Asili Ya Green Guard Ya CCM na Changamoto Kwa CHADEMA

Why is it so important to get the face? Because unless we have the fact we can't possibly even attempt to solve our problem intelligently. Without the facts, all we can do is stew around in confusion. Nikupongeze mleta mada ingawaje kuna watu hawapendi ukweli.
 
Ni bahati mbaya kwa mchambuzi mwenye uwezo mkubwa namna hii kushindwa kugusia kiini cha mjadala uliozuka kuhusu vikundi vya ulinzi vya vyama, kwa level ya analysis kama hii, sitaki niamini kuwa ameoverlook the target bali nashawishika kuwa pengine mchambuzi ana uwoga wa kutarget kiini cha mjadala ama analinda interest. Ama alivyosema atarudi baadaye kwa mjadala zaidi, natarajia ataendeleza mjadala ambao utaeleza au utajibu maswali yafuatayo.
1. Ni lini hasa CCM walianzisha Green Guard?
2. Nini kilipelekea CCM kuja na Green Gurads
3. Je kuna sheria yoyote au katiba imevunjwa katika kuanzishwa kwa Green Guard
4. Kwa ufahamu wangu, CDM imekuwa na Red Brigade kabla ya hatua ya hivi majuzi, je serikali inalifahamu hilo?
5. Katiba za vyama zinasemaje kuhusu kuwa na vikundi vya ulinzi? kama kuna kipengele hicho, je masaji anaelewa?
6. Je, kuna haja ya hivi vikundi vya ulinzi?

Nakubaliana na wewe mkuu,

Huenda katika mizani mwanzo ya uchambuzi tunatofautiana,

Lakini ningekuwa ni mimi ndiye nakusudia kuchambua suala hili kama lilivyo katika kicha cha makala hii hakika ningetembea katika msingi huo hapo juu mkuu!

Yote kwa yote lazima tumpongezi ndugu yetu Mchambuzi, amejitahidi sana japokuwa kuna mapungufu machache katika mantiki, lakini haiharibu tafakuri zetu!
 
Tutazunguuka kooote lakini Ukweli utabaki tu kua malengo ya Red Brigade ni sawa tu na ya Green Guard na Blue Guard.

RED BRIGADE
Benson Kigaila na Freeman Mbowe wameizungumzia Red Brigade kama kikundi cha vijana wa Chama wenye jukumu la kulinda Chama na viongozi wake katika mikutano mbalimbali na hata nje ya mikutano. Hili suala la kujilinda sio geni, na hata CUF wana kikundi chao pia cha kujilinda. Zipo taarifa kua hata mlipua bomu wa Arusha pale Soweto alilinda na polisi ili asikamatwe. Ndio Kusema kua kama Red Brigade ingekua imeimarishwa toka awali basi mlipuaji ama asingepata nafasi ya kulipua, au hata kama angepata basi asingefika mbali bila ya kukamatwa. Sio Kundi jipya ndani ya CDM na lilikuwepo muda mrefu tu sema tu halikua limetangazwa rasmi kama lipo.

Red Brigade ya Italia V/s Red Bregade ya CDM
Hapa ndipo uwezo wa viongozi wetu wa siasa unapotakiwa kutiliwa shaka. Eti Dr. Slaa alisoma Italia ambapo Red Bregade ipo so atakua ndio yeye alioianzisha CDM na zina uhusiano. Yaani kwakua kuna mtu alikua Uingereza Miaka fulani ya Nyuma kwa shughuli zisizohusu Mpira wa Miguu na alivyorudi Tanzania akawa mmoja wapo ya walioanzisha Sunderland S. C. (sasa Simba S. C.) basi ni wazi kua timu hizi za Sunderland ya Uingereza na ya Tanzania zinahusiana!! Huu ni upotoshaji wa hali ya juu na ni kuwafanya Watanzania mazuzu ambao wanaweza kusikiliza kila uongo na wakauamini.

Kuna Manchester UTD ngapi hapa nchini? Chelsea je? Pita mitaa ya shule za Magomeni nyakati za jioni utakuta timu kibao za vijana zenye majina ya timu za nje, je na hawa wana uhusiano na hizo timu za nje? Au mkuu LiverpoolFC una uhusiano wa moja kwa moja na hii timu huko kwa malkia?

GREEN GUARDS
Hapa tunafanyana watoto tu. Kwa mujibu wa http://oxforddictionaries.com/definition/english/guard
[h=3] verb
[/h] [with object]
  • 1watch over in order to protect or control:two men were left to guard the stockade the gates were guarded by soldiers

  • watch over (someone) to prevent them from escaping:his task was to help guard Japanese prisoners

  • Basketball stay close to (an opponent) in order to prevent them getting or passing the ball: when a player is so closely guarded he cannot pass the ball

  • 2protect against damage or harm:the company fiercely guarded its independence

  • [no object] (guard against) take precautions against:farmers must guard against sudden changes in the market

ambapo kwa lugha rahisi ni Ulinzi, walinzi, kulinda e.t.c

Green Guards ni walinzi wa kijani kwa kifupi. Sasa walinzi wanalinda nini hawa? Obviously ni dhana ile ile ya Red Brigade ya CDM ya kukilinda chama na viongozi wake kwenye mikutano mbalimbali na nje ya mikutano.

Haieleweki ni kwa vipi shughuli na uwepo wa Red Brigade uwe ni haramu, lakini wa Green Guards uwe halali. J. Kikwete, Tendwa, Saidi Mwema, na wengineo wawe fair tu katika hili. Haihitaji kuongea kimipasho kua Red Bregade ni haramu bila kufikiria kwanza hata wewe kama mwenyekiti unahusika na chama kumiliki Green Guards yenye malengo sawa na Red Bregade. Tena kwa dini yako na huu mwezi mtukufu utakua unashinda na njaa tu M/Kiti A/Jeshi wa nchi kuendelea kusisitiza uharamu wa Red Bregade bila kufikiria kwanza kuvunja Green Guards.
 
Last edited by a moderator:
Mada nzuri sana na inaeleza ubovu wa militarization of part politics. Shida ni sisi wenyewe kukubali daima kutatua matatizo kwa njia ya kuangalia matokeo badala ya kuangalia kiini cha matokeo. Kote duniani iwe ni huko kwa Putin, kwa Hitler na Musolini na kwa sasa kwa JK na Mbowe, hakuna hata mara moja militarization ilileta amani ila shari tu. Ajabu ni pale tunapokumbatia mifumo mibovu na tukiwa wenyewe tunaona ni baraka iki-backfire kwa njia ya pili tunasema ni hatari kwa usalama wa nchi. Kimsingi Red Brigade ni effect ya Green Guard kwa hiyo tukitaka kufuta Red Brigade lazima kwanza tufute Green Guard halafu tujadili nani anatumia nani katika uhalifu huu wa kisiasa.

Kwa mujibu wa matukio machache yaliyotokea, uamuzi wa CDM kuanzisha Red Brigade tena kwa matangazo ya nguvu, ni lazima mwangwi wa hofu usikike. Rwakatare and the patner ni mfano hai unaobeba hofu kuu. Watz kwa uzoefu mdogo uliopo, RB haitakuwa na jema kwa sababu CDM hakijawa matured kuweza kuhimili negative effects za RB. Mifano ipo mingi tu ikiwemo ya namna chama kilivyoshindwa ku harmonise na ki maintain discipline ya wabunge wake
 
Unajua mnapokuja huku na hoja hafifu mkiwa misukule badala ya watu wanaotambulika, mnafanikiwa sana kuepuka aibu kubwa huko mbeleni kwani rekodi zitaonyesha dhahiri kwamba you chose the wrong side of history; kama mngekuwa sio misukule humu hakika msingekuwa mnajadili mnayojadili kwani hata watoto wenu wangewashangaa sana mnawatengenezea taifa la namna gani;

Pole sana mkuu, kwani kama signature yako inavyosema, sio kosa lako, "system is at work";

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

ushauli tuu, usimjibu! atakuharibia siku bure, wazungu wana msemo never argue with...
 
Yericko Nyerere, standtruth, kasimba g, et al,

Nimeonelea nirudi kujadili baadhi ya hoja zenu muhimu zinazosisitiza juu ya mapungufu ya hoja yangu katika bandiko namba moja; lakini kabla ya yote, nadhani nimeeleweka kwenye bandiko namba moja nilikuwa nina nia gani kwani hili niliweka wazi kabisa, hasa kuhimiza kwamba lengo langu sio kujadili upande upi upo sahihi bali kutoa a historical account juu ya domestic forces mbalimbali ambazo zilitengeneza mazingira ya militarization of party politics, kisha to set a stage for a discussion juu ya wapi tuende, hasa baada ya kuelewa juu ya tatizo la kuwa external oriented katika kujadili suala husika - yani kuepuka kujadili kwa kuangalia jinsi gani vyombo husika vili emerge nchi za wenzetu badala ya kuangalia jinsi gani hilo lilitokea nyumbani; ni kwa mantiki hii nikajadili pia kwamba chama cha kupigania uhuru (TANU) kimeacha a movement legacy ambayo imekuja kuwa emulated na chadema nyakati hizi kutokana na ukweli kwamba pamoja na malengo yake mazuri, TANU haikuweza kumaliza kazi yake to empower wananchi - economically, socially and politically; ni katika muktadha huu, naomba nisisitize tena historia ni kama inajirudia kwani wananchi walio wengi wanalilia for the "second independence", huku chadema sasa wakiwa katika position ya TANU, huku to a certain extent, CCM ikiwa katika position ya mkoloni, hence the deepening hostility between ccm and chadema inayopelekea kukua kwa tatizo la national insecurity and instability kutokana na a serious gap in the functioning of the national security system ambayo it is increasingly becoming deprofessionalized and politicized; Swali linalofuatia ni je:

Solution ni nini, chadema waendelee na uamuzi wao au ccm ibadilike?

Hili ni swali la msingi lakini nitakuwa mwongo kama nitasema nina majibu; sana sana nina maoni yangu ambayo nitaendelea kuyatoa kwa jinsi mjadala huu utakavyoendelea;

That said and done, naomba nijadili kidogo juu ya historia ya mfumo wa kisiasa Tanzania; ingawa inawezekana baadhi yenu msione relevance yake na mjadala husika, nina amnini itasaidia angalau wachache kwa matumizi ya 'terms of reference' hata huko mbeleni; Sehemu kubwa wa yafuatayo ni elimu niliyopata kwa kujisomea makala na vitabu mbalimbali kuhusiana na historia ya nchi yetu, kwa mfano kazi za Dr. Max Muya, wa idara ya siasa UDSM na wengine wengi;

Tanganyika ilikuwa nchi ya vyama vingi wakati wa uhuru 1961; Taifa lilirithi katiba ya mfumo wa vyama vingi;vilikuwepo vyama vikuu vinne:

1) TANU
2) UTP (cha serikali ya mkoloni)
3) ANC (Zuberi Mtemvu)
4) AMNUT

Baada ya uhuru, vyama vingine vitatu vya siasa vilisajiliwa baada ya uhuru (kati ya 1962 na 1963):

1)People Convention Party (PCP)
2)African Independence Movement (AIM)
3)Peoples Democratic Party

Kwa vile mjadala huu unaegemea zaidi siasa za Tanzania bara, sitajadili vyama vya siasa vilivyokuwepo zanzibar zaidi ya kuvitaja (ASP, ZNP, ZPPP na UMMA); Pia nadhani sina haja ya kujadili kwanini taifa likaamua kufuata mfumo wa chama kimoja kwani sababu hizi zipo in the open, lakini kwa wale wasioelewa hili ni kama ifuatavyo kwa kifupi:

Kwanza - ilionekana kwamba, vyama vya TANU na ASP ndio vyama halali vya umma - yani vilikuwa ndivyo vyombo halali na vya uhakika vilivyounganisha nguvu ya umma na taifa - yani vyama vya wafanyakazi, wakulima, ushirika na vikundi vingine vya kiraia katika mapambano dhidi ya ukoloni na usultani ili kuleta uhuru; Pili, iliaminiwa kwamba mara tu baada ya uhuru, uongozi mpya wa wazalendo ulikabiliwa na tishio la mgawanyiko wa taifa katika misingi ya ukabila, udini, rangi na majimbo; ili kuondokana na hatari hii, ikaonekana ni muhimu kitovu cha madaraka nchini kuwa chini ya "chama" badala ya "bunge";

Ili kukamilisha lengo hili, mikakati na mbinu mbalimbali ya "kisheria" na "kisiasa" ilitumiwa kukiwezesha chama (TANU baadae CCM) kudhibiti utawala wa nchi;TANU ilikuja na mbinu kuu sita kufanikisha lengo husika:

1) Kudhibiti vyama vya wafanyakazi
2)Kudhibiti wakulima, wafugaji na vyama vyao (ushirika)
3) Dola
4)Utumishi Serikalini
5)Vyombo vya habari
6)Vyombo vya ulinzi na usalama

Ningependa kujikita katika eneo relevant na mjadala huu yani eneo namba sita hapo juu:

Madaraka ya TANU (later CCM) katika kudhibiti utawala wa nchi yalikuwa strengthened zaidi kwa kuunganishwa kwa vyombo vya dola, hasa majeshi ya ulinzi na usalama; hii ilienda hand in hand na kueneza mafunzo na nidhamu ya kijeshi; hatua ya kuunganisha chama na vyombo vya usalama zilianza 1964 baada ya a mutiny attempt;kufuatia this attempt, jeshi likavunjwa;

MUHIMU:
Wakati wa kuliunda upya jeshi, uandikishaji wa wanajeshi wapya ulitegemea uanachama wa TANU au Umoja wa Vijana (TYL); vigezo hivi vilitumika kwa ajili ya ajira katika vyombo vingine vya ulinzi wa raia - polisi, magereza na UWT; kufuatia hatua hii, watendaji wote katika vyombo hivi walipatiwa mafunzo ya itikadi ya chama kupitia mpango wa "elimu ya siasa"; kazi hii ilisimamiwa na makamisaa wa chama; ili kutumiza malengo yake ya kudhibiti utawala wa nchi, TANU ilifanya mabadiliko kadhaa katika katiba yake;kwa mujibu wa mabadiliko hayo, majeshi ya ulinzi na usalama yalifanywa kuwa MKOA wa chama Kiuongozi;Kwa hali hiyo, majeshi hayo yakaingizwa katika muundo wa chama kitaifa; hii ni sehemu ya sababu kwanini katika kipindi hicho hicho, sekretarieti ya chama ngazi ya taifa kwa mara ya kwanza ikaunda "Tume ya ulinzi na usalama"; Tume hii iliundwa kwa madhubuti kabisa on merit ya wajumbe wake - viongozi wakuu wa chama na serikali ya TANU na maafisa wa ngazi za juu katika vyombo vya ulinzi na usalama walikuwa ni among members wa tume hii;

Ni rahisi kuona kwamba chini ya muundo huu, chana kiliweza kudhibiti vilivyo vyombo nyeti vya dola na kwa njia hiyo, cgama kiliweza kutawala na pia kurekebisha na kusimamia nidhamu katika sekta nyingine za jamii easily;

Pia kuingiza vyombo vya ulinzi na usalama katika siasa kulifuatiwa na uteuzi wa wanajeshi kushika vyeo vya kisiasa; wanajeshi walipewa ruksa kugombea nafasi za kisiasa katika chama na vyombo vya dola;

MUHIMU:
Vile vile, jamii kwa ujumla wake iliingizwa katika mfumo wa kijeshi na kwa hali hii, ikawa rahisi kuthibiti taifa kwa amri (badala ya majadiliano) kama ilivyo suala la nidhamu ndani ya vyombo vya usalama; ilipofika mwaka 1971, mpango kabambe wa kuimarisha ulinzi wa umma ukaanzishwa;kwa mfano, kila mtu mzima raia wa Tanzania alitakiwa kuhudhuria mafunzo ya mgambo yaliyoendeshwa na maafifa wa JWTZ; pamoja na malengo ambayo pengine yalikuwa mazuri, athari ya hatua hii ikawa ni pamoja na ujenzi wa jamii ya raia wanaopokea amri kutoka juu bila ya kushiriki katika majadiliano;katika kuimarisha mtindo huu, maafisa wa chama walipatiwa mafunzo katika shule za kijeshi/intelligence na baadae walitakiwa kuripoti katika ofisi za chama;

Kwa kuhitimisha, kuna umuhimu wa kutambua historia ya nchi yetu inatueleza nini kuhusiana na mbinu na mikakati iliyotumiwa na ccm enzi ya mfumo wa chama kimoja, kuthibiti na kuendesha taifa, hasa suala zima la vyombo vya ulinzi na usalama; Ni imani yangu kwamba tukichanganya hoja zangu za bandiko namba moja pamoja na hoja za bandiko hili, tutakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuelewa kwa kina suala zima la militarization of party politics chini ya mfumo wa chama kimoja, madhara yake chini ya mfumo wa vyama vingi, na nini kifanyike kulinusuru taifa na machafuko;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Please Bw Mchambuzi, I always admire the way you critical analyze things here on JF. The problem is that very few CCM members inside here would never understand what you have said. CCM are obsessed with CDM's growing popularity and they would ignore posts like this. Please endelea kuwaelimisha maana sasa hivi watu wanaelewa zaidi na wengi wameshagundua kuwa mambo yanawezekena bila CCM.
 
Asante sana mkuu,

Sasa umenirejesha kwenye tafakuri kuu,

Ngoja nipitie kwa umakini kisha nitarudi,

Lakini kama itapendeza hii post uiunganishe na mada kuu pale juu!

Nadhani itakuwa bora zaidi
 
Back
Top Bottom