Asanteni JamiiForums, hatimaye nimeanzisha mradi wangu lakini bado changamoto zipo!

Pawaga & Mama Joe: Halafu kitu kingine muhimu nimekikumbuka asubuhi hii:

Hakikisha kabla ya kutoa chanjo ya mdondo (newcastle disease) kuku wako hawana virusi vya huo ugonjwa. Kwa nini?
Chanjo ya mdondo ina hali ya kama uwepo wa virusi vyenyewe kwenye dawa kwa hiyo unapompa kuku inazalishwa kinga kubwa kwenye mwili na hivyo unapokuja ugonjwa huo kuku anakuwa na kinga ya kutosha.

Ndio maana kuku aliyewahi kuugua mdondo na akapona hawezi kupata tena ugonjwa huo kwa sababu kinga ilishajitengeneza ndani ya mwili.

Kwa hiyo utakapompa kuku chanjo wakati tayari ana virusi mwilini mwake maana yake dawa itachochea uzalishaji mkubwa wa virusi na kuku hatachukua muda kuishi. Ndio maana kuna watu wana dhana kwamba dawa ya chanjo inaua kuku kumbe si kweli.

Unafanyaje au utajuaje kuku wako hawana mdondo ili uwape dawa?
Kwa kawaida huwezi kutambua kwa haraka kwamba wana ugonjwa mpaka watakapoonyesha dalili which is too let. Utakachofanya ni kuwapa Antibiotic (kama fluban au Doxycol) kwa muda wa siku saba. Hapo bila shaka utakuwa umetibu dalili zote na kwa kuwa ulifululiza kuwapa kwa muda huo virusi vitazidiwa na kuisha. Baada ya hapo sasa wape kinga ya matone.

Nimeeleza hivi ili isije kutokea umeua kuku wako kwa chanjo ukasema Platozoom amechangia!!!!!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom