Animators,Still & motion Graphics Designers,Mnaononaje Hapo?

kadoda11

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
21,453
20,712
Katika hii video,nimetumia Adobe AE CS5.Effects nilizo apply ni Light Layer,Shatter,Lens Flare na Ramp.Najua mabingwa tupo wengi wa haya mambo so napenda ku-share nanyi mawili matatu.je nimejaribu au nimechemsaha?nategemea changamoto na maarifa zaidi toka kwenu.
 
Last edited by a moderator:
mkikaa kimya sana,nashawishika kuamini ile kauli ya jamaa yangu mmoja pale alipo nambia wajuzi wa adobe after effect kwa bongo tupo wachache sana.asilimia kubwa ni watoto wa kihindi na ndio hao wanaotengeza matangazo makubwa ya tigo,vodacom na airtel tunayo yaona mara kwa mara ktk TV zetu huko nyumbani.NI MTIZAMO TU.
 
Nice try.

Concerns zangu ni:
Layer (foreground) ambayo imekuwa shattered imekaa kwa muda mfupi sana. Ungeipa kama sekunde mbili hivi ndipo isambaratike ili mtazamaji awe ameshtukizwa. Red ya background uliyoiwekea ramp ingeweza kufifia zaidi ili "KADODA" ionekane zaidi. Font uliyotumia (Nadhani ni Bimini) siyo attractive sana katika video hii. Nafikiri japo Arial ni common lakini ingeweza kufaa kuliko Bimini.

Mwisho wa siku inategemea na ulichotaka kuachieve, you may be right in some respect. Ila ningependa quality ya shattering iwe kama ya video namba 70 na 104 katika mtandao huu VIDEO COPILOT | After Effects Tutorials, Plug-ins and Stock Footage for Post Production Professionals
 
Kuna ukweli mkubwa katika haya unayosema. Lakini nyie wachache mbona kazi zenu hatuzioni? Hata hao wahindi kazi zao ziko wapi? Mara utasikia kuna jamaa mmoja ni noma, mara kuna mhindi fulani ni soo... jamani sanaa ni maonesho si maneno.. Onesheni mlichofanya, mbona mnaishia kuongea tu.
 
kaka nimekuelewa na nashukuru kwa ushauri wako mzuri,ila kutaka quality ya shatter effect iwe kama ya endrew kremer wa video copilot kunahitaji maaarifa zaidi.i'm an amature on this.cant compare myself with guys in video copilot led by endrew kremer....i shall try.
 
uwezo tunao ila kupata project deal kubwa ya kutengenza matangazo kama hayo ya mitandao ya simu za mkononi kunahitaji kufahamiana na watu.wahindi ndio wame-dominate ktk anga hizo.kwa upande wangu namshukuru mungu nina kamtandao ka client ambao wananikubari.
 
gud start, biashara ni matangazo safii, mimi pia napenda hii kitu bt cjui nianzie wapi
 
kaka nimekuelewa na nashukuru kwa ushauri wako mzuri,ila kutaka quality ya shatter effect iwe kama ya endrew kremer wa video copilot kunahitaji maaarifa zaidi.i'm an amature on this.cant compare myself with guys in video copilot led by endrew kremer....i shall try.

Ni kweli lakini mimi sikubaliani na kuanzia viwango vya chini sana. Jifunze kwa kutumia tutorials ambazo ni za viwango kama vya Andrew K. Bahati nzuri jamaa anafundisha vizuri sana hivyo huna cha kujitetea. Tutorials nzuri zipo sasa kwanini wewe ujifunze "tu-effect tudogotudogo." Niambie sababu ya wewe kutojifunza kwa Andrew badala yake unapambana mwenyewe halafu.... aisee sisikilizi maelezo unless uniambie hudhani bongo yako inaweza mchakamchaka wa A Kramer. Kadoda usianzie chini sana bana. Chukua tutorials nzuri tu, kesha usiku, punguza muda wa kuwa baa na kupiga soga. Nataka mwakani uniletee muvi ya Avatar. Sitaki maneno mimi.
 
uwezo tunao ila kupata project deal kubwa ya kutengenza matangazo kama hayo ya mitandao ya simu za mkononi kunahitaji kufahamiana na watu.wahindi ndio wame-dominate ktk anga hizo.kwa upande wangu namshukuru mungu nina kamtandao ka client ambao wananikubari.

Si kweli.

Hao wanaopewa madili makubwa kwa kawaida si Watanzania (wawe weusi ama wahindi) kwa sababu wengi wa Watz hatuwezi. Tangazo la tiGo la "Yap Yap Ebwanaee" limetengenezwa nchini India kwa sababu akina kadoda11 mnajifunza vitu vidogo vidogo. Tangazo la Chui la Serengeti limetengenezwa na Wahindi ambao sidhani kama ni Watanzania. Tangazo la EPIC Bongo Star Search limetengezwa na kampuni ya Aggrey&Clifford, ni ya Tanzania hii. Wamepewa kwa kuwa wameonesha wanachoweza kufanya na wakakubalika. Wamepewa pia deal la kufanya PR za NHC, soma mtandao wao. Lalamika tu.

Ukitengeneza kitu kizuri sana hata "wachawi" wanakiogopa. Nani akunyime deal ikiwa umetengeneza kitu maridadi sana? Watu wanataka vitu vizuri. Tengeneza muvi kali sana uza Ulaya.

Hizi kauli za "kibongobongo si mbaya sana" sitaki kabisa kuzisikia. Tengeneza kitu ambacho ni world class.

Naendelea kukuchana zaidi.
Jifunze vitu vizuri vikoje, rangi zake, sauti zake, mwendo wake. Jifunze Sanaa na Sayansi ya uzuri. Soma vitabu, tazama tutorials. Changamsha bongo na utumie akili yako hadi mwisho wake kwa sababu hutaitumia ukiishakufa, sasa upo duniani kwanini unajifunza vitu vidogo vidogo? Come-on man, fire up your brain. Washa moto.

Tangeneza kitu kizuri kupindukia kisha lalamika hujapewa deals kubwa. Malalamiko weka pembeni. Rudi darasani kwa Mwalimu Andrew Kramer, wengine ndo tunavyofanya.

BORA WEWE UMESEMA UNA KA-MTANDAO KADOGO KA CLIENTS WAKO, MIMI SINA KABISA MTANDAO, ILA MIONGONI MWA WATEJA NITAKAOWACHUKUA NI HAO WA MTANDAO WAKO, SERIOUSLY.

Ndo nimeshasema hivyo.
 
Yaani mi ndo nataka anza adobe premiere 3 sema sijui wapi nianzie
hebu help me out kwani najaribu hata kuweka video kwenye hiyo adobe ila nimeshindwa ila kupitia nyie hopefully nitaweza jifunza kidogo
 
kadoda11, kazi yako ninaikubali ila kama Magembe R. Malima alivyosema, hiyo font uliyotumia hapo juu haijapendezea. hata arial bado isingefurahisha, sipendi kutumia native adobe fonts (na nina extended adobe fonts). kwanini usidownload and install free fonts ambazo utaona unique? nakupa na link ya sehemu mi hupata baadhi ya fonts usipate sababu ya kutobadilisha hiyo font :biggrin: FONTS, FREE FONTS, DOWNLOAD FREE FONTS FOR WINDOWS.
kuhusu foreground, hapo sijakubaliana na mkuu Magembe kuhusu kudelay shutter ya foreground, but then opinions always differ. nakubaliana na Magembe kuhusu quality ya shuttering (hata kama sijaona hizo examples alizotoa), for one ningependa u slow the rate ambapo the stars fall off. all in all, a good project
 
Last edited by a moderator:
kadoda11 kazi ni nzuri sema wadau waliopita wanashindwa kukubali moja kwa moja kwa sababu kazi hiyo haina uhusiano na kitu au tukio flani la moja kwa moja lakini kama ingehusihwa na kitu flani ambacho wengi tunakifahamu ingekua poa ila kazi nzuri.....lakini FOnT haijatulia. Keep It Up Kazana sana
 
Last edited by a moderator:
mkikaa kimya sana,nashawishika kuamini ile kauli ya jamaa yangu mmoja pale alipo nambia wajuzi wa adobe after effect kwa bongo tupo wachache sana.asilimia kubwa ni watoto wa kihindi na ndio hao wanaotengeza matangazo makubwa ya tigo,vodacom na airtel tunayo yaona mara kwa mara ktk TV zetu huko nyumbani.NI MTIZAMO TU.
ngoja niiangalie nikupe review zangu
 
kadoda11 nimeshindwa kujudge coz kwanza nimeona nyota zinalipuka, then jina lako lina roll over...

lilivyoanza tu nikapata mawazo ya marekani coz ndo bendera yenye nyota nyingi,

nadhani creation yako imelack creativity na originality, i mean vile vitu ambavyo mtu akiona tu anatamani aone tena,

you have future but you have to work hard, n be creative sana....
kama una video nyingine impress me...

kwenye scale ya 1-10 umepata 4 (fairly enough)
 
Last edited by a moderator:
kadoda11,
nice try unaijua Roxio?
I think it's better than Adobe.
 
Ni kweli lakini mimi sikubaliani na kuanzia viwango vya chini sana. Jifunze kwa kutumia tutorials ambazo ni za viwango kama vya Andrew K. Bahati nzuri jamaa anafundisha vizuri sana hivyo huna cha kujitetea. Tutorials nzuri zipo sasa kwanini wewe ujifunze "tu-effect tudogotudogo." Niambie sababu ya wewe kutojifunza kwa Andrew badala yake unapambana mwenyewe halafu.... aisee sisikilizi maelezo unless uniambie hudhani bongo yako inaweza mchakamchaka wa A Kramer. Kadoda usianzie chini sana bana. Chukua tutorials nzuri tu, kesha usiku, punguza muda wa kuwa baa na kupiga soga. Nataka mwakani uniletee muvi ya Avatar. Sitaki maneno mimi.
labda tuu nijitee kaka,ni hivi ktk moja ya watu ambao napoteza wakati wangu mwingi kufuatilia sana tutorial zao ni endrew kremer.na kuhusu kusema eti najifunza tu-effect tudogo tudogo hiyo nayo siyo kweli.ninachofahamu mimi ktk talent ya motion graphics hakuna kitu kinachoitwa effect ndongo.ni ubinifu wa kuunda kitu ndio uta-determine uwezo wa effect.kila effect ina aina yake ya matumizi.
 
Si kweli.

Hao wanaopewa madili makubwa kwa kawaida si Watanzania (wawe weusi ama wahindi) kwa sababu wengi wa Watz hatuwezi. Tangazo la tiGo la "Yap Yap Ebwanaee" limetengenezwa nchini India kwa sababu akina kadoda11 mnajifunza vitu vidogo vidogo. Tangazo la Chui la Serengeti limetengenezwa na Wahindi ambao sidhani kama ni Watanzania. Tangazo la EPIC Bongo Star Search limetengezwa na kampuni ya Aggrey&Clifford, ni ya Tanzania hii. Wamepewa kwa kuwa wameonesha wanachoweza kufanya na wakakubalika. Wamepewa pia deal la kufanya PR za NHC, soma mtandao wao. Lalamika tu.

Ukitengeneza kitu kizuri sana hata "wachawi" wanakiogopa. Nani akunyime deal ikiwa umetengeneza kitu maridadi sana? Watu wanataka vitu vizuri. Tengeneza muvi kali sana uza Ulaya.

Hizi kauli za "kibongobongo si mbaya sana" sitaki kabisa kuzisikia. Tengeneza kitu ambacho ni world class.

Naendelea kukuchana zaidi.
Jifunze vitu vizuri vikoje, rangi zake, sauti zake, mwendo wake. Jifunze Sanaa na Sayansi ya uzuri. Soma vitabu, tazama tutorials. Changamsha bongo na utumie akili yako hadi mwisho wake kwa sababu hutaitumia ukiishakufa, sasa upo duniani kwanini unajifunza vitu vidogo vidogo? Come-on man, fire up your brain. Washa moto.

Tangeneza kitu kizuri kupindukia kisha lalamika hujapewa deals kubwa. Malalamiko weka pembeni. Rudi darasani kwa Mwalimu Andrew Kramer, wengine ndo tunavyofanya.

BORA WEWE UMESEMA UNA KA-MTANDAO KADOGO KA CLIENTS WAKO, MIMI SINA KABISA MTANDAO, ILA MIONGONI MWA WATEJA NITAKAOWACHUKUA NI HAO WA MTANDAO WAKO, SERIOUSLY.

Ndo nimeshasema hivyo.
sawa critic wangu.kwa upande flani upo sawa na kwa upande mwingine haupo sawa.BTW natamani kuona kazi yako hata moja.haya nichambue tena na hapo .
 
Last edited by a moderator:
kadoda11,
nice try unaijua Roxio?
I think it's better than Adobe.
asante mkubwa.kama unaniuliza ile Roxio ya ku-burn VCD/DVD hiyo naifahamu,lakini kama unaniluliza yenye uwezo wa kufanya 2D & 3D Modelling hiyo siifahamu mkubwa.mimi nafahamu Maya,3D Studio Max,cinema 4D,Adobe AE,Brender nk.
 
kadoda11 nimeshindwa kujudge coz kwanza nimeona nyota zinalipuka, then jina lako lina roll over...

lilivyoanza tu nikapata mawazo ya marekani coz ndo bendera yenye nyota nyingi,

nadhani creation yako imelack creativity na originality, i mean vile vitu ambavyo mtu akiona tu anatamani aone tena,

you have future but you have to work hard, n be creative sana....
kama una video nyingine impress me...

kwenye scale ya 1-10 umepata 4 (fairly enough)
sawa kiongozi,asante kwa maneno yako mazuri yenye kuniongezea ari.hiyo kitu niliifanya harakaharaka.najipanga kufanya kitu kikubwa zaidi na ninahaidi kukileta hapa ili mki-jugde.video nyingine ni hii hapa niliifanya kitambo kidogo.naomba uitazame.
 
Last edited by a moderator:
kadoda11 kazi ni nzuri sema wadau waliopita wanashindwa kukubali moja kwa moja kwa sababu kazi hiyo haina uhusiano na kitu au tukio flani la moja kwa moja lakini kama ingehusihwa na kitu flani ambacho wengi tunakifahamu ingekua poa ila kazi nzuri.....lakini FOnT haijatulia. Keep It Up Kazana sana
asante kaka,kuhusu font next time nitachangua font za aina nyingine.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom