Jazzie
Member
- Jan 30, 2008
- 73
- 35
Acts 13:36 For when David had served God's purpose in his own generation, he fell asleep; he was buried with his fathers and his body decayed
Ni ukweli usiopingika kwamba kila kizazi kinahitaji kiongozi wake. Hiyo ni kwa sababu kila kizazi kina matatizo yake, maono yake, na matakwa yake. Ni ukweli usiopingika kwamba kizazi cha Tanzania leo hii kina kiu ya kiongozi wake.
Kwa muda ilionekana kama vile kuna vijana wawili January Makamba and Zitto Kabwe, ambao walikuwa tayari kubeba jukumu la kusimama kama nyota ya uongozi wa kizazi kipya. Kili mmoja wetu anajua kilichojiri Bungeni hivi karibuni, hasa uamuzi wa January Makamba kupingana na hatua aliyoingoza Zitto Kabwe ya kudai uwajibikaji serikalini.
Ni dhahiri, ingawa wengine wanaweza kuwa na maoni tofauti, kwamba January amejiweka katika wakati mgumu kisiasa, hasa mbele ya vijana waliomtegemea.
Kwa muda January Makamba aliweza kungara katika anga za siasa Tanzania kwa sababu ya uwezo wa kupambanua mambo. Lakini kilichotokea Bungeni kimedhihirisha kitu kimoja uwezo wa January kupambanua mambo na kutoa kauli zilizoenda shule peke yake hakumfanyi mtu kuwa kiongozi na shujaa wa kizazi chake. Kuna wakati na mazingira yanamtaka kiongozi kudhihirisha mawazo na moyo wake ulipo.
Pale Bungeni, wakati huo ulitokea na bahati mbaya sana January akaugopa wakati huo.
Pale mjengoni, January Makamba alidhihirisha kwamba mawazo yake na moyo wake yako mbali kama Mashariki iliyo mbali na Magharibi. Na ndio maana dhana ya unafiki inamzonga January. Katika utetezi wake, January Makamba aliandika hiki hapa chini:
"I can disagree with Zittokabwe on methods to reach the same objectives, and we are still brothers"
Mpaka leo sijasikia chochote toka kwa January kuhusu njia mbadala (tofauti na njia aliyopendekeza Zitto Kabwe) ya kuleta uwajibikaji serikalini. Kwa mantiki hiyo, hiyo kauli yake hapo juu ilikuwa ni jitihada tu ya kuzima zengwe na jinamizi la kisiasa linalomkabili.
What a waste.

Last edited by a moderator: