Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma anashikiliwa na Polisi Mkoani Manyara kwa kosa la kusafirisha kinyume na sheria Wahamiaji 20 Raia wa Ethiopia.

Akiongea Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara ACP Lucas Mwakatundu amesema tukio hilo limetokea March 23 2024 ambapo gari hilo limekamatwa katika kizuizi barabara ya Arusha Babati eneo la Minjingu likiwa na Wahamiaji ishirini Raia wa Ethiopia kwenye gari namba T.774 BDL Land Cruiser likiwa na bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM.

“Gari hili V8 lilikuwa na Bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwenye upekuzi tulipoona sura tofauti na Watanzania ilibidi tuweke gari pembeni na baadae kuwashusha tukakuta wapo Wahamiaji 20 kwenye gari V8 na wote uelekeo wao ni kusini mwa Afrika wakitokea usawa wa Arusha, Dereva wa gari hili ni Mkazi wa Dodoma tunamshikilia mpaka sasa na kesho tunatarajia kuwakabidhi Uhamiaji”


Chanzo: Ayo TV
Hawa jamaa wa ethiopia hawajielewi , kwanini wasingekuwa wanasafiri wawili wawili kutumia mabasi mpk tunduma au kasumulu? Nasafiri sana ila sioni mabasi ya nyanda za juu kusini yakikaguliwa njiani kuangalia utaifa wa abiria.

Wanyasa wengi wanasafiri kutoka kyela kuja Dar bila ya vizuizi vyovyote njiani.
 
imagine ingekua ni gari ya CHADEMA, ungeweza kuandika hivi hivi? Ungesikia kesho msajili wa Vyama ametoa barua kwa CHADEMA kujieleza.
nilichoandika ni katika ujumla 🐒

sio tu ingekua Chadema hata ingekua CHAUMA, vyama na taasisi nyingine mbalimbali, ni kwamba uovu mwingi hivi sasa umejificha kwenye wema wa hizo taasisi au vyama, ukizubaa tu umelizwa 🐒
 
Hii ni Kawaida sana kwa baadhi ya watu ndani ya CCM nakumbuka Mdude_Nyagali aliwahi kusema hili mwaka 2022
Screenshot_20240325_085853_X.jpg
 
Back
Top Bottom