ANGALIZO Kwa CHADEMA: Kukaribiana na CCM Kisera ni hatari!

Sometime naona tunachanganyana kwenye maana ya bepari Vs ujamaanaubeari kinadharia na uhalisia wake kwenye nchi mbali mbali.

UK tunaijua wengi kama nchi ya kibepari toka zamani lakini . ukisoma soma wanavyoendesha mambo kihalisia kuna ujamaa mingi tu.

  • Single biggeest employer wa UK ni BAE ambyo ni kampuni ya kijeshi
  • Single biggest exporter wa UK ni BAE
  • Pubic sector nyingine ya ya afya UK nayo ukisoma ni kama ya kijamaa
  • Kuna wakati nilisoma kwenye elimu kulikuwa na sera shule binafsi zilizofanya vibaya zinawekwa chin ya uangalizi na usimamizi wa Serikali( ujamaa fulani)
  • Kampuni kama za BP ,British Telecom ,Britisha Airways historia zao inaonyesha zilikuwa chini ya usimamizi tena wa karibu wa serikali ( somehow kijamaa) mpaka miaka ya karibuni
  • Hata makampuni na mabenki yalyokuwa 100% private tumesikia hivii karibuni kuwa "They are tobig to fall" . Ilibidi "ujamaa" utumike kyaokoa hayo makampuni na mabenki.
Ubepari wanaokimbilia CCM wameruka hatua fulani .Sijui Hata CDM kama wana sera kuwa wakichukua nchi ndani ya Miaka mitano 40% ya zana za kilimo kwanza zitazalishwa nchin ina kiwnadacha UFI kilichofufuliwa na serikali.

Matokeo yake wanakuwa wepesi wa kuyauruga na kuuza mashirka nyeti kama RELI na TANESCO alafu wanakumbatia mashirika yasiyo na Tija kwa watanzania kama ATCL .

Uwe ni ujamaa au ubepari kwa hali tuliyonayo serikali ya chama kinachofaa Tanzania kile kiko tayari kuwa share hodler mkubwa tu wa mambo ya Nishati hasa umeme na kubinafsidha 100% anga na kuwa na stake ya atleast 70% kwenye RELI

Kifupi hivi sasa kuna tofauti ndogo sana(kisera ) kati ya CDM na CCM. Tofauti iiyop labada ni UFISADIambao ukweli unameza pesa kubwa sana na Hata CDM au CUF wakifanya yale yale MInus ufisadi japo si dawa kuna hatua zitapigwa kwa kasi
 
All ideologies have some uderlying philosophy..... but not vice versa!

Philosophy inaweza kuwa either "as a seeker of knowledge" au "as a proponent of ideas"

Inapokuja kwenye chama cha siasa, philosophy inachukua form ya "As a proponent of ideas".

Ndiyo maana kabla ya kuandika katiba ya chama cha siasa unaanza kwa kuelezea philosophy ya chama hicho... i.e how did you seek and obtain that idea. Ndiyo maana huanza na maneno haya... "Kwa kuwa...... Hivyo basi...."

Baada ya neno "Hivyo basi....... then unamwaga ideology (idea) ambayo ndiyo msimamo wa chama.

Ideology ya chama ndiyo ita-shape sera za chama (policies). Policy/sera means "course of action".

Sasa "Nguvu ya umma" as a philosophy inaendana vipi na "Mlengo wa kati" as an ideology?
Siyo haki kukiita chama ambacho ni centrist kuwa cha kijamaa. Na ideas za mtu mmoja mmoja haziundi chama unless ideas hizo zinafanana!


Sasa mada yangu basi siyo confusing kihivyo; Fikra (ideas) hutangulia itikadi (ideology) ambayo ndiyo huzaa sera... na sera huzaa sheria na miundo mbinu yake (system) ya kutekeleza sheria hizo na sera hizo. Falsafa is just a fancy way of saying "thinking" or "thought" a.k.a fikra. Na hapa tunazungumzia katika loose meaning of the word not in its technical connotation.
 
I don't worry whether the opposition parties have the same policies as the ruling party or not. This is because it takes time for ideological political parties to take shape in a country where 90% of electorates expect the same from their government. For instance, Tanzanians expect their government to offer free education, free health and other social services. So in this sort of environment to ask CHADEMA or any other political parties to take a distinct political orientation is a bit premature.

Furthermore, it's quite right for other parties to take the same political and philosophical stance as the ruling party. This is because the performance of the ruling party doesn't justify that they are what they claim to be. CCM is a leftist party, but the party has failed to deliver and uplift the lives of many Tanzanians. As such any political party that promises to perform better that the ruling party should be allowed to do so regardless of its political creed.

Political parties with different policies are very good for the country. However, before we get there we should be realistic. Political pluralism in Tanzania didn't start with the right foot. The constitution should have allowed independent candidates to seek political office, and I believe over time these individuals would have formed the building blocks for political pluralism through their alliances.

For example, independent members of parliaments who have formed groups based on geographical areas, philosophy and profession. The growth of these groups could be used to launch political parties with their own agenda.
 
Kama chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kitaendelea kujisogeza karibu na kubariki sera za chama tawala ndivyo hivyo hivyo CHADEMA itazidi kujiwekea mazingira ya kujiangamiza huko mbeleni. Na ndivyo hivyo hivyo tofauti kati yake na CCM itazidi kupotea na kwa upande wa sera kitaonekana hakina tofauti kubwa na matokeo yake badala ya kutofautishwa kisera watu wataanza kuangalia tofauti za watu tu.

Uhusiano kati ya Fikra, Sera, Itikadi na mfumo wa utawala


Watu wenye fikra zinazofanana huweza kukutana pamoja na kujadiliana na kujikuta kuwa wanakubaliana sana kuhusu mambo mbalimbali. Kwa mfano katika mazungumzo mtu anayeamini kuwa serikali inapaswa kutoa ruzuku kwenye shule za binafsi na mwingine naye anaamini kuwa shule na hata vyuo binafsi vinahitaji ruzuku ya kuviendesha hawa watakuwa wanafanana kifikra. Hawa basi wana fikra sawasawa.

Wakikaa pamoja na kukubaliana hata namna ya kutoa ruzuku hiyo au kujikuta wanakubaliana kwenye masuala ya maji, nishati, usalama, inteligensia n.k basi watu hawa wanaweza wakaamua kuanzisha chombo chao ili waweze kutekeleza fikra zao. Hivyo, itikadi huzaliwa. Itikadi basi ni mkusanyo wa fikra, mawazo na maono yanayotokana na kukubaliana fikra hizo ambayo huweka lengo la namna ya kutimiza fikra hizo kwa namna mbalimbali. Hivyo, kabla ya watu hawajakumbatia itikadi fulani ni lazima kwanza kabisa wajue kama itikadi hiyo inakubaliana na fikra zao.

Katika siasa na filosofia kuna itikadi mbalimbali ambazo zimesababisha makundi mbalimbali. Itikadi ya Kibepari kama vile ya Kijamaa ni mazao ya fikra za watu mbalimbali. Kwa upande wa Ubepari ni mazao ya watu kama kina Adam Smith na wenzake wa zama zake na miaka ya karibuni umekosolewa na kutengnezwa upya na wasomi wengine ambao wameondoka kidogo (au sana) kutoka katika fikra za kina Adam Smith. Ujamaa kwa upande wake ni mazao ya kina Lenin Mmm!NIMESHIBA,NAVUTA PUMZI,NITAREJEA BADAE
 
Kama chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kitaendelea kujisogeza karibu na kubariki sera za chama tawala ndivyo hivyo hivyo CHADEMA itazidi kujiwekea mazingira ya kujiangamiza huko mbeleni. Na ndivyo hivyo hivyo tofauti kati yake na CCM itazidi kupotea na kwa upande wa sera kitaonekana hakina tofauti kubwa na matokeo yake badala ya kutofautishwa kisera watu wataanza kuangalia tofauti za watu tu.

Duh.. sikutarajia wakati naandika hili ukaribu ambao niliuhofia ungekuwa ni hadi wa kubadilishana viongozi!
 
Umesahau chadema haina sera mkuu..

Isipokuwa ufisadi...ufisadi...ufisadi..(sijasikia zaid ya hilo tangu nianze kuwasikiliza 2005)

Wakati huo huo wakishindwa kuthibiti ufisadi ndani ya chama chenyewe, ukabila udini na upendeleo wa wazi, na ubadirifu wa mali za chama unaofanywa na wenye chama..lol
Siku hizi wameshaihama hii hoja
 
Hizo zilizoko kwenye tovuti nazifahamu nazipitia mara kwa mara za vyama vyote;

Lakini ulishawahi kuhudhuria mkutano wa hadhara wa chadema?

Mimi ni mhudhuriaji sijawahi kusikia wakiwaambia wananchi hizo sera zao ni ufisadi, ufisadi..no more..
 
Ndio lengo la kuwakumbusha na kukumbushana. Najua wanafanya hvyo mara nyingi tu wanazizungumzia sera zao lakini bahati mbaya wakati mwingine wanaonekana kama kujisikia vibaya kukosoa sera za CCM. Wapo ambao wanaamini sera za CCM zina uzuri fulani na hivyo zinahitaji kuboreshwa ili serikali itawale vizuri. Niliwahi kuandika huko nyuma siyo jukumu la upinzani kuishauri CCM ili itawale vizuri! Jukumu la upinzani ni kudhoofisha chama tawala ili kishindwa uchaguzi ili huo upinzani uingie madarakani kuja kutekeleza sera zake.
 
Umesahau chadema haina sera mkuu..

Isipokuwa ufisadi...ufisadi...ufisadi..(sijasikia zaid ya hilo tangu nianze kuwasikiliza 2005)

Wakati huo huo wakishindwa kuthibiti ufisadi ndani ya chama chenyewe, ukabila udini na upendeleo wa wazi, na ubadirifu wa mali za chama unaofanywa na wenye chama..lol
Zama zimebadilika.
Hivi sasa ukisema neno ufisadi ndani ya chadema utaitwa msaliti, gamba e.t.c.
Halipo tena...siku hizi ni ukuta...
 
Back
Top Bottom