Arusha yawaka moto.

Wikiliki

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
528
139
Ndugu wana jf niko katikati ya jiji la Arusha,hali ya hapa si shwari magari ya polisi yakiwa yamejaa FFU yakiwa na bendera nyekundu huku yakipiga ving'ora yakiwa sambamba na lile la kumwaga maji ya kuwasha yanazunguka kila kona ya mji wa Arusha.
 
Moto wa nini sasa umewaka?
Kuna mtu amemwagiwa maji au nini?
Labda deployment za kawaida tu za askari?
 
IGP Mwema angalia huyo Andengenye analichafua geshi lako tukufu kwa kulazmisha mambo ya kijinga yanamwisho wake haya
 
Nini tena, waambieni kabisa hatutaki mambo ya Ivory Coast hapa....kwani mkutano ndio unalindwa na mabomu na vifaru? Polisi wetu hawajiamini
 
Polisi hawajui waht it means by peoples power. Watu wamechoka na ubabe hauwezi saidia kitu
 
Ni kweli kabisa, wanapita katika viunga vya mji wa AR ... FFU wakiwa katika fullu jezi za kupambana !!!! Yaani nikumaanisha hali si shwari gari la maji ya kuwasha, mabendera mekundu katika magari ya FFU, ngao , mabomu ya machozi viunoni na mavifaa kibao ......!!!!!

Vijana wa Andengenye wako tayari kwa mapambano na amri ameshaitoa tayari .......!!!!!! :A S-danger::A S-danger:
 
Polisi hawajui kazi yao
Polisi hawana elimu (zaidi ya ile form four failure)
Polisi wanapenda sifa za kijinga
Waliowatuma hawajui pia kazi yao na wapo kwa kulinda maslahi yao
Kweli tutategemea jema hapa?
Ya nini wazunguke na magari yao ya ajabuajabu, na mavazi ya kiroboti mitaani?
Ande ameletwa kufanya kazi maalum, na ndio hiyo anayo ifanya.
 
Sasa watampiga nani wakati watu hawana nia ya kufanya fujo?
Ndo zile za Mahita ya kuonyesha ma'short-gun kila siku kwenye media, bila wahusika kuwepo!
Anataka Media attention huyu!
 
Mijinga mikubwa hii, yaani haioni kuwa inatumiwa ili kuwaweka wajinga wenzao madarakani? afadhali nilikosa post ya polisi nisingeweza kufanya ujinga huu
 
The revolution will not be televised!! Fukuto za moto ujao. Sisi watanzania TUMECHOKA!! God Bless Tz and its True people!
 
Unajua hii TZ ni ya ajabu sana. Mji wa Arusha ni TOURIST town, sasa hizi tishia tishia za polisi hawaoni kuwa kuna impact kubwa kwenye sector ya utalii. Hamna njia nyingine mbadala ya kuhakikisha usalama pasipo hii aina ya vitisho?? Huu ni upuuzi afu eti tunasema tuna taka vutia watalii kwa namna hii jamani??
 
Wana JF hali haiko shwari Arusha mjini kwa kiwango ambacho watu wanakitegemea maana mjini kuna polisi wanapita na gari kubwa la maji ya kuwasha landrover mbili zikiwa zimejaa askari wa FFU na mapikipiki ya kutosha wanazunguka sehemu zenye watu wengi kama vile soko kuu stend na kwingineko.

Watu wengi wamekaa maeneo mbalimbali na hawajajikusanya rasmi ila wanaonekana kama ni watu ambao wanafanya shopping za kawaida lakini ukiongea kila mmoja wanasema wao wanasubiri Agizo kutoka viongozi wa CHADEMA watapokusanyika watawafuata huko hawaogopi hayo magari tena bora yaendelee kupita mitaani ili wayazoee wasije kuyaogopa tenana wengi ukiwaona ni kama vile wanawasanifu polisi

Jamani sijui uonevu huu utaendelea mpaka lini wandugu
 
Polisi hawajui kazi yao
Polisi hawana elimu (zaidi ya ile form four failure)
Polisi wanapenda sifa za kijinga
Waliowatuma hawajui pia kazi yao na wapo kwa kulinda maslahi yao
Kweli tutategemea jema hapa?
Ya nini wazunguke na magari yao ya ajabuajabu, na mavazi ya kiroboti mitaani?
Ande ameletwa kufanya kazi maalum, na ndio hiyo anayo ifanya.

Polisi, (wengi wao) ni mbumbumbumbu:painkiller:
 
Hii sasa ni hatari, kwani kuna hatari gani hadi askari waanze kuwatisha watu namna hiyo!!!
 
Back
Top Bottom