Arusha Stadium kufurika 30/5/2015, Ni mkutano wa hadhara wa Lowassa

Status
Not open for further replies.
Uwanja wa Sheikh Abeid unatarajiwa kufurika watu siku ya tarehe 30/5/2015 kwa kuwa kipenzi cha watanzania na Rais Mtarajiwa atasimama mbele ya umati huo kukubali kutumwa kwa kuwatumikia watu hao kwenye kiti cha urais.
Moja ya changamoto kubwa ambayo atakutana nayo Rais ajaye ni pamoja na
1. bomu la ajira kwa vijana.
2. Suala la matumizi mabaya ya fedha za umma
3.Ukwepaji kodi na matumizi mabovu ya rasilimali za Nchi yetu.
4.Suala la kupuuzwa kwa elimu na watendaji wake.
5. Kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.

Hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo kiongozi wa Nchi hii anayekuja atakutana nayo na bila shaka tutataka ayatatue kwa kiwango chake.

Uwezo wa Mh.lowasa kiutendaji si wa kubeza na ukiangalia nyadhifa alizowahi kushika serekalini na uwezo wake kisiasa utagundua kwamba hamna mtu ambaye anaweza kusimama nae katika kinyang'anyiro cha Urais na kumzidi.
Tukubali kwamba hili ni fungu jema chaguo la watu chaguo la Mungu.
Jitokeze uje umsikilize.

Mtaenda kumsikiliza nyie wafaidika na wapenda UFISADI nchini na watu wachache ambao hawawezi kunyambulisha mambo. FISADI la MAFISADI apewe nchi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!, ng'o!!!!!!!!!!!!!!!!. embu rejea hii mada labda mmesahau kwasababu ya kufikiri kwa matumbo.
[WAZIRI Mkuu “aliyeng’olewa na Bunge,” Edward Lowassa, ameanza kujitetea akisema hakupokea rushwa yoyote kutoka kampuni ya Richmond Development Company. Lowassa anasema kilichotokea ni kwamba aliponzwa na watendaji walio chini yake; na kwamba binafsi hakuhusika na mchakato mzima ulioipa ushindi wa zabuni Richmond.

Anasema, “Sikuhusika katika mchakato wa zabuni ulioipa ushindi Richmond. Mimi niliponzwa na wasaidizi wangu. Hawa ndiyo walioniangusha. Nimewajibika kwa niaba yao,” Lowassa amewaambia wafuasi wake na wananchi kwa ujumla. Lowassa anasema kazi ya kufanya uchambuzi wa kuchagua mzabuni, haikufanywa na yeye, bali ilifanywa na Kamati Maalum ya Serikali (GNT).

Hakuna ubishi kwamba utetezi huu mpya wa Lowassa unahitaji kuhojiwa. Je, Lowassa kwa nini hakueleza haya ndani ya Bunge; Na alipewa nafasi bungeni, alishindwa kulieleza Bunge kile ambacho kwenye mkutano wa hadhara, kijijini kwake, katika jimbo la Monduli? Inawezekana kabisa, Lowassa hakusema bungeni yale aliyosema Monduli kwa kuwa alijua wabunge wangeyapinga kwa kuwa wanajua ukweli mzima wa suala hili.

Ndiyo maana wala hakujihangaisha kujibu hoja za Kamati teule iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe, iliyoonyesha mazingira ya kuhusika kwake. Vilevile, Lowassa alijua kuwa Bunge lingekataa utetezi wake. Matokeo yake, angebanwa na kanuni zinazotaka mbunge kutosema uwongo bungeni.

Inawezekana pia kwamba Lowassa alishindwa kusema hayo bungeni, kwa hofu kwamba Nazir Karamgi na Dk. Msabaha walikuwamo ndani ya Bunge, na hivyo wangeweza kusema ukweli wa yote yaliyotokea. Lakini ukiacha hilo, hata utetezi wenyewe wa Lowassa bado una mashaka.

Kwanza, Lowassa anakubali kuwa Kamati ya Maalum ya serikali iliyoshughulikia zabuni ya Richmond iliundwa kwa maelekezo na maagizo yake. Lowassa ambaye leo anakana kuhusika na Richmond, ndiye anasadikiwa kutoa amri na hata kutisha wasaidizi wake, akitaka Kamati “Ibebe Richmond” na kuipa kazi iliyoomba.

Vilevile, ni Lowassa ambaye anatajwa kushinikiza upokonywaji Bodi ya Tenda ya Tanesco kazi ya kutafuta mzabuni, baada ya Bodi hiyo kukataa kuipa kazi ya kufua umeme wa dharula kampuni ya Richmond.

Ni Lowassa yuleyule anayetajwa kushinikiza kupunguzwa kwa vigezo ili kufanikisha azima ya kuipa kazi kampuni hiyo ya kitapeli. Lowassa na wenzake walijua, pasipo na shaka kuwa Richmond ni kampuni isiyokuwa na hadhi, sifa, wala uwezo wa kufanya kazi iliyotaka kupewa.

Hili linathibitishwa na barua ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Ibrahim Msabaha kwenda kwa Lowassa, ambayo watetezi na wafuasi wa Lowassa wanaitumia kutaka kumsafisha. Barua hiyo yenye Kumb. Na. CDB 286/397/01 ya 17 Juni, 2006 inasema, “…Nakubaliana na mapendekezo ya Kamati ya Majadiliano ya Serikali (GNT) ya kuteua Richmond na naomba kuwasilisha kwako, kwa uamuzi na maelekezo.”

Hii inathibitisha madai ya siku nyingi kwamba aliyeiteua Richmond kuingia mkataba na Tanesco, hakuwa Dk. Msabaha, alikuwa Lowassa. Ni wazi kwamba Lowassa alitumia ustadi mkubwa kuiteua Richmond, kwani alitumia kichaka cha Kamati yake ya Majadiliano.

Barua ya Dk. Msabaha inaonyesha na kuthibitisha ukweli kwamba Lowassa alikuwa mstari wa mbele katika kusimamia, kupitisha, kuagiza na hata kuamuru Kamati kuipa zabuni Richmond. Si barua ya Dk. Msabaha pekee, ambayo inathibitisha ukweli huo, bali hata barua iliyotoka ndani ya ofisi ya Lowassa mwenyewe inaliweka wazi jambo hili.

Msaidizi Mkuu wa Lowassa, Ole Kuyan, katika barua yake kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anasema, “…Endelea kusaini mkataba kati ya Richmond na serikali, maana Waziri Mkuu, Edward Lowassa tayari ameridhika kwamba Richmond ipewe mkataba.

Kauli kwamba Waziri Mkuu Lowassa “ameridhika” inafunga mjadala na inadhirisha kwamba Lowassa alijua kila hatua katika kufanikisha mkataba huu. Aidha, kauli ya Kuyan, kwamba Waziri Mkuu ameridhika na hivyo mkataba kati ya serikali na Richmond usainiwe, inaonyesha wazi kuwa Lowassa ndiye aliyekuwa anasimamia jambo hili.

Kwa upande mwingine, hoja ya Lowassa kwamba aliwahi kumuonya Dk. Msabaha kuhusu “Ubabaishaji wa Richmond,” na “kutaka kuvunja mkataba huo mara mbili, lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na kuzuiwa na wanasheria,” haina uzito wala mantiki.

Sababu ni mbili: Kwanza, hakuna hata mwanasheria mmoja nchini na nje ya nchi, ambaye angeshauri serikali kubaki katika mkataba wa Richmond, kama Lowassa angesema ukweli kwamba Richmond haipo kwa mujibu wa sheria.

Hii ina maana haipo katika orodha ya kampuni za Marekani, wala katika orodha ya Wakala wa Msajili wa Kampuni (BRELA) nchini Tanzania. Lilikuwa ni jukumu la Lowassa kuwaeleza kinaga ubaga wanasheria kwamba, si hapa Tanzania wala Marekani, ambako Richmond imesajiliwa.

Halikuwa jukumu la wanasheria kujua kama Richmond ni kampuni hewa. Hilo lilikuwa jukumu la Lowassa na serikali yake. Kwani wanasheria ni kama madaktari; jukumu la kueleza maradhi linabaki kwa mgonjwa mwenyewe. Na mficha maradhi, umauti humfichua. Lowassa hakuchukua jukumu hilo.

Hakusema ukweli kwa wanasheria kuwa Richmond haipo kisheria. Kwamba Richmond ni kampuni ya mfukoni. Kwamba haina uwezo wala heshima ya kufanya kazi na serikali. Kwa hakika, kama yote haya yangejulikana wazi kwa wanasheria, lazima wangeshauri serikali kuvunja mkataba, tena mara moja.

Kwa kuwa Richmond haikuwa imesajiliwa, wanasheria wanajua kuwa hakuna mtu ambaye angekwenda mahakamani na kudai yeye ni mmiliki wa Richmond. Je, angeanzia wapi? Angetumia nyaraka gani kuthibitisha madai yake? Angesema nini mbele ya sheria? Wapi hasa angeshika?

Kutokana na hali hiyo, Lowassa asitake kukwepa jukumu lake la kikatiba la kutumia vyombo vya serikali kufanya uchunguzi na kujua uhalali wa kuwapo kwa Richmond. Serikalai ilipaswa kujua nani mmiliki wa Richmond. Yuko wapi? Uwezo wake kifedha ni upi?

Je, si tapeli lililokubuhu ambalo lilitaka kuingiza taifa mkengeni kama ilivyotokea? Lilikuwa ni moja ya majukumu ya ofisi ya Lowassa kwenda BRELA, na kupekua mafaili ili kubaini ukweli wa madai ya wananchi na vyombo vya habari vilivyokuwa vinapaza sauti vikisema, Richmond haikuwa kampuni, bali kilikuwa kikundi cha watu waliojikusanya ili kuchota hazina ya taifa.

Lakini pamoja na kwamba Lowassa alijua ukweli huo, aliamua kukaa kimya. Hili alilifanya ili kupata mahali pakutokea, pale ukweli utakapodhihiri. Maana hata pale ilipodhihirika kuwa Richmond haikuwa na uwezo wa kifedha, na kwamba mabenki ya Marekani yamekataa kutoa barua ya dhamana (LC), bado serikali iliamrisha au ilishauri au ilishawishi benki ya CRDB kubeba jukumu hilo.

Je, mbona Lowassa hataki kulisema hili, badala yake anaendelea kung’ang’ania wanasheria akidai wamemshauri vibaya? Ni Lowassa ambaye alijiapiza na kusema, “Richmond ni watu makini,” na kwamba umeme utaingia katika Gridi ya Taifa ndani ya mwezi mmoja. Ni uwongo huo uliomuambukiza Rais Jakaya Kikwete, hadi kufikia kuchukua hatua ya kuwadanganya wananchi na jumuiya ya kimataifa juu ya ujio wa umeme wa Richmond.

Wanaokumbuka vema wanajua kuwa alikuwa ni Lowassa ambaye alihubiri wananchi kutojadili Richmond kwa madai kwamba, “mabwawa ya kuzalisha umeme tayari yamejaa maji,” na hivyo hakuna tena tatizo la umeme nchini.

Ukiondoa hilo, kuna hili analolieneza kuwa yeye ni bingwa wa kuvunja mikataba nchini. Mfano anaotoa ni mkataba kati ya serikali na kampuni ya City Water. Sasa swali tunajiuliza: Kama kauli ya Lowassa ina ukweli, kwa nini alishindwa kuvunja mkataba huu wa Richmond?

Mbona huu ndiyo ulikuwa wazi zaidi, ambapo hata ‘juha’ alifahamu kuwa Richmond ilikuwa kampuni ya kitapeli? Kudai kuwa serikali na Lowassa hawakujua kuwa Richmond lilikuwa genge la walaghai, na hivyo kuwaachia matapeli wa kila rangi kufanya watakavyo, ni kuidharaulisha serikali kwa viwango vya juu mno.

Katika taarifa yake kwa Shirika la Habari la Associated Press (AP) la Marekani, anayetajwa kuwa mmiliki wa Richmond Mahammed Gire anasema, “Si sisi, wala yeyote kati ya watumishi wetu, hakuna aliyepokea sarafu nyekundu au kulipwa chochote, kutoka serikali ya Tanzania au kwa ofisa yeyote wa kampuni yetu.”

Anasema, “Badala yake tumekuwa tukishuhudia kauli za uongo na madai potofu juu yetu,” inasema taarifa ya kampuni hiyo. Je, Waziri Mkuu Lowassa hana wasaidizi? Kwa nini alishindwa kuwasiliana na Mohammed Gire, aliyetajwa kuwa mmiliki wa Richmond na kujua ukweli wa jambo hili? Je, kama yote haya aliyajua, lakini alishindwa kuyasimamia kwa dhati, kwa nini watu wanajihangaisha kutaka kumsafisha? Mkurugenzi wa Mawasiliano wa ikulu, Salva Rwenyemamu amethibitisha kuwa anamfahamu aliyekuwa anadaiwa kuwa “mwenye” Richmond, mtu mmoja aitwaye Gire.

Salva anakiri kuwa alitambulishwa kwa mtu huyo na Rostam Aziz ambaye alikiri pia kuwa ni rafiki yake. Vipi Lowassa alishindwa kuwasiliana na rafiki yake sana, Rostam Aziz kuhusu suala hili? Kutokana na maelezo hayo ya Salva ambayo hayawezi kutiliwa mashaka, ni wazi kuwa Rostam anaijua vema kampuni ya Richmond.

Na kwa kuwa Lowassa na Rostam ni chanda na pete, hakuna mwenye ubavu wa kumficha mwenzake jambo. Hivyo haiingii akilini kwamba Rostam angeweza kumdanganya Lowassa juu ya Richmond, hadi Lowassa aharibikiwe kwa kiwango hiki.

Kwa kiongozi kama Lowassa kukubali kuidhinisha mamilioni yote hayo ya shilingi kwa kampuni hewa, ni lazima kuna jambo limejificha.


]
 
Sipendi kuheshimu maoni ya yoyote yule amuitae mwingine MUIZI.kwa nini asichukuliwe hatua za kisheria...Fact ni kwamba udhaifu wa bunge letu kutokufanya wanalotakiwa kufanya ndiko kunakosababisha mapungufu serikalini.Wabunge bila ya kujali itikadi zao wangesimamia serikali ipasavyo tungekuwa mbali saana.
 
Habari kutoka kwa team Lowassa zinasema kuwa tukio
la Lowassa kutangaza nia linalotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi 30/May/2015 huenda likarushwa Live, yaani moja kwa moja kupitia redio na Television kadhaa binafsi.
Mpaka sasa waandaji wa tukio hilo kutoka Team Lowassa wamekataa kuweka wazi ni vituo gani vya redio na Luninga ambavyo viko kwenye mazungumzo nao ili kurusha tukio hilo kwa hofu ya kufanyiwa fitna na kutiwa hofu kutoka kambi hasimu.

Ikumbukwe pia TBC na Star TV tayari wameshaweka wazi(kupitia kwa waandishi wao) kuwa kamwe hawatarusha habari na matukio yoyote chanya ya kisiasa ya Lowassa katika harakati zake za kutaka kupitishwa na CCM ili kugombea urais na wakati huo huo watarusha matukio ya harakati za kisiasa za Membe na Pinda. Hilo ni kutokana na sera za wamiliki wa vituo hivyo kwa kipindi hiki.

Tayari TBC walishaanza mkakati huo, baada ya kufanya mahojiano na Benard Membe siku ya jumapili iliyopita usiku na kumpa airtime kuzungumzia nia yake ya kutaka kugombea urais kupitia CCM na kutamka mikakati yake hiyo, na wakati huo huo wakagoma kabisa kurusha habari za Lowassa wakati akiongea na wahariri siku moja baadaye.
 
Hakuna shida maana TBC itafanyiwa overhall baada ya Lowassa kuingia madarakani... Diallo anajulikana kuwa ndo mtakatishaji wa fedha za Membe ... Kamwe hataweza kurusha matukio muhimu ya Lowassa ... ITV ambayo Watanzania wote wanaijua kama ndo TV ya Taifa hatuna shaka kuwa watarusha kama sehemu ya kuongeza Demokrasia nchini.... Channel 10 nao watarusha kama kawaida plus Clouds TV ...
Habari kutoka kwa team Lowassa zinasema kuwa tukio
la Lowassa kutangaza nia linalotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi 30/May/2015 huenda likarushwa Live, yaani moja kwa moja kupitia redio na Television kadhaa binafsi.
Mpaka sasa waandaji wa tukio hilo kutoka Team Lowassa wamekataa kuweka wazi ni vituo gani vya redio na Luninga ambavyo viko kwenye mazungumzo nao ili kurusha tukio hilo kwa hofu ya kufanyiwa fitna na kutiwa hofu kutoka kambi hasimu.

Ikumbukwe pia TBC na Star TV tayari wameshaweka wazi(kupitia kwa waandishi wao) kuwa kamwe hawatarusha habari na matukio yoyote chanya ya kisiasa ya Lowassa katika harakati zake za kutaka kupitishwa na CCM ili kugombea urais na wakati huo huo watarusha matukio ya harakati za kisiasa za Membe na Pinda. Hilo ni kutokana na sera za wamiliki wa vituo hivyo kwa kipindi hiki.

Tayari TBC walishaanza mkakati huo, baada ya kufanya mahojiano na Benard Membe siku ya jumapili iliyopita usiku na kumpa airtime kuzungumzia nia yake ya kutaka kugombea urais kupitia CCM na kutamka mikakati yake hiyo, na wakati huo huo wakagoma kabisa kurusha habari za Lowassa wakati akiongea na wahariri siku moja baadaye.
 
Hakuna shida maana TBC itafanyiwa overhall baada ya Lowassa kuingia madarakani... Diallo anajulikana kuwa ndo mtakatishaji wa fedha za Membe ... Kamwe hataweza kurusha matukio muhimu ya Lowassa ... ITV ambayo Watanzania wote wanaijua kama ndo TV ya Taifa hatuna shaka kuwa watarusha kama sehemu ya kuongeza Demokrasia nchini.... Channel 10 nao watarusha kama kawaida plus Clouds TV ...
Tulipowaambia kwamba TBC ina matatizo,inarusha habari za upande mmoja tu wa CCM na kuzikanyaga habari kutoka upande wa upinzani hususani CHADEMA. Nyinyi mukawa mnachekelea na kufurahia tabia hii ya TBC. Sasa dhambi ya ubaguzi inawatafuna wenyewe sasa. Na Sasa ndio mnakubali kwamba ITV imechukuwa pahala pa television ya taifa wakati mwanzo mulikuwa munaibeza na kuidhihaki na kuinyanyapaa! NYINYI KWELI MAPAKACHA!
 
Hakuna kitu kinacho ligharimu taifa kama kutofikiria kwa umbali mkubwa, uyu aliye radhi kwa chochote ilimradi akaishi Magogoni. Akiupata ni lzima apambane ku pay back watakao mfadhi.
 
Tutaheshimiana tu!
1. Vituo nane kuwa hewani saa 8 mchana hadi 11 jioni
2. Hakutakuwa na umeme kuanzia SAA 2 asubuhi hadi 12 jioni!

Tutaheshimiana tu.
 

Attachments

  • 1432880815065.jpg
    1432880815065.jpg
    66.7 KB · Views: 792
  • 1432880869640.jpg
    1432880869640.jpg
    59.9 KB · Views: 813
Manaake hadi Ilala imeitwa Mkoa ilhali ni Wilaya. Tutaheshimiana tu!
 
Haaaa haaa nasikia wanafunzi wa chuo cha ualimu Patandi wamekataza kuhudhuria sherehe hizo na jumamosi wamepangiwa kufanya mtihani kuanzia saa 8 mchana hadi 12 jioni tutaheshimiana tu.
 
Mkoani Kagera ukiwa na wilaya 8 TANESCO wameata umeme tangu juzi jumatano na kwamba utarejeshwa jumatatu au jumapili.Tutaheshimiana tu
 
Jambo hilo litakuwa ni kumsafisha Lowassa, na huko ni kuogopa atakayoysema kuhusu RichardMondi. Kwani hizo TV na radio stations hazitawe kurusha marudio yako?
 
Manaake hadi Ilala imeitwa Mkoa ilhali ni Wilaya. Tutaheshimiana tu!

Ndugu....kanuni zanazoratibu shirika la umeme...limeweka zoning office na Ilala ni Mkoa....kwa ujumla kwa mujibu wa Tanesko Dar kuna mikoa ya kiutendaji zaidi ya Saba.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom