Arusha: Madiwani waliotimuliwa na CHADEMA wabwagwa mahakamani!

Sikuwa na shaka na hukumu hiyo, kwani ushindi ulikuwa WAZI. Tunasubiri hatima ya MEYA Jiji la Arusha. Hii ni aibu kwa Waziri Mkuu Pinda, Mkuchika, Nape pamoja na Chatanda.
 
...je, yawezekana Arusha ikawa (ignite) chanzo cha moto wa mabadiliko ya taifa hili la Mashariki mwa Afrika??????

Sehemu yoyote inaweza kuwa chanzo cha mabadiliko Arusha walisha choka siku nyingi alichokifanya Lema ni kuwapa ujasiri vijana na hilo amefanikiwa sana huwezi amini hata baada ya polisi kuua wakazi wa Arusha na kujeruhi lakini hata Leo hii watu wa Arusha ukiwaambia tuandamane sijui kama utamaliza saa hawajaaa na wakati mwingi huwa wana lazimisha kuandamana mfano ni siku mkutano wa CC ya Chadema walitaka kuandamana wakazuiwa...kifupi watu wa arusha wamechoka na CCM na subiri kwenye kampeni za kata nne zilizo wazi patachimbika ningependa sana nimuone Nepi Arusha
 
Freeman-Mbowe-CHADEMA.jpg

MAHAKAMA ya hakimu mkazi Arusha imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na madiwani watano waliofukuzwa kwenye Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambapo imedaiwa kuwa madiwani hao wanatakiwa kulipa garama mbalimbali ambazo zimetumika katika kesi hiyo.
Hapo awali Madiwani hao waliwasilisha pingamizi ambapo pingamizi hilo lilidai kuwa madiwani hao hawakutendewa haki na chama hicho ambapo chama hicho kiliwafukuza .

hayo yamedhibitika leo, katika mahakama ya hakimu mkazi ya jiji la arusha ambapo kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Hawa Mguruta ambapo alisema kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kupitia hoja nne za pingamizi zilizowasilishwa mahakamani hapo na mawakili wadaiwa , Method Kimomogoro na Albert Msando na majibu ya wakili wa wadai ,, Severine Lawena .

Katika shauri hilo la madai namba 17 la mwaka 2011 washitakiwa walikuwa ni Chama Cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA) na Freeman Mbowe huku wadai wakiwa ni madiwani waliofukuzwa kwenye chama hicho na kata zao kwenye mabano ni Naibu Meya , Estomii Mallah ( Kimandolu) , John Bayo (Elerai), Ruben Ngowi ( Themi), Rehema Mohamed (Viti Maalum) na Charles Mpanda (Kaloleni).

Aidha Hakimu Mguruta alisema kuwa anakubaliana na hoja za mawakili wa wadai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kuchunguza maamuzi ya chombo binafsi kama ilivyo kamati kuu ya Chadema ambapo walibainisha kuwa chombo chenye mamlaka hayo ni mahakama kuu .

"ni kwamba nakubaliana na hoja kuwa Chadema haiwezi kushitakiwa kwa jina lake kwani jina hilo halina uhai kisheria hivyo haiwezi kushitaki wala kushitakiwa kwa mujibu wa sheria'alieleza Hakimu Mguruta.

Hakimu Mguruta alisema kuwa anakubaliana na hoja ya mawakili hao kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho (Mbowe) hawezi kushitakiwa binafsi alipaswa kushitakiwa kwa nafasi yake ua Uenyekiti wa Taifa vinginevyo hataweza kutekeleza maelekezo ya mahakama hiyo ndani ya Chadema

"Mbowe alipaswa kushtakiwa kwa nafasi yake ya uenyekiti wa Taifa kwani endapo ataondolewa kwenye nafasi hiyo au kujiuzulu hataweza kutekeleza maamuzi ya mahakama kwani hataweza kuendesha na kusimamia maamuzi ya vikao ndani ya chadema" alisema hakimu mguruta .

Katika hatua nyingine Hakimu huyo alikubaliana na hoja kuwa kesi hiyo imefika mahakamani hapo ikiwa imepitwa na wakati kwani tayari madiwani hao walishakata rufaa kwenye baraza kuu la Chadema hivyo kesi hiyo imepoteza maana huku akiongeza kuwa mahakama kuu ndiyo yenye uwezo wa kupitia maamuzi yaliyofanywa na na vikao ndani ya taasisi lakini haiwezi kuhoji au kuamua juu ya taratibu za ndani za chama husika .

Wakati maamuzi hayo yakitolewa madiwani watatu kati ya watano waliofungua kesi hiyo walikuwa mahakamani hapo ambao ni Diwani wa kata ya Elerai Bw John Bayo , Naibu Meya wa jiji la Arusha ambaye pia ni diwani wa a kata ya Kimandolu, Bw Estomih Mallah ambapo walipotakiwa kutoa maoni yao mara baada ya kikao cha mahakama kumalizika walisema kuwa hawana maoni ya kuongea na vyombo vya habari. .

Aidha iliwabidi madiwani hao waliofungua kesi hiyo kusubiri ndani ya chumba cha mahakama mpaka mashabiki hao wa Chadema walipotoka nje ndipo nao wakatoka ingawa waliendelea kukaa kwenye maeneo hayo ya mahakama mpaka wanachama hao walipoondoka kwa maandamano na mbunge wa Arusha Mjini , Godbless lema .

Hata hivyo katika hatua nyingine polisi wenye silaha na mabomu ya machozi wakiwa kwenye magari mawili ya Polisi yenye namba za usajili PT 1844 na PT 0746 walifika na kuwaamuru wanachama hao kutawanyika mbele ya jengo la ofisi za mkuu wa wilaya ya Arusha zilipo ofisi za mbunge huyo ambapo walitii na kuondoka .
 
hawa jamaaa hawakutakiwa kuwa na kiburi maana hata mahakama isingeweza kuwaweka kwa sababu hawana chama cha kuwakilisha
 
Juzi nimwona mmoja wao kwenye graduation ya sekondari moja hivi akisindikizana na wana CCM na mea wao nikajua hapa kwisha kazi
 
Pole sana Thomaso hizo ni dalili ya ukombozi.Hebu jiulize mngeshinda nyie mngesema nn?. Hautishiki eeeh ngoja tena kwenye chaguzi ndogo utaona cha moto.
Hamtutishi hata kidogo.kushinda kesi ni kitu cha kawaida sana tu na labda hata mmetoa rushwa ili mshinde.ngoja tuchunguze.
 
Mbona wapiga ngumi ukutani hivo mwenzetu huumiii; CHADEMA ni ngoma nyingine kabisa mzee wala usipoteze muda wako kukibishya juu ya mabadili haya ya kufa mtu nchini!!!!!!!!!!!!

Hamtutishi hata kidogo.kushinda kesi ni kitu cha kawaida sana tu na labda hata mmetoa rushwa ili mshinde.ngoja tuchunguze.
 
[h=2]Tuesday, September 20, 2011[/h][h=3]MAHAKAMA YAFUTA KESI YA MADIWANI WA CHADEMA ARUSHA[/h]

MAHAKAMA ya hakimu mkazi Arusha imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na madiwani watano waliofukuzwa kwenye Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambapo imedaiwa kuwa madiwani hao wanatakiwa kulipa garama mbalimbali ambazo zimetumika katika kesi hiyo.
Hapo awali Madiwani hao waliwasilisha pingamizi ambapo pingamizi hilo lilidai kuwa madiwani hao hawakutendewa haki na chama hicho ambapo chama hicho kiliwafukuza .

hayo yamedhibitika leo,(JANA) katika mahakama ya hakimu mkazi ya jiji la arusha ambapo kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Hawa Mguruta ambapo alisema kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kupitia hoja nne za pingamizi zilizowasilishwa mahakamani hapo na mawakili wadaiwa , Method Kimomogoro na Albert Msando na majibu ya wakili wa wadai ,, Severine Lawena .

Katika shauri hilo la madai namba 17 la mwaka 2011 washitakiwa walikuwa ni Chama Cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA) na Freeman Mbowe huku wadai wakiwa ni madiwani waliofukuzwa kwenye chama hicho na kata zao kwenye mabano ni Naibu Meya , Estomii Mallah ( Kimandolu) , John Bayo (Elerai), Ruben Ngowi ( Themi), Rehema Mohamed (Viti Maalum) na Charles Mpanda (Kaloleni).

Aidha Hakimu Mguruta alisema kuwa anakubaliana na hoja za mawakili wa wadai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kuchunguza maamuzi ya chombo binafsi kama ilivyo kamati kuu ya Chadema ambapo walibainisha kuwa chombo chenye mamlaka hayo ni mahakama kuu .

"ni kwamba nakubaliana na hoja kuwa Chadema haiwezi kushitakiwa kwa jina lake kwani jina hilo halina uhai kisheria hivyo haiwezi kushitaki wala kushitakiwa kwa mujibu wa sheria'alieleza Hakimu Mguruta.

Hakimu Mguruta alisema kuwa anakubaliana na hoja ya mawakili hao kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho (Mbowe) hawezi kushitakiwa binafsi alipaswa kushitakiwa kwa nafasi yake ua Uenyekiti wa Taifa vinginevyo hataweza kutekeleza maelekezo ya mahakama hiyo ndani ya Chadema

“Mbowe alipaswa kushtakiwa kwa nafasi yake ya uenyekiti wa Taifa kwani endapo ataondolewa kwenye nafasi hiyo au kujiuzulu hataweza kutekeleza maamuzi ya mahakama kwani hataweza kuendesha na kusimamia maamuzi ya vikao ndani ya chadema” alisema hakimu mguruta .

Katika hatua nyingine Hakimu huyo alikubaliana na hoja kuwa kesi hiyo imefika mahakamani hapo ikiwa imepitwa na wakati kwani tayari madiwani hao walishakata rufaa kwenye baraza kuu la Chadema hivyo kesi hiyo imepoteza maana huku akiongeza kuwa mahakama kuu ndiyo yenye uwezo wa kupitia maamuzi yaliyofanywa na na vikao ndani ya taasisi lakini haiwezi kuhoji au kuamua juu ya taratibu za ndani za chama husika .

Wakati maamuzi hayo yakitolewa madiwani watatu kati ya watano waliofungua kesi hiyo walikuwa mahakamani hapo ambao ni Diwani wa kata ya Elerai Bw John Bayo , Naibu Meya wa jiji la Arusha ambaye pia ni diwani wa a kata ya Kimandolu, Bw Estomih Mallah ambapo walipotakiwa kutoa maoni yao mara baada ya kikao cha mahakama kumalizika walisema kuwa hawana maoni ya kuongea na vyombo vya habari. .

Aidha iliwabidi madiwani hao waliofungua kesi hiyo kusubiri ndani ya chumba cha mahakama mpaka mashabiki hao wa Chadema walipotoka nje ndipo nao wakatoka ingawa waliendelea kukaa kwenye maeneo hayo ya mahakama mpaka wanachama hao walipoondoka kwa maandamano na mbunge wa Arusha Mjini , Godbless lema .

Hata hivyo katika hatua nyingine polisi wenye silaha na mabomu ya machozi wakiwa kwenye magari mawili ya Polisi yenye namba za usajili PT 1844 na PT 0746 walifika na kuwaamuru wanachama hao kutawanyika mbele ya jengo la ofisi za mkuu wa wilaya ya Arusha zilipo ofisi za mbunge huyo ambapo walitii na kuondoka .
 
Jamani kile kitufe cha THANKS umekiweka wapi wewe MOD wa zamu?????????????

Mkuu Crashwise, heshima mbeeeeeeeeeele kama tai!!!!!!! Sasa moto mkubwa Kamanda Lema akauhamishie kule Igunga; mbona yule Waziri ChaUsingizi aliyehamia Igunga majuzi atalia atachoka!!!!!!!!!!!

Huu Ushindi wa CHADEMA huko A-Town ni special dedication kwa MACHALII wote wa Arusha, BAVICHA na MACHALII wetu ngunguli wa kule Igunga kwa kazi nzuri mnaoendelea kufanya hadi hivi sasa.

Walazwahoi wote nchini, siku za kucheka meno yote 32 kuonekana nje ziko karibu sanaaaaa!!!!!!!!!!!

Sehemu yoyote inaweza kuwa chanzo cha mabadiliko Arusha walisha choka siku nyingi alichokifanya Lema ni kuwapa ujasiri vijana na hilo amefanikiwa sana huwezi amini hata baada ya polisi kuua wakazi wa Arusha na kujeruhi lakini hata Leo hii watu wa Arusha ukiwaambia tuandamane sijui kama utamaliza saa hawajaaa na wakati mwingi huwa wana lazimisha kuandamana mfano ni siku mkutano wa CC ya Chadema walitaka kuandamana wakazuiwa...kifupi watu wa arusha wamechoka na CCM na subiri kwenye kampeni za kata nne zilizo wazi patachimbika ningependa sana nimuone Nepi Arusha
 
Kwa sasa ni vizuri kwa hao waliokuwa madiwani wa Arusha kuelewa kuwa Ccm wamewadhalilisha, wamewatumia na kuwatupa bila
ya wao kuelewa nini kilichokuwa cha msingi walichokuwa wanawajibika kukifanya, ni uelewo mdogo wa kuelekeza nguvu na mawazo
yote katika pesa na kusahau kwa nini wananchi waliwachagua ili wawe voingozi kwa kusimamia kuchangia na kuleta maendeleo kwa
pamoja.
 
tunapenda kuona mihimili ya dola inafanya kazi zake bila kuingiliwa.Sometimes we can call it a gifted hand from the father of creation,changes in Tanzania must be ocurred,yes we can.kukamatwa kwa nyani miti yote teleza bana.mnyonge mnyongeni ila iko siku ukweli utajidhihirisha.big up sana mahakama
 
Kwisha habari yako Mizengo Peter kayanza Pinda kwa umbea wako.Ni mwanasheria kwa taaluma lakini sifuri kwa ushauri!!!!!!!!!! Mkuchika alitaka masifa hakuonyesha waredi juu ya sakata hilo!!!!!!!!! bravo Chadema!!!!!!!!!!! Down Pinda Mpimbwe!!!!!!!!!!!!
 
Hola DEMOKRATOS on duty!!!Mkuch haweze jiuzuru wewe anaona haibu badala ya kuwajibika.Angekuwa mwana CHADEMA hasingeambiwa kujiuzuru bali yeye mwenyewe anajua taratibu.Chakufanya sasa huyu jamaa abuluzwe mahakamani kwanza.
 
Back
Top Bottom