UZUSHI Asec Mimosas imeomba mechi ya marudiano na Simba ifanyike kwa Mkapa

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu habari,

Hii habari ya Asec Mimosas kuomba kutumia uwanja wa Mkapa kwenye mechi yao ya marudiano dhidi ya Simba kwenye ligi ya mabingwa Afrika ina ukweli wowote?

1707641595970.jpeg

 
Tunachokijua
Ligi ya mabingwa Afrika (CAF Champions League) ambayo ni mashindano ya kila mwaka ya kandanda yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na kuvikutanisha vilabu bora zaidi barani Afrika. Ndiyo mashindano ya kandanda yenye hadhi zaidi ya vikombe vya vilabu vya Afrika.

Baada ya hatua ya kufuzu kwenda kucheza makundi ya ligi ya mabingwa kumalizika na Klabu ya Simba kuwa miongoni mwa vilabu vilivyofuzu kucheza hatua hiyo, Simba ilipangwa kundi B ikiwa na vilabu vingine 3 ambavyo ni Asec Mimosas, Wydad SC na Jwaneng Galaxy.

Mechi za makundi zilianza 24, 11, 2023 ambapo 25, 11, 2023 Simba ilicheza mechi yake ya kwanza na Asec Mimosas katika uwanja wa Benjamini Mkapa maarufu kama Uwanja wa Taifa na kuibuka na sare ya kufungana goli moja kwa moja. Katika hatua hiyo Simba Inatarajia kucheza mechi ya marudiano na Asec Mimosas tarehe 23, 02, 2024.
IMG_7675.jpeg
Je, Asec Mimosas wameandika barua ya kuomba kucheza mechi yao ya marudiano na Simba katika uwanja wa Benjamini Mkapa?
Baada ya kusambaa kwa uvumi huo kwenye mitandao mbalimbali, JamiiCheck imewasiliana na Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo ambaye alikanusha kuwepo kwa taarifa hizo na kudai kuwa ni uzushi tu kwani uwaja hauombwi TFF kama taarifa zilivyodai kwa kuwa hayo ni mashindano ya CAF.

Nao baadhi ya wadau ndani ya Simba walipoulizwa walidai hizo ni propaganda tu a hakuna ukweli kuhusu taarifa hizo.


Pia mwandishi wa habari za michezo wa Ghana Micky Jr alichapicha kwenye ukurasa wake wa X akisema mechi kati ya Simba na Asec Mimosas itachezwa nchini Ivory Cost.

1707640970324-png.2900589
Hivyo JamiiCheck imejiridhisha bila shaka kuwa Asec Mimosas hawajaomba kutumia uwanja wa Mkapa kwa mechi yao dhidi ya Simba na kwamba taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii ni za uzushi.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom