Aomba gharama za kumtunza Dk Mahanga gerezani

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,667
1,566
mahanga.jpg


Dar es Salaam
Aliyekuwa Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga huenda akafungwa mwaka mmoja jela iwapo atashindwa kulipia Sh 47 milioni za gharama ya kesi aliyoifungua Mahakama Kuu kupinga taarifa na habari zilizoandikwa dhidi yake kwamba elimu yake ni feki.

Dk Mahanga ambaye kwa sasa ni kada Chadema alifungua kesi hiyo mwaka 2009 baada ya gazeti la Nipashe kuandika habari kuwa elimu yake ni feki, ikinukuu kitabu cha 'mafisadi wa elimu' kilichoandikwa na Kainerugaba Msemakweli na kutaja orodha ya wabunge akiwamo Dk Mahanga ambaye wakati huo alikuwa naibu waziri.

Kutokana na kushindwa kulipa gharama za kesi hiyo, Desemba 2 mwaka huu,- Ofisi ya Msajili wa Mahakama Kuu imemuandikia barua Mkuu wa Gereza Kuu la Ukonga kutaka kujua maombi ya makisio ya gharama za kumtunza mfungwa wa kesi ya madai namba 145 ya 2009 ambaye ni Dk Mahanga.

Sehemu ya barua hiyo yenye kichwa cha habari ?Maombi ya makisio ya gharama za kumtunza mfungwa kwa kesi ya madai namba 145/2009? inasema, "...Mshinda tuzo ndugu Kainerugaba Msemakweli ameleta maombi ya kutaka mdaiwa Dk Makongoro Mahanga atumikie kifungo kama mfungwa wa kesi za madai. Tafadhali nijulishe makadirio ya gharama za kumtunza mfungwa wa kesi za madai kwa siku."

Katika kesi hiyo, Dk Mahanga anatakiwa kumlipa Msemakweli Sh 14 milioni na mwandishi wa habari aliyeandika habari hiyo, Muhibu Said Sh 33 milioni.

Dk Mahanga alipoulizwa juu ya suala hilo alisema hana taarifa zozote na anaweza kulipa fedha hizo na kukwepa kwenda jela.

Msemakweli ambaye pia ni mwanasheria alisema jana kuwa baada ya Dk Mahanga kutoonekana, Mahakama Kuu iliamuru mlalamikaji alipe gharama za kesi.

Muhibu alisema, "Ninachotaka kuona kikifanyika ni kufuatwa kwa sheria tu na mhusika (Dk Mahanga) atekeleze kila anachopaswa kukifanya kwa mujibu wa sheria.

Chanzo: Mwananchi
 
Hivi alishitakiwa na CCM, na je kesi imefunguliwa akisa mwanachama wa CDM. Kama maswali yote mawili jibu ni hapana kwa nini tunadhani ni jambl lenye tija kutetea watu kwa misingi ya vyma vyao na siyo makosa yao?
 
Hukumu iliahatoka amlipe ila hajalipa.
Na ilitoka kipindi bado ni waziri
Nahis hujamwelewa kamanda TAWA, kwa nini hizi hatua za kuuliza gharama gerezani haikuwa kipindi hicho mpaka wanakuja kufufua kesi kipindi hiki?
 
Hivi alishitakiwa na CCM, na je kesi imefunguliwa akisa mwanachama wa CDM. Kama maswali yote mawili jibu ni hapana kwa nini tunadhani ni jambl lenye tija kutetea watu kwa misingi ya vyma vyao na siyo makosa yao?

Kuna nyakati huwa naona kichefu chefu kwa baadhi ya comments... Ila watu wa aina yako huwa wananipa TIBA sahihi sn... HONGERA
 
Mwendo wa kulipa kisasi kwa walioisaliti ccm. Kweli ccm ni ileile

Sasa Hapo Nani Analipiza Kisasi?Kwan Huyo Msemakweli Ni Kajitangaza Yeye Ni Kada Wa Chama Gani?
Kwahiyo Kada Wa Ukawa Hatakiwi Kushtakiwa Kesi Tu Alishabikia Ukawa?
Ukawa Vipi?Nani Amewaloga?
 
Back
Top Bottom