Arusha: Jeshi la Polisi lawafutia madaraja Madereva 776 kwa kukosa sifa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
60c54709-b3cc-4ed9-a5dd-02c364eec704.jpeg


Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama. limeendela kuimarisha ulinzi na usalama hali iliyopelekea kupunguza vitendo vya uhalifu katika Mkoa huu.

Sambamba na hilo katika kuhakikisha lina dhibiti ajali za barabarani, hivi karibuni Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea na ukaguzi wa leseni ambapa hadi hivi sasa jumla ya madereva (8142) wamehakikiwa kati yao madereva 776 wamefutiwa madaraja kwa kukosa sifa huku wakitakiwa Kwenda kusoma ili kupata sifa za kuendesha magari husika.

Kama ilivyo desturi tunapoelekea kufunga mwaka, kunakuwa na shamrashamra za wananchi kufurahia kumaliza mwaka wakiwa salama na kuingia mwaka mpya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linao wajibu kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani na utulivu sikukuu hiyo.

Katika kusherehekea sikukuu hiyo Jeshi la Polisi Mkoani hapa linawahakikishia wananchi wote wa Mkoa huu pamoja na wageni waliofika Mkoani kwetu ambapo ni lango Utalii nchini kuwa tumejipanga vyema kuhakikisha sikukuu hiyo inasherehekewa kwa amani na utulivu.

Jeshi la Polisi Mkoani hapa litahakikisha nyumba za ibada, kumbi za starehe na maeneo mengine yanakuwa na ulinzi wa kutosha ambapo askari watakuwa katika doria za miguu na magari kila kona ya jiji na wilaya zote za Mkoa huu Pamoja na doria kwa kutumia mifumo ya Tehama.

katika kusherehekea sikukuu hiyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linakataza na kutoa onyo mambo yafuatayo Kwa upande wa upigaji wa fataki, watakaoruhusiwa ni wale tu ambao watakua na vibali na hawataruhiwa kufyatua katika makazi ya watu, ni marufuku kuchoma matairi, kupanga mawe barabarani wakati wakusherehekea sikukuu hiyo.

Kama ilivyo nyakati zote Jeshi la Polisi Mkoani hapa tunawaomba wananchi waendelee kushirikiana nasi katika kuwabaini na kuwafichua wahalifu na uhalifu ili Mkoa wetu ambao ni lango la utalii hapa nchini uendelee kuwa shwari muda wote ikizingatiwa Mkoa wetu upokea wageni wengi wandani na nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom