hivi karibuni semeni upesi au niwape mda kwanza mvutane ndo mlete jibu..?!
 
Siaminu ktk kuwa Kila kitu kwa mwanaume, siwezi kuwa mama dada kaka shangazi Kila mtu ana nafasi yake ktk kumfurahisha mwanaume husika kutegemeana na mapito ya maisha yake,, huwa najisemea hivi mchana atazunguka na nduguze, ila usiku Mimi ndo nitalala nae, siwezi jihangaisha na mtu asieweza kulala uchi na mume wangu,
 
Ila mdogo wako wakike huwezi muacha na mumeo..?
 
Wakati wa uchumba mbona mnajifanya kuwapenda sana ndg wa mume? Hizo kanuni za kutobanwa mziainishe kabla ya kuolewa, acheni roho mbaya, maisha ya kiafrika ndo hayo, Kwanza ndg wa mume unakuwa na hakika hawezi kukuibia mume kwa asilimia nyingi

Wawape nafasi sio kurundikana hapo kabla watu hawajaoana walikuwa wanaishie wapi
Kila mtu aishi kwao au kwake
 
Wakati wa uchumba mbona mnajifanya kuwapenda sana ndg wa mume? Hizo kanuni za kutobanwa mziainishe kabla ya kuolewa, acheni roho mbaya, maisha ya kiafrika ndo hayo, Kwanza ndg wa mume unakuwa na hakika hawezi kukuibia mume kwa asilimia nyingi
kumbe wasiwasi ni kuibiwa mume 🤣🤣🤣🤣
 
Nyie si ndo huwa mnajisema mmeumbiwa tamaa leo imekuwaje:?

Kila abiria achunge mzigo wake😂
Sio wote mi mbona sina tamaa nimeutuliza tulii sitaki kelele na mtu!.. mi hata mdogo wako awe mzuri Kama Cleopatra simshobokei hata awe amebarikiwa mwili wote kwa kutuna panapostahili kutuna na kubonyea panapostahili kubonyea mi hata sina time...😁
 
Tubadilike mtu akishaoa au akiolewa waacheni waishi maisha yao,watu wameoana tayari mshaenda kujazana kuishi hapo mara bibi,sijui shangazi,sijui shemeji,acheni wanandoa waishi kwa uhuru mnawabana, mara waletewe mtoto sijui wa nani walee ,acheni wanandoa waishi wenyewe kusalimiana iwe mara moja moja na mtoe taarifa sio kwenda tu kama kwenu .

Ndugu mnachangia sana wanandoa kuachana kwa sababu mkishaenda kukaa mnaanza maneno na chokochoko. Watu wakioana waacheni waishi maisha Yao wapeni uhuru,wapeni nafasi.

Kina mama wengi wanavunja ndoa za watoto wao kwa kuingilia na kuanza kuwapangia wanandoa waishi namna gani ,wazae watoto wangapi?
Kina mama kuweni busy na maisha yenu maisha ya wanandoa hayawahusu nyie wabarikini inatosha sio kuanza kuchongoa midomo na wivu wivu usio na maana,eti kisa umemzaa kwa uchungu ndio umpangie maisha haitakiwi

Nimegundua ndoa nyingi huvunjika kisa ndugu,kwenda kujirundika kukaa kaa tu kwa watu wameoana
Tubadilike
ukweli mtupu
 
Inatakiwa uvae uso wa mbuzi.. ndugu sio wa kucheka cheka nao.

Sent using Jamii Forums mobile app
kabisa, mkiachana wanaanza kukusema tena wakati uliwapa priority
 
Mnatuchanganaya sasa elewekeni tuwaruhusu ndugu au tusiwaruhusu..?
Nataka kuoa hivi karibuni semeni upesi au niwape mda kwanza mvutane ndo mlete jibu..?!
wapende sema usiwaruhusu wakuharibie ndoa yako, umeoa tu ndugu washajazana nyumbani kwenu, hii inafanya kila siku muwe na ugomvi maana hamko huru, unataka kumtoa mke wako out ndugu wanaanza kumsema anakuchuna .
Ndugu wakija kusalimia wasikae mda mrefu wakawa too comfortable.
Wakiwa na shida za kifedha watumie kiasi (huruma isizidi uwezo)
Wakikupa madhaifu ya mwenzi wako, yapokee lakini tumia akili zako pia kumtetea ila ukirud kwake mkanye chumbani
 
Mnatuchanganaya sasa elewekeni tuwaruhusu ndugu au tusiwaruhusu..?
Nataka kuoa hivi karibuni semeni upesi au niwape mda kwanza mvutane ndo mlete jibu..?!
wapende sema usiwaruhusu wakuharibie ndoa yako, umeoa tu ndugu washajazana nyumbani kwenu, hii inafanya kila siku muwe na ugomvi maana hamko huru, unataka kumtoa mke wako out ndugu wanaanza kumsema anakuchuna .
Ndugu wakija kusalimia wasikae mda mrefu wakawa too comfortable.
Wakiwa na shida za kifedha watumie kiasi (huruma isizidi uwezo)
Wakikupa madhaifu ya mwenzi wako, yapokee lakini tumia akili zako pia kumtetea ila ukirud kwake mkanye chumbani
 
Tubadilike mtu akishaoa au akiolewa waacheni waishi maisha yao,watu wameoana tayari mshaenda kujazana kuishi hapo mara bibi,sijui shangazi,sijui shemeji,acheni wanandoa waishi kwa uhuru mnawabana, mara waletewe mtoto sijui wa nani walee ,acheni wanandoa waishi wenyewe kusalimiana iwe mara moja moja na mtoe taarifa sio kwenda tu kama kwenu .

Ndugu mnachangia sana wanandoa kuachana kwa sababu mkishaenda kukaa mnaanza maneno na chokochoko. Watu wakioana waacheni waishi maisha Yao wapeni uhuru,wapeni nafasi.

Kina mama wengi wanavunja ndoa za watoto wao kwa kuingilia na kuanza kuwapangia wanandoa waishi namna gani ,wazae watoto wangapi?
Kina mama kuweni busy na maisha yenu maisha ya wanandoa hayawahusu nyie wabarikini inatosha sio kuanza kuchongoa midomo na wivu wivu usio na maana,eti kisa umemzaa kwa uchungu ndio umpangie maisha haitakiwi

Nimegundua ndoa nyingi huvunjika kisa ndugu,kwenda kujirundika kukaa kaa tu kwa watu wameoana
Tubadilike

Mimi juzi tu nimemkataza mpwa wangu kuja kukaa kwangu.

Ni hivi, huyu mpwa wangu nilimleta mjini, nikasimamia show akapata msingi wa kukaa mjini. Mimi baadae nikachomoka nimefikia ughaibuni ila mke wangu mmoja yupo mkoani. Sasa mpwa anataka kuhama Dar kurudi mkoani baada ya miaka kama 7 hivi toka nimuache Dar, anaomba nimpe hifadhi kwangu.

Yaani afikie kwa mke wangu anapojipanga, hii siyo mara ya kwanza yeye kujaribu kurudi mkoani, 2019 aliniomba hifadhi hivi hivi nikamruhusu, cha kushangaza alifika kwangu na watoto wawili, kwanza hakuniambia amepata mtoto wingine mdogo. Wa kwanza nilijua anaye ila pia hakuniambia anakuja naye kwangu.

Sasa baada ya muda akaamua kuondoka kurudi Dar, leo anaomba kurudi kwangu. Inamaana nitakuwa na wajibu wa kumlisha na watoto wake wawili, najua tu atakapofika tu wataanza mambo yao ya wanawake watagombana na mke wangu bure, mke wangu na mtoto wangu nawahudumia kwa bajeti nayoiweza mimi, nikimruhusu aje na watoto wake wawili ntakuwa na bajeti ya watu watano na karaha juu.

Nimeamua kuwa mbaya. Sitaki ujinga wa ndugu. Isitoshe nyumbani kwao siyo mbali na ninapoishi sema kwa kuwa amechezea maisha kama mwanamke anaona aibu kwenda kukaa nyumbani kwao.

Nimemuambia kwangu hakuna nafasi ajipange atafute namna ya kuanza maisha. Nimefanya hivyo kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima katika familia yangu na pia kumpa changamoto ajisimamie, siyo kila siku aje kuomba msaada atazoea.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom