Arusha: Wanakijiji Arumeru walazimika kuvaa Ndoo na Helmets vichwani kujikinga na Mawe ya ajabu yanayorushwa hewani

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,847
15,262
Wanakijiji wa kijiji cha kiwawa kilichopo Arumeru wamelazimika kuvaa ndoo na kofia ngumu vichwani kufuatia mawe yanayorushwa usiku na mchana pasipo kujua mawe hayo Yanatokea wap.

Aidha wanakijiji hao wameshindwa kufanya shughuli zao za Kila siku zikiwemo za kujiingiza kipato kutokana na hofu ya kupigwa na Mawe hayo ambayo yamekuwa yakirushwa usiku kucha hadi mchana.

Baadhi ya wanakijiji wamejeruhiwa na. Mawe hayo kichwani na sehemu nyingi za mwili.

Hasara nyingine ni mawe hayo kutoboa mabati pindi yarushwapo, kuharibu viio vya milango na madirisha.

Hadi muda huu bado ufumbuzi wa tatizo hilo halijatatuliwa na wala kujua mawe hayo Yanatokea wapi.
 
Naishi hayo maeneo kwa karibu japokuwa hiyo njia naipitia mara moja moja sana ila hata leo jioni bodaboda wangu kaniambia hii story
 
Hizi ndizo hbr inapazwa wazungu wazikie waje kwa wingi kushangaa Jambo Hilo kamati ya royal tour mko wapi hii Ni pesa nzuri Sana tukifanya marketing serious na advertisement za kutosha lazm watu watafurika kushanga Jambo Hilo na nnchi yetu itakuwa popular mno
 
Naishi hayo maeneo kwa karibu japokuwa hiyo njia naipitia mara moja moja sana ila hata leo jioni bodaboda wangu kaniambia hii story

Hellow kaka mm nipo njiani now nakuja kwa ajil ya kuripot naomba mawasiliano yako ili niweze kufika huko njoo pm pse
 
Kuna umuhimu wa uchunguzi, kisayansi hapa. Polisi watujuze kwani inadaiwa walikuwepo huko, na ndoo kichwani.

Eneo kubwa kiasi gani? km 1 2 3...
 
Wanakijiji wa kijiji cha kiwawa kilichopo Arumeru wamelazimika kuvaa ndoo na kofia ngumu vichwani kufuatia mawe yanayorushwa usiku na mchana pasipo kujua mawe hayo Yanatokea wap.

Aidha wanakijiji hao wameshindwa kufanya shughuli zao za Kila siku zikiwemo za kujiingiza kipato kutokana na hofu ya kupigwa na Mawe hayo ambayo yamekuwa yakirushwa usiku kucha hadi mchana.

Baadhi ya wanakijiji wamejeruhiwa na. Mawe hayo kichwani na sehemu nyingi za mwili.

Hasara nyingine ni mawe hayo kutoboa mabati pindi yarushwapo, kuharibu viio vya milango na madirisha.

Hadi muda huu bado ufumbuzi wa tatizo hilo halijatatuliwa na wala kujua mawe hayo Yanatokea wapi.
View attachment 2234848

Kitu rahisi hicho, waokote mawe yote yaliyorushwa halafu wayanusishe kwa "sniffing dogs" mbwa walipewa mafunzo (mbwa wa polisi) kisha wawaachie hao mbwa wazagae maeneo hayo kutafuta harufu ya hayo mawe ili wajue yanatoka wapi na mtu gani anayarusha.----ila kama ni mambo ya visasi kwa dhuluma au uhalifu uliofanyika basi hapo lazima ifanyike toba nk,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom