Asili Ya Green Guard Ya CCM na Changamoto Kwa CHADEMA

Mada nzuri sana na inaeleza ubovu wa militarization of part politics. Shida ni sisi wenyewe kukubali daima kutatua matatizo kwa njia ya kuangalia matokeo badala ya kuangalia kiini cha matokeo. Kote duniani iwe ni huko kwa Putin, kwa Hitler na Musolini na kwa sasa kwa JK na Mbowe, hakuna hata mara moja militarization ilileta amani ila shari tu. Ajabu ni pale tunapokumbatia mifumo mibovu na tukiwa wenyewe tunaona ni baraka iki-backfire kwa njia ya pili tunasema ni hatari kwa usalama wa nchi. Kimsingi Red Brigade ni effect ya Green Guard kwa hiyo tukitaka kufuta Red Brigade lazima kwanza tufute Green Guard halafu tujadili nani anatumia nani katika uhalifu huu wa kisiasa.
 
wala hakuna haja ya kuandika stori ndeefu...hapa kuna tofauti....mbowe anasema wanaunda vikosi vya ulinzi..na usalama kwa chama chao kwani hawana imani na mapolisi na wanajeshi wa Tanzania.....hivyo wanaunda jeshi lao kuwalinda......
hapa utaona wanaunda jeshi....kwani hawana imani na vikosi vya Tanzania vilivo rasmi....huuu ni uhaini.....na kutaka kufanya fujo....sasa ikitokea la kutokea kwanye ulinzi wao....then hao walinzi watakua na majukumu gani? wakikamata mhalifu...watamchukulia hatua gani....wanampeleka wapi ? au watamhukumu wao wenyewe?
tunakumbuka kule zanzibar ccm ilitumia vikoso kama hivi vilivojulikana kama janjaweed...matokeo yake ni kuvamiwa na kupigwa kwa raia ovyo.....hatimae ....watu waliuliwa bure...kule znz

tofauti na vikosi vya ccm au cuf...wao bado wanaweka mamlaka ya ulinzi na sheria kwa majeshi yetu
hapa tujihadhari na uanzishwaji wa interharamwe na janjaweed ambao watakuja kuvuruga amani ya nchii hii
 
Kasheshe,

Mchambuzi
Ni kwa bahati mbaya sana analysis yako haijakamika... Mfano inashindwa kuonyesha kwamba kuna vyombo halali vilivyoanzishwa kisheria na kikatiba kuziba mapengo ambayo yalikuwepo kabla ya Uhuru. Vyombo hivi vimeanzishwa miaka ya 60/70 etc Nimeshavitaja hivyo vyombo. Hivyo basi nadhani iwe CCM au CDM au mwingine kuanzidha chombo rasmi cha ulinzi lazima viwe registered kwa sheria za sasa... Maana hata Vikundi kama NGO zina-be registered na kama chama au vyama vitaweka baysna vikundi vya ulinzi kwenye katiba zao lazima vyombo husika viridhie.

Sikuwa na lengo la kuleta analysis kamilifu zaidi ya kuelezea chanzo cha militarization of party politics in Tanzania kwa kuanzia ili kuweka mambo sawa kwa mujibu wa historia ya siasa za nchi yetu, hasa kwa kuanzia na the movement legacy under the then TANU nationalists;baada ya presentation hiyo, lengo langu ni kuhakikisha tunafanikisha mjadala sote kwa pamoja ambao unazingatia ni wapi tumetoka na militarization of party politics kama nilivyojadili na wapi tuelekee kama taifa; vinginevyo una hoja za msingi sana lakini zinahitaji kwanza kujua the root cause ya suala husika, suala ambalo ndio maudhui ya mada yangu;

Lakini nchi hii si ina Bunge na vyama husika ndio vinara kwenye hilo Bunge? Kama ni muhimu kila taasisi iwe na jeshi lake basi sheria itungwe labda iwe taasisi yoyote kwanini vyama tu?

Kutokana na legacy iliyoachwa na vyama vya ukombozi, itakuwa ni vigumu sana kwa vyama vya siasa africa to transform kutokea political movement kuwa political party;hata ccm haijakamilisha mchakato wake wa kuwa a complete political party, bado kina elements za a political movement;nitarejea baadae kufafanua hili na madhara yake kwa siasa za nchi;
Mwisho
Acha kuwasemea CDM; categorically they said wanataka ulinzi mbadala na sio under BAVICHA bali under CDM hayo mengine ya kwako mkuu...

It extremly wrong kulinganisha mazingira ya before uhuru yaani chini ya serikali ya kikoloni na wakati nchi ikiwa chini ya serikali iliyo chaguliwa kimokrasia... These are two different environments.

Ni muhimu uelewe kwamba kazi ya ukombozi iliyianzishwa na TANU haikukamilika, vinginevyo vyama kama chadema visingekuwa na prominence nyakati hizi; kwa mtazamo wa wengi, ikulu ya mkoloni na ikulu ya baada ya mwalimu kung'atuka haina tofauti ya maana linapokuja suala la prosperity ya wananchi walio wengi (vijijini) na wale wanaokimbilia mijini kutafuta maisha;;ni kwa mantiki hii, ndio maana historia ni kama inajurudia, na kwa bahati mbaya au nzuri kutegemea unajenga vipi hoja, wahanga wa marudio haya ya historia ni chadema;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ni mada nzuri sana na mchango wako ni maridhiwa. Ningeweza kwenda na kuangalia upande mwingine Umkhotowesizwe iliyoanzishwa na vijana wa ANC chini ya Nelson Mandela. Je, ilikuwa sahihi kwa ANC kuamua kujilinda na kuanzisha kikosi chake hicho?
 
Karibu katika mjadala mzee mwanakijiji; kwa mtazamo wangu, ilikuwa ni sahihi kwani kazi ya ukombozi ilikuwa ni a risky business and a threat kwa watawala na watawala walihakikisha wanaikabili ANC na agenda yake, come what may;Hapa nyumbani, harakati za ukombozi ziliachwa njiani na TANU baada ya watawala kuamua kujiunga na wanyonyaji;ni kwa mantiki hiyo, mazingira ya chadema yataendelea kuwa a risky business and a threat to the status quo;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hawali kwenye post namba moja ulipokuwa unatoa somo la historia umezungumzia masuala yafuatayo ambapo moja ya faida ya kuwa member wa youth league ya TANU ni kwamba wachilia mbali kuwa mlinzi bali lilikuwa ni daraja pia la kupeleka vijana kwenye ajira quote yenyewe ni hiyo hapo chini.

kwa vijana ambao hawakuwa na elimu ya kutosha ya kupata ajira katika bureaucratic structures za nchi, uanachama wa TANU Youth League ulikuwa ni fursa pekee, pia tiketi kwa vijana kujipatia immediate wages/salaries katika nafasi mbalimbali za chama na pia daraja la kupata promotion na ajira za mishahara serikalini baadae;
Kwa maana hiyo logic has it kama kulikuwa na internal hierarchical progress maana yake hao vijana walikuwa zaidi ya walinzi bali wengi walianza kama walinzi wa chama na kuweza ku-progress within the party and into other sectors of the government under one party rule. To me it sounds like that process entails furthering their education hili waweze shika nafasi zingine za serikali if that was the case maana wengi umesema walianza wakiwa hawana elimu.

Kwa maana hiyo msomaji anaweza sema hujaitimisha malengo yote ya hawali ya youth league ya wakati hule ambayo imeendelea kuwa tamaduni ya CCM mpaka leo kwamba lilikuwa ni chimbuko pia la viongozi wao. (tukitoa matumizi mabaya ambayo wanasiasa wenye nia mbaya leo wanavyokitumia)

On the other hand hiki cha CDM kinaenda kuzaliwa chini ya nchi huru na yenye law enforcement bodies ambayo inatambulika kikatiba na kwa CDM baada ya karibu miaka ishirini ya chama cha demokrasia na maendeleo kuzaliwa. Mwenyekiti wao ametamka wazi nia na madhumuni ya hawa ni for security reasons only, citing intolerable police misconduct during their public rallies and the need to protect them and their followers.

Here comes the conundrum which might exist in any sovereign state ambapo polisi ndio chombo cha usalama. Mfano CDM wanafanya mkutano fujo zinatokea labda tuchukulie NCCR imeweka mapendekizi wavuruge huo mkutano. Jamaa wao wa red brigade wanatoa kibano unataka polisi wawaangalie tu wakati wao wanajukumu la kulinda nchi kikatiba, na polisi wakiingilia jamaa CDM wana haki ya kurudisha makombora nao kwakuwa huo ni mkutano ama vipi.

Maana wasije kujianzishia mambo halafu baadae waje kulalama wanaingiliwa wakati shughuli za ulinzi zinajulikana ni jukumu la nani popote duniani. Na zaidi exactly were are the limitation of red brigade hili suala linahitaji ufafanuzi zaidi kutoka kwa viongozi wa CDM, maana kwa kusema awa waamini polisi tena na ivyo inaamua kujenga walinzi wake hilo halizui polisi kutoa kibano kwa hao jamaa inapobidi.

Maana sidhani kama waturuhusiwa kuwa na silaha zao or else tutakuwa tunaruhusu kila mtu kujilinda maana hata mimi naweza sema siiamini polisi na nipewe mtutu wangu tu jamaa wakisogea nijilinde ndio mwanzo wa anarchy yenyewe, no wonder the police force was thought to be a solution to avoid such problems.
 
Kwa vile umeisoma kama "habari", kwa kweli sitarajii mrejesho wa maana yoyote kutoka kwako;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Ingekuwa ina maana ningechangia, sikuona maana hata chembe ndio maana nikakueleza kuwa maudhui ni kiduchu, ungeweza kuiandika yote kwa mistari mitatu tu.
 
Thank you! Now we know where we are coming from, where are we are... Should we then chat our way forward....

Naomba mvunge yeyote wa chama chochote apeleke mswaada wa marekebiisho ya sheria husika ya usslama wa raia... Kuongeza clausee hii hapa....

"Ni marufuku chama chochote cha siasa kuwa na kikundi au vikundi vya ukakamavu, ulinzi au self defence katika jamhuri ya muungano" vikundi vinavyoruhusiwa ni vya ujasiria mali, kijamii social groups na vya namna hiyo.

NAWASILISHA....

Naomba muboreshe hiyo clause... Itumwe kwa mh. Spika haraka sana.
 
Ingekuwa ina maana ningechangia, sikuona maana hata chembe ndio maana nikakueleza kuwa maudhui ni kiduchu, ungeweza kuiandika yote kwa mistari mitatu tu.
Seriously, tutarajie nini kutoka kwa Zomba zaidi ya vijembe, mipasho, kejeli na chuki za kidini?umuhimu wako kwa wahusika ni ku frustrate watu na kuvuruga hoja zenye mashiko, vinginevyo sio kawaida yako kuonekana kwenye mada ambazo haziwagusi you and I know who;Mtawapata the few ambao hawajawa trained to deal with people like you, sio sisi; Karibu sana kwenye mjadala kama msomaji kwani nikisema mchangiaji nitakuwa nimekosea sana kwani again nje ya kejeli, vijembe, mipasho na chuki za udini, kila mtu anajua zomba huwa hana hoja;

mwennyewe hii ndiyo umeiona hoja yenye maana na ukapoteza muda haswa kuiandika? Ungetumia mistari mitatu tu ingetosha. Pole sana, ukweli siku zote ni mchungu ndiyo maana ukaingiza na dini na ----- mwingine.
 
Mchambuzi upo sahihi sana katika kuelezea historia ya jambo lakini kwa upande wangu ni kama umeenda around the bush ili msomaji mwenyewe ndiye atoe conclusion.

Ukweli ni kwamba kila chama kina kikundi chake sina haja ya kuvitaja. Sasa kitendo cha CDM kusema kitakiimarisha kikundi hicho ndicho kilichozia taharuki kubwa mpaka rais kulitolea kauli jambo hilo.

Binafsi kama ungeenda mbali zaidi katika kujadili katika hili ungewasaidia sana akina Mwigulu na wenzake ambao wanamtazamo tofauti na kufanya mambo ambayo yanakichafua zaidi chama kuliko kukihenga jambo ambalo tayari umesema siyo lengo la mada yako.
 
Last edited by a moderator:
mwennyewe hii ndiyo umeiona hoja yenye maana na ukapoteza muda haswa kuiandika? Ungetumia mistari mitatu tu ingetosha. Pole sana, ukweli siku zote ni mchungu ndiyo maana ukaingiza na dini na ----- mwingine.

Unajua mnapokuja huku na hoja hafifu mkiwa misukule badala ya watu wanaotambulika, mnafanikiwa sana kuepuka aibu kubwa huko mbeleni kwani rekodi zitaonyesha dhahiri kwamba you chose the wrong side of history; kama mngekuwa sio misukule humu hakika msingekuwa mnajadili mnayojadili kwani hata watoto wenu wangewashangaa sana mnawatengenezea taifa la namna gani;

Pole sana mkuu, kwani kama signature yako inavyosema, sio kosa lako, "system is at work";

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Maelezo yako yanajichanganya na hayajitoshelezi

Funguka zaidi, vinginevyo kama unaielewa vyema historia ya nchi yetu kuanzia harakati za uhuru, ujenzi wa chama cha TANU kama taasisi ya kushika dola ya Tanganyika (baadae Tanzania) na hatimaye Kufanikisha chama cha mapinduzi kushika hatamu ya nchi, ungeelewa mantiki ya hoja yangu;tiketi ya kila kitu katika Tanganyika na baadae Tanzania ilikuwa ni chama; shughuli za taasisi yoyote katika dola ya Tanganyika na baadae Tanzania zilifuatana na maamuzi ya chama;Politics za TANU na baadae CCM zilikuwa supreme to everything including uraia, utu, uchumi, rationality, common sense, you name it; kilichosaidia hali kwenda shwari ni kwamba the end was justified, tatizo likawa kwenye means, lakini muhimu zaidi, kiongozi wa nchi never profited from politics;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu Mchambuzi, ningeomba uachane na wanaovuruga mjadala!! Binafsi nimefurahia ujumbe wa uzi wako, isipokuwa kuna sehemu nadhani zitaendelea baadae...maana kama ni paper basi hiyo uliyotoa ni kama sehemu ya introduction. I do expect you to open our mind on the objectives of the relevant group during the three errors 1) wakati wa kupigia uhuru, 2)baada ya kupigania uhuru, and 3)baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.
 
Funguka zaidi, vinginevyo kama unaielewa vyema historia ya nchi yetu kuanzia harakati za uhuru, ujenzi wa chama cha TANU kama taasisi ya kushika dola ya Tanganyika (baadae Tanzania) na hatimaye Kufanikisha chama cha mapinduzi kushika hatamu ya nchi, ungeelewa mantiki ya hoja yangu;tiketi ya kila kitu katika Tanganyika na baadae Tanzania ilikuwa ni chama; shughuli za taasisi yoyote katika dola ya Tanganyika na baadae Tanzania zilifuatana na maamuzi ya chama;Politics za TANU na baadae CCM zilikuwa supreme to everything including uraia, utu, uchumi, rationality, common sense, you name it; kilichosaidia hali kwenda shwari ni kwamba the end was justified, tatizo likawa kwenye means, lakini muhimu zaidi, kiongozi wa nchi never profited from politics;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Cheki na Mwigulu akupa data za kutosha ,halafu ndio uje kivingine hapa kwa sasa uko sharo sana unapotosha tuu
 
Cheki na Mwigulu akupa data za kutosha ,halafu ndio uje kivingine hapa kwa sasa uko sharo sana unapotosha tuu

Sasa nimekusoma, upo kimwigulu zaidi ingawa sijakuelewa iwapo una maana nipo kisharobaro au una maanisha shallow;

Sina haja ya kucheki na mwigulu kwani sidhani kama ana data zozote ambazo nazihitaji kufanikisha maudhui ya mada yangu; Kama hoja yako (na pengine ya mwigulu)ni kwamba hapa kuna upotoshaji, kumbuka kwamba nimem tag mwigulu katika bandiko namba moja hapo juu, hivyo ana fursa ya kuja humu to challenge hoja yeye kama mwigulu, lakini pia wewe kama mmoja wa watu belonging to his school of thought kama unavyojitambulisha; wakati tunamsubiri mwigulu, kwanini usije na hoja zako per hizo data ulizoziona kwake au una ulazima wa kusubiri ruksa ya mwigulu?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mchambuzi
Ni kwa bahati mbaya sana analysis yako haijakamika... Mfano inashindwa kuonyesha kwamba kuna vyombo halali vilivyoanzishwa kisheria na kikatiba kuziba mapengo ambayo yalikuwepo kabla ya Uhuru. Vyombo hivi vimeanzishwa miaka ya 60/70 etc Nimeshavitaja hivyo vyombo. Hivyo basi nadhani iwe CCM au CDM au mwingine kuanzidha chombo rasmi cha ulinzi lazima viwe registered kwa sheria za sasa... Maana hata Vikundi kama NGO zina-be registered na kama chama au vyama vitaweka baysna vikundi vya ulinzi kwenye katiba zao lazima vyombo husika viridhie.

Lakini nchi hii si ina Bunge na vyama husika ndio vinara kwenye hilo Bunge? Kama ni muhimu kila taasisi iwe na jeshi lake basi sheria itungwe labda iwe taasisi yoyote kwanini vyama tu?

Mwisho
Acha kuwasemea CDM; categorically they said wanataka ulinzi mbadala na sio under BAVICHA bali under CDM hayo mengine ya kwako mkuu...

It extremly wrong kulinganisha mazingira ya before uhuru yaani chini ya serikali ya kikoloni na wakati nchi ikiwa chini ya serikali iliyo chaguliwa kimokrasia... These are two different environments.

Mkoloni hakuwahi kuwatesa watanganyika kwa kuwang'oa kucha na meno bila ganzi.

Kitu cha ajabu sana nyie maccm huwa hamtaki kukubali kuwa Kuna upungufu mkubwa katika uendeshaji wa jeshi la polisi na hivyo kuishia kushauri kuwa hao polisi wanaolalamikiwa waendelee kuwalinda wanaowalalamikia. Mapungufu ya kiulinzi kwa polisi kutumika kisiasa ndio yamepelekea vyama kufikiria ulinzi kwa mapana zaidi.
 
Mchambuzi kuna vitu vingi ambavo labda wewe huvijui juu ya TYL na mtililiko wa mambo katika nchi yetu! Kwanza grooming ya UWT in relation TYL na baadaye UVCCM! Kimsingi kuna watu waliokuwa grromed kuchukua posti TISS wakati simply walikuwa wanachama waaminifu wa TYL and UVCCM, lakini jambo hili kwa siku za usoni linaweza kuleta matatizo kwakuwa TISS hao fautishi majukumu accordingly! Yeah umefanya literature review vizuri, lakini realities zinakuwa concealed sijui ni kwa kuprotect interesti za nani!

Ajira za the then TYL ambao wakawa groomed to vyombo vya usalama ndio wanaosababisha kero hawajui wamtumikie master yupi, je wamtumikie aliewasababishia ajira yaani CCM? au wawatumikie wananchi!

Mkuu hapa ulikuwa unaelekea kwenye kiini cha tatizo haswa. Historia ya Mchambuzi ni swa lakini ameshindwa pia kugusia uhusiano wa Chama tawala na vyombo vya usalama hasa wakati wa Chama kushika hatamu. Tukijikita kwa historia ya TYL na kisha kujielekeza kwenye siasa za Chama kimoja na chama kushika hatamu tunaweza kupata jibu.
 
Last edited by a moderator:
wala hakuna haja ya kuandika stori ndeefu...hapa kuna tofauti....mbowe anasema wanaunda vikosi vya ulinzi..na usalama kwa chama chao kwani hawana imani na mapolisi na wanajeshi wa Tanzania.....hivyo wanaunda jeshi lao kuwalinda......
hapa utaona wanaunda jeshi....kwani hawana imani na vikosi vya Tanzania vilivo rasmi....huuu ni uhaini.....na kutaka kufanya fujo....sasa ikitokea la kutokea kwanye ulinzi wao....then hao walinzi watakua na majukumu gani? wakikamata mhalifu...watamchukulia hatua gani....wanampeleka wapi ? au watamhukumu wao wenyewe?
tunakumbuka kule zanzibar ccm ilitumia vikoso kama hivi vilivojulikana kama janjaweed...matokeo yake ni kuvamiwa na kupigwa kwa raia ovyo.....hatimae ....watu waliuliwa bure...kule znz

tofauti na vikosi vya ccm au cuf...wao bado wanaweka mamlaka ya ulinzi na sheria kwa majeshi yetu
hapa tujihadhari na uanzishwaji wa interharamwe na janjaweed ambao watakuja kuvuruga amani ya nchii hii
wale wa wacha kudanganya watu wewe, mbona hujasema kuhusu Green Guard
 
Back
Top Bottom