Angelina Jolie aanza kusumbuliwa na Mama wa mtoto aliyemuasili

Habari za wakati huu wa dau wa jukwaa hili.

Nilikua napitia katika mitandao ya kijamii, nikakutana na hii habari ya huyu mlimbwende Angelina Jolie.
Ya kwamba aliadopt watoto, mmoja wapo anatokea Ethiopia anaitwa Zahara, tangu kakiwa kachanga kabisa kama miezi mitano hivi.

So hiyo tu na watoto wengine pia kama watu hivi, kuna wa kiume mwenye asili ya Asia na Kuna mwingine mzungu.

Na amekua akiwatunza mpaka Sasa, kasheshe inakuja Kwa huyu Binti Toka Ethiopia, kwamba kashakua mzuri na mama yake anaanza kuleta longolongo kuhusu mwanawe, wakati Angelina Jolie alimchukua kama orphan yaani yatima.

Anyway sijui itaishia wapi.

Kwa anaefahamu au mwenye kujua zaidi tujadili japo kidogo,

1. Hivi sisi wabongo tunaweza fanya hiki alichofanya huyu Angelina Jolie? Jinsi tulivyo na miroho yetu ilivyo mibaya?

2. Sisi blacks mbona tunajidhalilisha sana, Kwa mfano huyu mama wa Zahara Binti wa Angelina Jolie,? Leo ndo anamuona mzuri? Zahara kanoga, kapendeza, na anafaa kabisa Kwa matumizi ya binadamu(Kwa sisi wanaume tu).

3 Binafsi nampongeza sana huyu Angelina Jolie Kwa alichokifanya kuadopt hao watoto, ningekua na uwezo Ile wa uumbaji basi huyu Pepo inamuhusu kabisa.

Mkuu kwa wabongo tunafanya au tuliwahi fanya hiyo mambo lakini kwakweli wabongo ni tatizo.
Mimi niliwahi kuasili watoto 3 wawili walikuwa ndugu na mmoja ni wa familia nyingine
Tatizo lilikuja pale wale wawili walipo fika chuo kikuu wana boom akijitokeza mtu kuwa ni mzazi wao na mambo kibaaao!
Nilipata usumbufu wa kila aina ikabidi niache watoto waamue kwasababu tayari ni wakubwa.

Akabaki 1 ambae sasa yupo kidato 4 huyu nae mlezi wake akaanza longolongo kwakuwa sipendi vyesi nikamburuza Ustawi wa jamii kwasababu sikumchukua mtoto kienyeji. Akasalim amri amuache mtoto asome Mtoto ataamua pa kwenda akifikisha miaka 18.

Kuasili watoto wa watu wasiojielewa ni mtihani.
Ukitaka kuasili nenda kaasili kutoka vituo vya watoto yatima tofauti na hapo fanya shughuli nyingine za kusaidia wasiojiweza. Lakini usiali mtoto mwenye wazazi hatakama hajiwezi kupindukia.
 
Mkuu kwa wabongo tunafanya au tuliwahi fanya hiyo mambo lakini kwakweli wabongo ni tatizo.
Mimi niliwahi kuasili watoto 3 wawili walikuwa ndugu na mmoja ni wa familia nyingine
Tatizo lilikuja pale wale wawili walipo fika chuo kikuu wana boom akijitokeza mtu kuwa ni mzazi wao na mambo kibaaao!
Nilipata usumbufu wa kila aina ikabidi niache watoto waamue kwasababu tayari ni wakubwa.

Akabaki 1 ambae sasa yupo kidato 4 huyu nae mlezi wake akaanza longolongo kwakuwa sipendagu vyesi nikamburuza Ustawi wa jamii kwasababu sikumchukua mtoto kienyeji. Akasalim amri amuache mtoto asome Mtoto ataamua pa kwenda akifikisha miaka 18.

Kuasili watoto wa watu wasiojielewa ni mtihani.
Ukitaka kuasili nenda kaasili kutoka vituo vya watoto yatima tofauti na hapo fanya shughuli nyingine za kusaidia wasiojiweza. Lakini usiali mtoto mwenye wazazi hatakama hajiwezi kupindukia.

Upo sahihi hapo pa "usiasili mtoto mwenye wazazi" kama maisha yao ni magumu sana msaidie akiwa hapo hapo kwa wazazi wake,

Pia huko kwenye vituo wengi wanalalamika masharti yao ni magumu sana inafanya watu wanashindwa kuasili watoto.
 
Stori na picha
 
Attachments

  • FB_IMG_1699340178273.jpg
    FB_IMG_1699340178273.jpg
    63.3 KB · Views: 3
  • FB_IMG_1699339645832.jpg
    FB_IMG_1699339645832.jpg
    51 KB · Views: 5
  • FB_IMG_1699339599018.jpg
    FB_IMG_1699339599018.jpg
    66.9 KB · Views: 3
  • 1699335721224.jpg
    1699335721224.jpg
    67.5 KB · Views: 5
Angelina Jolie aliadopt mtoto wa kwanza wa kiume nchini Cambodia, akaja kuadopt mwengine wa kiume nchini Vietnam, akaja kuadopt mtoto mwengine wa kike nchini Ethiopia, hakua peke yake kwenye safari hiyo alikua na aliyekua mumewe Brad Pitt waliadopt wote,

Kwa mtoto wa Ethiopia jina lake Zahara, Angelina alimkuta kituo cha kulea watoto yatima akiwa ana miezi 7 tu, wahusika wa kituo wakamwambia mtoto yule ni yatima wazazi wake walifariki kwa virusi vya Ukimwi, huruma ilimjaa Jolie na kuamua kumchukua kwa taratibu zote stahiki,

Ukweli ukaja kujulikana miaka mitatu baadae, mama mzazi wa Zahara alikua hai, ni binti aliyepata ujauzito kwa kubakwa, huku akiishi na bibi yake na mjomba wake wakiwa katika maisha ya ufukara, baada ya kumzaa Zahara hali ilizidi kua mbaya, Mama Zahara akatoroka nyumbani na kumuachia mtoto bibi yake, bibi nae kwa hofu ya kumkosa mtoto kutokana na lishe duni akampeleka kituo cha kulea watoto yatima na kuomba msaada wampokee mtoto, atakufa kwa njaa,

Mama mtoto alichokiomba ni kuongea na mwanae hata kwa njia ya simu, kumjulisha kua ana familia Ethiopia na mama yake hajafa pia anampenda sana.

Wala hakutaka kumchukua ampeleke wapi na umaskini bado umemtawala.
Hiyo haipo.........aende kule alikokimbilia si ndio alipaona bora
 
Wanamchanganya mtoto tu, na Angelina naye hawajamfanyia haki.

This is very selfish.

Ukishakubali kumtupa mtoto wako, umeshakubali, usitake tamaa za kuona mtoto kakua ukataka kuongea naye.

Very selfish mother.
Huyo mwanamke mpuuzi sana. Kama kweli angekua anampenda mtoto wake kama anavyosema si angekaa kimya kuliko kumsumbua kiakili na kumchanganya kwa sasa.
 
Angelina Jolie aliadopt mtoto wa kwanza wa kiume nchini Cambodia, akaja kuadopt mwengine wa kiume nchini Vietnam, akaja kuadopt mtoto mwengine wa kike nchini Ethiopia, hakua peke yake kwenye safari hiyo alikua na aliyekua mumewe Brad Pitt waliadopt wote,

Kwa mtoto wa Ethiopia jina lake Zahara, Angelina alimkuta kituo cha kulea watoto yatima akiwa ana miezi 7 tu, wahusika wa kituo wakamwambia mtoto yule ni yatima wazazi wake walifariki kwa virusi vya Ukimwi, huruma ilimjaa Jolie na kuamua kumchukua kwa taratibu zote stahiki,

Ukweli ukaja kujulikana miaka mitatu baadae, mama mzazi wa Zahara alikua hai, ni binti aliyepata ujauzito kwa kubakwa, huku akiishi na bibi yake na mjomba wake wakiwa katika maisha ya ufukara, baada ya kumzaa Zahara hali ilizidi kua mbaya, Mama Zahara akatoroka nyumbani na kumuachia mtoto bibi yake, bibi nae kwa hofu ya kumkosa mtoto kutokana na lishe duni akampeleka kituo cha kulea watoto yatima na kuomba msaada wampokee mtoto, atakufa kwa njaa,

Mama mtoto alichokiomba ni kuongea na mwanae hata kwa njia ya simu, kumjulisha kua ana familia Ethiopia na mama yake hajafa pia anampenda sana.

Wala hakutaka kumchukua ampeleke wapi na umaskini bado umemtawala.
Maza ni mpuuzi sana, alimtelekeza dogo afe njaa.
 
Dah!... umasikini ulaaniwe.
 
Back
Top Bottom