JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Mgomo huo ulioibuka asubuhi ya leo Julai 3, 2023 baada ya madereva Daladala kudai kuingiliwa ruti na wenzao wa Bajaj, hatimaye wameyamaliza na usafiri unaratijiwa kurejea kama kawaida kuanzia asubuhi ya Julai 4, 2023.
Baada ya mazungumzo hatimaye maridhiano yamefikiwa kati ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) na madereva wa daladala.
Akizungumza na madereva waliogoma kwenye Stendi ya Kilombero, Afisa Mwandamizi wa LATRA, Amani Mwakalebela ametangaza kurejea kwa usafiri huo kutokana na maridhiano hayo.
Amesema kuanzia Julai 10, 2023 itakuwa mwisho wa Bajaj kwenda Mjini au kujihusisha na majukumu yanayofanana na daladala, badala yake wanatakiwa kukodishwa na si kukusanya abiria kama daladala wanavyofanya.
Hali ilivyo Kwa Morombo jijiji Arusha Kwenye mgomo wa Daladala usiokuwa na kikomo madereva wakilalamikia kuongezeka kwa Bajaji jijini Arusha na Kuwaingilia kwenye Ruti zao ambapo Wananchi wametumia usafiri wa Mguta, Julai 3, 2023 kuingia mjini.
Pia soma: Mgomo wa Daladala Jijini Arusha asubuhi hii ya Julai 3, 2023