Arusha Stadium kufurika 30/5/2015, Ni mkutano wa hadhara wa Lowassa

Status
Not open for further replies.
CCM inaelekea kubaya zaidi na zaidi kila kukicha. Hapa Dodoma,Waziri Sophia Simba anahaha kukusanya na kusafirisha makada na wananchi wa kawaida kwenda Arusha. Wasafirishwa wanapewa sh.30000 na watakapofika Arusha malipo mengine yatafanyika.

Kesho,Ndugu Edward Lowassa anatangaza nia ya Urais huko Arusha. Sophia Simba anawasafirisha watu mchana wa leo kwenda Arusha,kutoka hapa Dodoma kwenda kwa Lowassa. Pesa inamwagwa vilivyo.

Hivi ndivyo uungwaji mkono unavyopaswa kuwa? Lowassa anaendelea kujidhihirisha jinsi asivyofaa kwa kutaka kuununua Urais. Fisadi aogopwe kama acid!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kanda ya Kati)

Lowasa na wapambe wake ni janga la taifa.Hawa watu wananunua ikuru kwa pesa zao walizopata kwa wizi.Lowasa vijana tumkatae tumzomee kwa kumuita fisadi fisadi na kumtupia makopo.Nyerere alikomboaa nchi angali kijana sisi ni wakati wetu kukomboa nchi kutoka mikononi mwa gamba gumu na fisadi la kimataifa
 
Me nawashangaa nyinyi wanaccm hivi kweli kwa style hii Lowasa anafaa kupitushwa hata kamati kuu mnajipambanua mnafata falsafa ya Mwl. Nyerere yupi ambaye anaamini ikulu ni mahali patakatifu cjui hebu mnaopata access mwambieni mwnkiti wa chama asimamie haki Mwl. Hakutaka haya yote takukuru wako wapi?
 
Naona mnawweseka saana kuona lowasa anachukua hisia za watu wenye akili timamu kama sisi nakuwaacha wanafiki na wachumia tumbo kama nyinyi
 
Ngoja wabebane wataliona fagio la chuma wakati ukifika hakutq fisadi atayepona kwenye fagio la chuma.
 
Naona mnawweseka saana kuona lowasa anachukua hisia za watu wenye akili timamu kama sisi nakuwaacha wanafiki na wachumia tumbo kama nyinyi
Lowasa anachukua husani zenu wenye upeo mdogo mnaoweka mbele ufisadi na rushwa katika kutafuta uongozi.
 
Safi sana Sophia Simba, mwaka huu mpaka CCM lipasuke vpande vipande, endelea kukaza uzi.

Waziri mwingine naye aje agawe pesa na kusafirisha watu kwenda kwa Membe

Mwingine kwa Magufuri, hadi CCM libaki vipande vipande. Mungu mwaka huu lazima ajidhihirishe kwa Watanzania baada ya kutuacha utumwani mwa CCM kwa mda mrefu.
 
* Maelfu na Mamia washawasili mpaka sasa

* Zaidi ya makundi 200 pia kuingia leo, Hoteli shida... Mji wa Moshi nao wafurika..

Huu uwingi wa watu katika jiji la Arusha kwa hakika siwezi kuufananisha na tukio lolote lile mpaka sasa... Mamillioni na mamia ya wananchi kutoka kila pembe na kila kona ya Nchi washawasili tayari kabisa kwa tukio la karne, kesho tarehe 30.05.2015 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid....

Kwa hali iliyopo ni wazi jiji la Arusha limezidiwa kwa uwingi wa watu, ni shangwe, shamrashamra na furaha ndiyo zimetawala katika viungo vyote vya jiji wananchi wakiwa tayari kabisa kwa kesho kusikia neno la ukombozi na kupata matumaini mapya ya maisha yao....

"Kaka kwa sasa umechelewa huwezi kupata vyumba kabisa umechelewa kama unaweza rudi ukalale Moshi napo sina uhakika kama utapata manake wote walikosa huku wameenda Moshi" Mmoja wa Meneja wa hoteli aliniambia jana saa sita usiku nilipoingia katika hili jiji ili nami niweze kuwa sehemu ya historia...

Kila kona ya jiji, rangi za kijani na njano zimetamalaki, kila kona nyimbo za chama hasa zile alizowahi kuimba Capt. Komba zimekuwa sikisikika kwa wingi, kila kona ni nyimbo za ukombozi kama zile zilizoimbwa nyakati za majemedari wetu wa Africa (Mandela, Nyerere, Lumumba, Kenyata, Sekou Toure ) na macomrade wengine hii ni kuthibitisha kwamba saa ya ukombozi wa mara ya pili umewadia...

Hakuna nyakati ambayo Tanzania inatakiwa kujivunia kama nyakati hizi ambazo mkombozi wa kuleta elimu bora kapatikana, kilimo bora, afya bora, mtatuzi wa suala la ajira, mjenzi wa viwanda na mkuzi wa uchumi kwa double digits kapatikana, na siyo mwingine bali ni yule ambaye tulikuwa tukimsubiri kwa muda mrefu sana na hatimaye kesho atanguruma katika uwanja wa Sheikh Abeid....

Vijana katika makundi yao tokea jana usiku nao pia wamekuwa mstari wa mbele hasa wakitiana hamasa na shamrashamra kwa kuimba nyimbo za kikombozi (Vijana msilale lale lale, vijana msilale lale lale bado mapambano x 2)... Hii ndiyo Arusha ambayo mpaka sasa walai hakuna pa kukanyaga kila kona kumejaa huku vifijo na nderemo zikiendelea....

"Wakati ni sasa, simama na uhesabiwe"....
 
CCM inaelekea kubaya zaidi na zaidi kila kukicha. Hapa Dodoma,Waziri Sophia Simba anahaha kukusanya na kusafirisha makada na wananchi wa kawaida kwenda Arusha. Wasafirishwa wanapewa sh.30000 na watakapofika Arusha malipo mengine yatafanyika.

Kesho,Ndugu Edward Lowassa anatangaza nia ya Urais huko Arusha. Sophia Simba anawasafirisha watu mchana wa leo kwenda Arusha,kutoka hapa Dodoma kwenda kwa Lowassa. Pesa inamwagwa vilivyo.

Hivi ndivyo uungwaji mkono unavyopaswa kuwa? Lowassa anaendelea kujidhihirisha jinsi asivyofaa kwa kutaka kuununua Urais. Fisadi aogopwe kama acid!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kanda ya Kati)

Acha CCM muumizane kaka . Poleni sana . Kumbe ata wewe wamjua kwamba ni fisadi ?Je akipitishwa utagoma kumfanyia kampeni ? Tupe neno mzee wa Kuvutana
 
Mojawapo ya kamba walizofungwa jirani zetu wa Kenya katika kampeni za uchaguzi mkuu uliompa Uhuru kiti cha urais ni pamoja na wapiga kura kuaminishwa ati wamchague Rais mwenye mihela yake ili nchi iondokane na tatizo la ufisadi uliokithiri.

Kinyume na matarajio yao, tatizo la ufisadi limebaki mtambuka. Kwa hiyo pamoja na mihela ile ya Mkulu, ufisadi umeendelea kubisha hodi hadi mlangoni kwake. Uozo unaanzia huko. Kibaya zaidi ni pale status-quo ya "corruption with impunity" inavyodumishwa. Watuhumiwa wanabadilishiwa lebo za ofisi. Leo huku kesho kule. Hakuna hatua stahiki zinazochukuliwa dhidi ya WEZI wa mali ya umma. Aidha MAFISADI hao hawaguswi au hawagusiki.

Picha hii inajirudia katika nchi nyingi. Matokeo ya udhaifu huu ni dhahiri na imefikia pale watawala wanapofananishwa na Wakoloni. Kwa Afrika yetu tunao wakoloni weusi kwa vile wale wengine walikuwa Wazungu. Wale tunaowanyooshea vidole kama chanzo cha matatizo yanayolikumba bara la Africa hata leo hii, miaka 50 baadae.

Hapa kwetu, watuhumiwa mbalimbali wa kansa hii ya ufisadi wamejipanga kuwania utawala wa nchi yetu. Kama kwa jirani zetu, wanataka watuaminishe wao ni MATAJIRI, wanayo mihela yao na kwa hiyo aidha wamevimbiwa nazo au pia watatusaidia nasi tusionazo tuwe matajiri. Ati umasikini ni kitu kibaya sana. Ya kwamba ukimpa maskini uongozi atageuka kuwa fisadi na kwa hiyo hafai!
Hatuhitaji kuangalia mbali. Pale kwa jirani, uozo umeanzia kichwani. Matokeo yake mnayaona. Tusidanganyike!
 
Ni lowasaa kila mahali mkuu... safari ya matumaini inaanzia Arusha
 
la kushangaza pamoja na mbwembwe hizi NEC ya ccm itakata jina la senior fisadi!!
 
Uuuuuwwwwiiii wakuu yupo anaetangaza nia kwenye ukumbi wa chuo cha mipango dodoma huyu ni balaa ametoa ofa kwa wanavyuo wote vinywaji chakula usafir wa kwenda na kurud buuurreeee full bata ni shidaaaa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom