Anti-Social wenzangu tujuane tabia zetu

Kutokana na kura ya Da'Vinci kutokea katika uzi mwingine inatuongezea idadi kutoka 11 kuwa 12 waliojibu na 11 kati yao wameendana na nadharia.

Nadharia imepredict kwa usahihi kwa asilimia 91.6% hadi hivi sasa.

Kumbuka bado tunalisubiri jibu la Kunguru wa Manzese kuthibitisha kama kweli alikuwa ako siriazi yeye ni extrovert na kidole gumba ni cha KUSHOTO!!!? Confirmation required ..... [Bias detected, data zilizoendana hata sijahangaika kucomfirm tena why😏. Lakini tuwe wakweli tu, nani kati yenu atamuamini moja kwa moja kila anachokisema mwamba liyejipa A.K.A kwa jina Kunguru wa Manzese?? - mi nimewaza anatania at best]

Huyu akibadili upepo tunakuwa na uhakika wa asilimia mia kuwa ni namna ya uelekeo wa kufikiri inayopelekea mtu apende kuzungukwa na mambo mengi au la. Na hii isituchanganye maana machoni pa introvert[wengine husema highly sensitive person] hivyo vichache ni vina mengi tu ya kutosha.
Atakuwa labda ni ambivert
 
Asante

Ubao sasa unasoma 13/15* 100 = 86.7% right

Basi mnaonaje tukiamua kustate kwamba ni fact kuwa hao introverted [walioitwa kimakosa antisocials] ni matokeo ya wao kupenda kutumia ubongo wa kushoto zaidi kuliko wa kulia katika maamuzi yao hata yale ya harakaharaka.

Kutokana na upande huo kupenda kuchakata na kupambanua facts nyingi basi wamejikuta wakipendelea mazingiranyenye vitu/watu wachache wa kuchakata.

Haikatai wao kusimama hadharani na kutema madini/kuhutubia watu wengi katika maeneo rasmi maana katika standard situations hawahitaji kuchakata data nyingi. Kimbembe huja katika casual situations ambapo hakuna sheria bali mambo huenda kwa flow tu🤦‍♂️. Hapa wale watumiao ubongo wa kulia zaidi hupapenda maana ndio mambo yao sasa. Hao huitwa extroverts..........

Au basi, utafiti uendelee kichinichini🐣
 
Atakuwa labda ni ambivert
Yas kweli inawezekana maana haya mambo sio kanuni kali ni kama spectrum au continuuum fulani. Na kila mmoja anao ulefthandedness kiasi na urighthandedness kiasi fulani........ namaanisha huo wa ufikiri sio ule wa kulia chakula mazee
 
Sometimes I hate people
Finding and reading more good stories of people around the world usually helps.

Lakini pia tafuta kuwaelewa watu zaidi kuliko kuwasamehe au kuwachunguza tu.

Wanaotumia sana hiyo kushoto ni rahisi zaidi kuwa optimistic, lakini wakiwa pessimistic ni hatari maana paranoia kwao ni ya kugusa tu.

Hata wa kulia naye kuathiriwa na paranoia inawezekana ni rahisi pia sina data, lakini cha msingi cha kufanyia kazi kwa wote ni TAFUTA KUJIJAZA NA MATAARIFA MAZURIMAZURI YA WATU AROUND YOU
 
Sijui kama na fit kwenye kundi hili au la. Ni hivi
Sipendi kuangalia TV Kabisa. Naangalia pale tu kukiwa na tukio maalum. Pia nikipata TV series nzuri za action like NCIS la huwa naangalia

Sipendi soka! Napenda michezo lakini sio soka. Rafik zangu hunishangaa nikikaa naangalia marathon live au F1. Boxing napenda pia ila inakua mida mibaya

Sipendi kwenda kwenye sherehe hasa harusi. Ratiba zake hazina ubunifu, mambo ni yale yale tangu Enzi za kale.

Nina marafiki wachache sana na hata Hao inaweza kupita siku kadhaa hatujawasiliana. Hawana shida maana na wao ni Kama mimi tu kitabia. Muda wangu nautumia kusoma vitabu au kucheki educative video YouTube na vimeo.

Sipendi kukaa sehemu yenye watu wengi. Hata nikisafiri natafuta hotel zile ndogo zenye utulivu.

Sipendi sana kutumia simu, hasa sms. Simu yangu ni Nokia. Natumia Tab mara chache haizidi saa 2 kwa siku. Tab natumia kucheki JF na reddit. Nikiwa safarini naitumia kucheza sudoku na chess

Nalala mapema sana. Nadra kunikuta macho baada ya saa 3 usiku. Leo niko macho kwa sababu namsubiri wife na mamake wako harusini, mi niko nje kwenye gari nawasubiri

Nitaongezea ...
 
Niende moja kwa moja kwenye mada, nina vitabia ambavyo ni ngumu kunibadilisha na kujibadilisha,
(1) Sipendi kuangalia TV, utaniona kwenye TV hasa kukiwa na mpira wa miguu vinginevyo mie ni mtu wa redio kwa sana, tena hasa TBC TAIFA na vipindi vyangu vile taarifa za habari, hotuba za baba wa taifa, muziki wa zilipendwa ukichambuliwa na MASOUD MASOUD mie kwangu burudani kabisa.

(2) Mwanamke/Msichana akijipodoa sana kwangu anaboa. Akijitoboa pua yake hata kutazama sura naogopa kabisa, akijifunga vikuu miguuni ananiboa, n.k.Napenda sana Mwanamke awe Natural, yaani aoge zake apake mafuta yake ya nazi na kumchana nywele zake au asile twende kilioni

(3) Sherehe Sherehe hizi sijui za Ndoa, Birthday DAAAH hizo ndio sizipendagi kabisa, kama ndoa nitaishia kutoa mchango tu lakini ukumbini hunioni. Kichwani naona kama kupotezeana muda tu, watu wanaonyeshana uzuri wao, mavazi yao, na ratiba nyingi zisizo na kichwa wala miguu.

(4)Nipo DSM kwa zaidi ya miaka 20 tokea nipo Form 1 sijatoka tena lakini kwenda Beach kujipumzisha hata mara 10 hazifiki. Hayo maonyesho ya Sabasaba hata viwanja vyenyewe sijawahi kukanyaga, n.k.

Kwa ufupi kama sina Issue ya kunitoa Home, nitakaa tu na watoto wangu wanafanya home work zao za shule mie nipo pembeni yao nasoma vitabu vyangu vya riwaya tu vya akina Willy Gamba, Ben Mtobwa,Hammie Rajab, John Simbamwene, n.k nikichoka Riwaya nitarukia vitabu vya akina Kiyosaki,Robin Sharma.

NAENJOY maisha yangu
Huna makuu, ni maisha mazuri!
 
Mimi nina tabia ambayo sijui inaweza kuwekwa kwenye kundi gani kisaikolojia, sipendi na nachukia mikufu, sipendi dhahabu wala shaba au madini yoyote, huwa sielewi kwanini dhahabu iwe na thamani.
Unaona mtu ametia mikufu au bling bling anaonekana kama anayependeza kwa watu ila kwangu mimi nachukia sana hivyo vitu.
 
Mie napenda sana kuangalia movie, kuchati online na watu nisiowajua, kusikiliza miziki, kutomb na kusoma vitabu vyenye story za kusisimua. Sitaki kuamini mimi ni ant social ila kitendo cha kuwa busy na ma movie na vitu vingine vikanipelekea kuwa anti social. Nikiwa mbele za watu nikawa nakosa vya kuchangia, inakuletea uoga kuwa nikisema jambo nitakuwa nakosea. .

Nikaja kugundua life style yangu inanipeleka pabaya nikaanza kujenga mzoea na watu mpaka imekuwa kero. Nikitembea kilometers moja nishasalimiana na kila mtu na wamenipachika jina MWENYEKITI. Watu wa mtaani wanataka sana niwe mwenyekiti wao wa serikali za mtaa. .

Kuwa anti social sio maana ya kuwa usisalimiane na watu, kikubwa ni kusimamia au ku balance watu wa msingi wawepo kwenye circle yako. Kuna mda unasikia mtu kajiua kuwa mwenyewe na kujiaminisha huhitaji wengine ni jambo la kuangalia kwa jicho la tatu. .
Pengine hujatambua karama na vipawa vyako. Kama wanaokuzunguka wanataka uwe kiongizi wao, basi kuna jambo hapo, pengine una mawazo chanya na ni mtatuzi wa changamoto japo kwa maneno.
 
Mwaka 2005 ilikuwa mwisho wangu kujihusisha na dini/ibada na ni baada ya padri kukataa kumzika classmate.

Sijawahi na sitowahi kuwakubali ccm au yanga/utopolo.

Sipendi kuongea sana hivyo ukinikuta na mtu ujue ni mtulivu kama mimi.

Nashabikia simba na ni mwanachama mkubwa tu ila sijawahi kuvaa jezi ya simba toka utotoni.

Sijawahi kuvaa nguo yenye maandishi au picha au mchoro wowote.

Mimi ni ngumi mkononi na nikipiga ni moja tu.

Sijawahi hudhuria sherehe yoyote, nikienda msibani sijawahi kutazama maiti.

Barabarani ukinizingua nakufata hadi ukipark nakueleza. Ukibishana nakupasua.
Hili ni tatizo la akili.
 
No. Mnalitumia visivyo neno ant-social: Anti-social behaviours are actions that harm or lack consideration for the well-being of others. It has also been defined as any type of conduct that violates the basic rights of another person and any behaviour that is considered to be disruptive to others in society

Mimi sichangamani na watu sana bila mpango na sipendi vyanzo vyote vya uongo ikiwamo drama, habari na udaku.

Nikikaa na mtu/watu napenda yawe ni mazingira ya usawa na majadiliano au mabishano kuliko umbea na udaku.

Napenda uchambuzi wa kina na mda mwingine naandika mada zangu mwenyewe na kuzichambua mwenyewe.

Siyumbishwi kama upepo na point zangu huwa zinajisimamia zenyewe kimamlaka hadi mtu kama hajawahi kuniona anahisigi ni jitu kuuuuubwa kuliko mm mwenyewe nilivyo.

Napenda dunia na jamii iwe mahala pazuri/edeni/mbinguni na kazi zangu maandiko yangu yana uelekeo huohuo --Hence ni PRO- SOCIAL kabisakabisaa
Uelewa wangu juu ya anti social ulikuwa kama wa wengi wa wachangiaji zamani, Ila nilijifunza hapa JF kwenye uzi wenye mada kama hii.
 
Anti-social halafu una smart phone!!!??? Wewe una matatizo yako ya kisaikolojia tu, katafute mshauri nasihi akusaidie.
Tena mwingine anasema ni anti-social lakini anashinda kwenye social media. Watanzania kuna tatizo mahali.
Maana halisi ya hiyo Hali inawapiga chenga wengi.
 
We unadhani kama hatafuti pesa anaishije ndugu?
Kwa misongo ya mawazo kama hiyo, hadi anataka mwanamke awe natural amekua mali asili kwani?
Unajifungiaje ndani weekend kama unazo hela, zipo sehemu tele zilizotulia Mtu kama una Laki yako tu mfukoni unaenda kutulia huko bila bugudha,

Umaskini mbayaaaaaaaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom