Asanteni JamiiForums, hatimaye nimeanzisha mradi wangu lakini bado changamoto zipo!

Pawaga

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
1,330
966
Habari wakuu?

Jamani mimi ni graduate niliyeamua kujiajiri kwa kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa mfumo wa NUSU HURIA, Wazo hili nimelipata humu humu na baada ya kusoma nikaamua kuliweka ktk utekelezaji.

Tayari nimeshajenga fensi ya senyenge ukubwa wa nusu ekali na mabanda ndani yake na kesho natarajia kuweka kuku 25 yan tetea 20 na jogoo 5 kama kianzio.

Huu mradi nauanza kama wa majaribio tu kwa kipind cha mwaka 1 ya mpaka Nov, 2013.

Niwashukuru sana kwa kusaidiana lakin bado nahitaj msaada wenu wa kujua DAWA muhim za kuwa nazo eneo la mradi kwa kuwa eneo hilo lipo mbali na mji hvyo siwez kuwa naenda mara kwa mara mjini kuchukua dawa...

Nawashukuru sana
 
Jogoo wengi sana kwani umewapima uwezo wao wa kuperform? Hongera sana sana and be blessed
 
Mmmmh hcho ni chakula gan?,ni kuku wa kinyej ninao-deal nao. Pia kwan wanatakiwa jogoo wangap kwa tetea hao?
 
Mmmmh hcho ni chakula gan?,ni kuku wa kinyej ninao-deal nao. Pia kwan wanatakiwa jogoo wangap kwa tetea hao?

Jogoo 1 kwa mitetea 10....lakini hakikisha wanakula vizuri.

Usichanganye jogoo mwenye undugu na mitetea

Banda liwe safi

Chanjo ya mdondo au newcastle wapewe na ni muhimu....kosa moja unaweza kuamka na kukuta kuku wote wamekufa
na hapa tumia ya matone na siku unapoinunua hakikisha unahifadhi kwenye ubaridi na uwachanje wote siku hiyo.

Antibiotic muhimu kuwepo (hizi zinahitaji hali ya kawaida)

Hakikisha banda unaweka dawa ya kuuua viroboto na utitri (akheri powder ni nzuri)

NB: Tumia chakula ulichoelekezwa acha madawa ya kukuza na kuku wa kisasa
 
Asante sana platozoom kwa ushaur bora,tatizo ni hzo dawa zinazohitaj ubaridi maana huku hakuna umeme pia ni mbali sana kutoka mjin(84 km) hvi cjui itakuwaje kwa hili,.nahitaji kujifunza zaidi ili uwe mradi bora na endelevu
 
Kuhusu dawa kwenye ubaridi - ukienda kununua wanakuwekea kwenye barafu. Waambie unakweenda mbali na utafika kabla haijayeyuka tukichukulia mwendo wa saa tatu hadi tano.

Mimi kuna kipindi huwa nanunua inakaa muda wa saa 12. Njia nzuri zaidi ni kwenda na chupa ya chai na kuomba hiyo dawa wakuwekee kwenye hiyo chupa na barafu. Kuhusu majogoo unaweza kuwapunguza wabaki wawili au watatu - ubaya wa kuwa na majogoo wengi ni kuwa badala ya kufanya kazi ya kupanda wanafanya kazi ya kugombania majike.

Mwisho usisahaau dawa ya minyooo kila baada ya miezi mitatu - kwa sasa usisubiri hiyo miezi anza kuwapa sasa kisha hesabu miezi MITATU. Ni vizuri tukajua uko mkoa gani kwa maana maelekezo mengine yanategemea uko wapi.

NAKUTAKIA MAFANIKIO MEMA.
 
Asante sana platozoom kwa ushaur bora,tatizo ni hzo dawa zinazohitaj ubaridi maana huku hakuna umeme pia ni mbali sana kutoka mjin(84 km) hvi cjui itakuwaje kwa hili,.nahitaji kujifunza zaidi ili uwe mradi bora na endelevu

Dawa ya matone nenda duka la madawa ya mifugo halafu watakupa kipande cha barafu ila uwe na themos, unatumbukiza barafu na kuiweka dawa yako ndani na kufunga chupa! mpaka kwenye banda lako.

Hizo nyingine za antibiotic hazina tatizo.
 
Omugurusi ubarikiwe sana ntapunguza jogoo wawili wabaki watatu tu. Pia mimi nipo iringa na ndipo mradi utakapoendeshwa,nimekupata kaka platozoom. Mmmmh tatizo ni capital ila napenda kama ningekuwa na tetea wengi zaida dada angu fistlady1. all in all nawashukuru sana wadau kwa mchango wenu.
 
Last edited by a moderator:
Salam zmefika mkuu,nipo itunundu. tutumie kiswhl ili tushare vzur na wote,.kwa utani na kikwetu pls tukutane kule chit chat ndugu yangu ngaliba
 
Jogoo wengi sana kwani umewapima uwezo wao wa kuperform? Hongera sana sana and be blessed[/QU asante mkuu,yah nlikuwa cjui ratio ya tetea vs jogoo but now nimepata kitu hvyo ntarekebisha uwiano huo,. Hii ndo raha ya JF yan elim unapata bureee wewe tu ushndwe kuapply,
 
hongera sana mkuu...hatua nzuri sana changamoto zipo kwenye kila biashara.kikubwa jitahidi kufuatilia chanjo na kinga pia jaribu kufuatilia kuku kwa karibu sana pindi unapoona tofauti kwa kuku yeyote ni vyema ukamtenga mapema iwezekanavyo na kumtibia.pia jitahidi mradi wako uwe kwenye 'documents' yani kumbukumbu ili iwe rahisi ufuatiliaji wa marudio ya chanjo.kila la heri.
 
Hongera sana kweli JF shule nzuri na bure, Jipe moyo utaweza tu, nilikuwa sijui ratio ya jogoo/mitetea, asante sana kwa hili somo.
 
big up kijana ila December inakaribia angalia usije ukawafanya vitoweo tu kuwa na discipline all in all ukiufanya serious huu mradi unalipa sana
 
Hapo ukitunza vizuri Pasaka mijogoo waweza piga bei ya buku 20
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom