Aongeza wake kutoka 86 hadi 107

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,972
3,830
LAGOS, Nigeria
MUUMINI wa dini ya kiislamu anayetibu kwa tiba za jadi katika mji wa Bida, Nigeria, Bello Maasaba, ambaye alikamatwa kwa kuoa wake 86, ameendelea kuoa na kufikisha wake 107. Taarifa zilisema Maasaba (87) mwenye watoto 185, Septemba 2008, alikamatwa na kuwekwa jela kwa tuhuma za kuoa wanawake 86, ambapo serikali ya eneo hilo inayofuata sheria za kiislamu ilimlazimisha awaache wake 82 na kubaki na wake wanne. Hata hivyo alitolewa jela baada ya wake zake kuandamana, na wengine 57 kutoa ushahidi mahakamani kwamba waliolewa kwa ridhaa yao.

Maasaba ambaye familia yake imeelezwa kuwa na zaidi ya watu 5,000, alisema katika miaka ya 1970 alipokea ufunuo toka kwa Mungu, ukimuelekeza awe mganga wa jadi na aowe wake wengi. “Nilipokea ufunuo toka kwa Mungu ukiniagiza kuoa wake wengi. Kama ingekuwa siyo ufunuo wa Mungu, ningeowa wake wasiozidi wawili,” alisema Maasaba. Hata hivyo amekuwa akipambana na utawala unao ongozwa kwa misingi ya sheria za kiislamu katika mji wa Bida, ambapo mwanamume wa kiislamu anaruhusiwa kuoa wake wasiozidi wanne. Taarifa zingine zilisema kuwa kwa sasa Maasaba anaishi na wake 89, mke mdogo ana umri wa miaka 19 na mke mkubwa ana umri wa miaka 64. Maasaba ambaye anaishi kwenye nyumba ya vyumba 89, wake tisa kati ya 107 walifariki dunia na wengine 12 aliwaacha kwa utovu wa nidhamu. Taarifa zilisema kati ya watoto wake 185, watoto 133 maisha yao siyo mazuri kutokana na kuumwa, na amewakataza kupata matibabu hospitali, akidai tiba yake ndiyo sahihi. Alisema mtu yeyote katika familia yake anayepatwa na ugonjwa anatakiwa kuripoti kwake ili amuombee. Maasaba alisema familia yake inafahamu atakayekwenda kinyume na maagizo yake, atapata uvumbe mwilini utakamsababishia kifo.


source:Aongeza wake kutoka 86 hadi 107
 
king mswati wa swaziland anao wake 13 lakini pia aliyekuwa swahiba wake mkuu alikuwa anamsaidia, sasa huyu mwenye 107 nafikiri pia atakuwa anasaidiwa ?
 
ajue pia ameongeza wanaume. kwani lazima anaibiwa huyo kibabu
 
Back
Top Bottom