Apigishwa mbizi kwenye dimbwi la maji ya barabarani kwa kukutwa katinga sare za jeshi

Wote hapo wana makosa aliye vaa sare na mwanajeshi aliye chukua sheria mkononi nyie mnatetea upande mmoja tu nadhani mnachaganya mnafikiri watu wanashabikia uvaaji wa sare ya jeshi tunataka kujua ni sheria gani inayo mpa mwanajeshi mamlaka hayo wote hao ni wakakosefu hata kama we ni mwanajeshi

Kumbe umejua kuwa wote wamekosea,ndo hivyo ukijifanya unajua kuvunja sheria ujue wapo wanaojua kuvunja zaidi yako.Kwa hiyo.hapo ni ngoma drooo.Aliyeuza cheni katoa cheni bandia na aliyenunua cheni katoa hela bandia.
 
Mimi narudia wanajeshi wote akili zao ndogo kwanini wanampa adhabu mtu asie staili kwanini wasiende kuzuia kiwandani wasitengeneze wanaonea watu.

akili yako ni sawa kabisa na huyo kijana aliyevaa hzo sare hali akijua kwamba anavunja shieria za nchi
 
Kahitimu kwanza MAFUNZO ya Jwtz kisha ndio utajua mamlaka haya anayatoa wapi.

Mafunzo na mamlaka ni vitu viwili tofauti. Unaweza ukapewa mafunzo usipewe mamlaka au si kila ukihitimu mafunzo mafunzo unapewa mamlaka. Ukimaliza JKT au mafunzo ya JW hayaambatani na kupewa mamlaka ya kuyatumia hadi amri itoke kwa immediate Kamanda.

Kwanza tukubali Jeshi hawana kazi za kuwatosha ndo maana huyu bwana alikuwa anajipitia zake akakutana na raia akamsimamisha na kuanza kumsulubu bila kujali muda anaopoteza.
 
Kumbe umejua kuwa wote wamekosea,ndo hivyo ukijifanya unajua kuvunja sheria ujue wapo wanaojua kuvunja zaidi yako.Kwa hiyo.hapo ni ngoma drooo.Aliyeuza cheni katoa cheni bandia na aliyenunua cheni katoa hela bandia.

We unatetea upuuzi wa uvunjaji wa sheria na kama ni mwanajeshi una tatizo somewhere si bure
 
Ha Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha haaaaaaah, sasa ndo unagundua kuwa ni kuvunja sheria

aisee...!! anachosema EMT hawezi kuvunja sheria kuvaa nguo za jeshi, na pia huyo alievaa nguo za jeshi kavunja sheria lakini mwanajeshi hana mamlaka ya kumzamisha kwenye dimbwi,kama kavunja sheria ahukumiwe kwa mujibu wa sheria na sio kwa mujibu wa mwanajeshi anavyotaka,angempeleka kunakohusika.

sasa nyinyi mnaomtetea mwanajeshi kwa upande mwingine pia mnamtetea mvunja sheria mwingine.
 
Last edited by a moderator:

Kwa hiyo alivunja sheria akitegemea atapelekwa kunakohusika!? Siku hizi ukivunja sheria hata wananchi wanakuadhibu, hujawahi kusikia au kuona kibaka kauliwa na wananchi au ni kwamba sheria hazipo!!? Ukivunja sheria na wewe usilalamike unapovunjiwa sheria
 
Ni kinyume na sheria ipi mkuu?
Si hiyo ya kutoa adhabu kwa kupiga mbizi kwenye maji machafu bila kujali afya ya huyo jamaa maana wengine wana afya mgogoro na hiyo sio special operation kwamba mwanajeshi atapata excuse in case jamaa akapoteza maisha. Hata hivyo siungi mkono hoja ya raia kung'ang'ania kuvaa nguo za kijeshi wakati ilishakatazwa hata kama ni za dukani maana wengi wanazitumia kwa ujambazi
 
aisee...!! anachosema EMT hawezi kuvunja sheria kuvaa nguo za jeshi, na pia huyo alievaa nguo za jeshi kavunja sheria lakini mwanajeshi hana mamlaka ya kumzamisha kwenye dimbwi,kama kavunja sheria ahukumiwe kwa mujibu wa sheria na sio kwa mujibu wa mwanajeshi anavyotaka,angempeleka kunakohusika.

sasa nyinyi mnaomtetea mwanajeshi kwa upande mwingine pia mnamtetea mvunja sheria mwingine.

kamanda yuko bize na ulinzi wa taifa,hana muda wa kupoteza kwenda mahakamani kutoa ushahidi kwa kesi ndogo kama hiyo.ambayo inamalizika kwa muda mfupi
 
Kwa hiyo alivunja sheria akitegemea atapelekwa kunakohusika!? Siku hizi ukivunja sheria hata wananchi wanakuadhibu, hujawahi kusikia au kuona kibaka kauliwa na wananchi au ni kwamba sheria hazipo!!? Ukivunja sheria na wewe usilalamike unapovunjiwa sheria

aisee...! ngoja niwaache na EMT
 
Last edited by a moderator:
Katika zoezi hilo ikaja kuwa kijana ana matatizo ya afya akapoteza maisha jee sheria itakuwa imelalia upande upi hapo? Suala hilo ni kosa kisheria na papo mahala pa kutoa adhabu inayostahili sio kila mtu ana mamlaka ya kuadhibu mtu.

Mmesahau kuwa Mheshimiwa Pinda alisema "Wapigwe tu maana hakuna namna nyingine, tumeshachoka sasa!"? Au ile inakubalika kwa polisi tu kutandika raia na si kwa wanajeshi?
 
Mbona wale makomandoo walowakamata juzi juzi hawakuwalowanisha mitarano au kwa kuwa wanajua moto wao ni wagezi na huzimiki kwa maji kama moto wa makaratasi.
Hivi kama kila mtu atajichukulia hatua kulingana na nafasi yake,hivi unafikiri hao wanajeshi wataweza kutembea mitaani pale watakapo kutana na wananchi wenye hasira na vinyongo vya muda mrefu ambavyo vikihamka hakuna gwanda wala kifaru kitakachoweza kuzuia ?
Wakti mwingine unaweza kujiuliza kama maamuzi ya haraka yanaweza kuchukuliwa na mtu kama huyo ambae anatakiwa ndie awe mwalimu wa matendo ya kibusara kwa watu wengi.
Ipo siku hadhi itashuka na heshima ya watanzania itaisha na ndipo watakapoona kuwa watanzania wanawaheshimu kwa kuwa ni sehemu yao lakini siyo kwamba inawaogopa.
Ktk dunia ya leo hakuna binadamu muoga anaemuogopa binadamu mwingine.
Elimu yenyewe ya mavazi hayo haitolewi halafu wao kazi yao ni kuwa walowanisha watu ktk mitaro ya maji au wamesahau kuwa hiyo ni sehemu ya kumjenga binadamu kuwa na moyo wa ujasiri ?
Ipo siku kibao kitawageukia na wao wakipanda hiace au daladala za uraiani walipe nauli la sivyo wajipange kuujua moto wa wananchi unaowafanya wao kupendeza na kodi zao.

wengi mnaojadili naona hamfahamu taaluma ya kijeshi, hawakufunzwa kurekebisha jamii, kazi yao ni kulinda mipaka na kuua adui tu inapobidi pia kusaidia jamii kipindi cha maafa na majanga si vinginevyo, kimsingi huyo kijana alikosea hakuona nguo zote za kuvaa mpaka avae nguo za dizaini hizo, pia tunauhakika gani kama hakuwa anataka kufanya uhalifu, sioni sababu ya kumtetea.
 
Mafunzo na mamlaka ni vitu viwili tofauti. Unaweza ukapewa mafunzo usipewe mamlaka au si kila ukihitimu mafunzo mafunzo unapewa mamlaka. Ukimaliza JKT au mafunzo ya JW hayaambatani na kupewa mamlaka ya kuyatumia hadi amri itoke kwa immediate Kamanda.

Kwanza tukubali Jeshi hawana kazi za kuwatosha ndo maana huyu bwana alikuwa anajipitia zake akakutana na raia akamsimamisha na kuanza kumsulubu bila kujali muda anaopoteza.

Hakuwa raia, alikuwa mwanajeshi feki. Wengine wanavaa nguo za namna hiyo wanaingia mtaani na kutishia watu kuwa ni wanajeshi na kwa kuwa wanafahamu wanajeshi wanaogopwa wanafanikiwa kupora na kuondoka. Wakiulizwa baadaye watasema waliovamia walivaa sare za 'jeshi. We unadhani aliyevamiwa na kiwewe atakachokuwa nacho ataweza kutofautisha kama hiyo nguo ni ya JWTZ, au ya jeshi la nchi nyingine?.
 
mkuu unafaa sana kuwa mtetezi wa haki za binadamu.nakupa like kama buku hivi,nakuomba tu mkuu tafuta na wewe sare za jeshi(kama huna),vaa katiza mitaa na uingie kwenye kumi na saba...nadhani utaweza sana kutetea unchotetea.usikalie tu kubwabwaja humu jf.vaa kombati ingia kitaa.usisahu ipad yako au simu yako kwa ajili ya kuturushia updates ukiwa ndani ya 18 za wazee wa sumu.nadhani utakuwa mtetezi mzuri sana baada ya hapo.

kila la kheri mkuu,nasubiri updates

Mkuu rai yako unayotoa ni sawa na kuwaambia mawakili wasisitee watu wanaotuhumiwa na makosa / wahalifu kwa kuwa tu wamefanya makosa (kinachofanyika ni taratibu zifuatwe kuhakikisha alievaa sare zinazofanana na jeshi achukuliwe sheria)

Mkuu Tanzania ni zaidi uijuavyo maana kuna watu wapo mjini humu lakini taarifa kwamba za kwamba nguo zinazofanana na kijeshi zimepigwa marufuku hawana hivyo wakati mwingine mkwara unatakiwa ili asirudie lakini usipitilize, kama angekutwa ndani ya kambi ya jeshi sijui ingekuaje
 
Mkuu rai yako unayotoa ni sawa na kuwaambia mawakili wasisitee watu wanaotuhumiwa na makosa / wahalifu kwa kuwa tu wamefanya makosa (kinachofanyika ni taratibu zifuatwe kuhakikisha alievaa sare zinazofanana na jeshi achukuliwe sheria)

Sasa vaa na ww uktane na mm uone kma ntakchkulia hatua stahiki au ntakuvunja mbavu
 
Tunaweza kushabikia na kufuraishwa na kitendo kijana mmoja alielazimishwa kuoga maji machafu kwa kosa la kuvaa sare za jeshi. Kimsingi ni kosa kuvaa sare hizo lakini ikumbukwe kua ipo sheria na chombo husika kinacho husika tena kwa kufata utaratibu na kumuhukumu mkosaji kwa kuvunja sheria zilizowekwa na si kujichukulia sheria mkononi na kumzalilisha kiasi kile. Mambo kama haya tunapaswa kuyachukia na kuyakemea maana ni kinyume na haki za binadamu, na tukio kama hilo linaweza lisikutokee wewe bali likamkuta ndugu yako au rafiki wa karibu je utashabikia?
 
Attachments

  • 1413549475669.jpg
    1413549475669.jpg
    26.2 KB · Views: 153
Back
Top Bottom