Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
- Thread starter
- #41
Wildcard unanichanganya mimi na mwanasiasa. Sijawahi kuwa mwanasiasa hivyo haya ya kugombea nawaachia wanasiasa. Siombei nije kugombea.
Hata Dr Kitila Mkumbo simwoni kama ni mwanasiasa. Yumo mle ndani ya CHADEMA na anasaidia mengi kimyakimya. Naomba nawe uwe ndani ya chama kimojawapo ndani ya hivi vingi tulivyonavyo. Matokeo tutayaona tu.Wildcard unanichanganya mimi na mwanasiasa. Sijawahi kuwa mwanasiasa hivyo haya ya kugombea nawaachia wanasiasa. Siombei nije kugombea.
Bila ya SERA na UTENDAJI mbadala wa wazi kwa WATANZANIA "silence death" ya CCM ni ndoto.Wanajamvi! Nimepitia main topic na comments zote! Nashukuru sijaona wale jamaa zake na FF wanaosema kila wakati topic ndefu! Topic ndefu! Topic ndefu!......... Kimsingi nikupongeze Mwanakijiji kwa kutoa uchambuzi yakinifu na ushauri uliotukuka kwa CHADEMA! Mwanzo nilipoanza kuisoma topic yako nilianza kukasirika lakini kila ninapoendelea na aya basi utamu wa ushauri unaongezeka.................... Niseme CCM is in silence death!
Mwanakijiji,
Bila ya wewe kujitokeza na kuamua wazi kugombea katika mojawapo wa utitiri wa vyama tulivyonavyo mawazo mazito kama haya na mengine ambayo umekuwa ukitoa mara kwa mara mitandaoni na kwenye vyombo vingine vya habari yanabaki hivi yalivyo basi. Chukua mifano ya akina Zitto, Dr Slaa, Mh Mbowe, Mh Mnyika,... ambao wametafuta majukwaa ya wazi yanayowafikia wananchi moja kwa moja wanavyofikisha ujumbe kirahisi na wakati mwingine kwa kuazima maneno na fikra zako.
Jitokeze Mwanakijiji. Muda unakuacha kwa kasi ya ajabu na ninaamini nchi yetu inahitaji watu kama wewe sasa kuliko wakati mwingine wowote. Nayasema haya kutoka moyoni mwangu wala sio kujipendekeza kwako kwani sikufahamu nje ya mabandiko yako kwenye media mbalimbali.
Nje ya SIASA kwa nchi zetu hizi changa ni vigumu kuandika ukasomwa na wengi au kuzungumza wengi wakakusikia. Vinginevyo uwe kama Bill Gates ambako ni kugumu zaidi. Tunataka tuwe na chama MAKINI zaidi ya CCM. Hiki chama ni lazima kiundwe na watu MAKINI na safi kama Mwanakijiji, Jenerali na wengine wa aina hiyo.Hapa napo pana tatizo ambalo limetugharimu sana,kumekuwa na kasumba ya watu wenye fikra pevu ama hata utaalamu fulani kushawishika kuingia katika siasa, binafsi hii kwa kiasi kikubwa imetufanya tukose watu makini na muhimu ambao wangeplay role katika wide ground kwenye kutoa mawazo,ushauri utaalamu na hata utafiti,tumelundika hazina kubwa ya wataalamu bungeni ambao mwisho wa siku wanaishia kusema ndioo! hata kama jambo linalopitishwa ni la hovyo.
Watu kama MMM wanatakiwa kubaki neutral ili mawazo yao yapokelewe na pande zote. lakini akiwa katika platfom ya siasa kupitia chama fulani,mawazo yake siku zote yataonekana ni ya kichama chama.Sote tunakumbuka Jenerali Ulimwengu alivyokataa vyeo vya kisiasa,imemjengea heshima na confidence ya kusemea mambo ya kitaifa bila hofu ya maslahi ya Chama.
Kwa mtazamo wangu,kuna watu wameumbwa kuwa nuru katika jamii,ukiwawekea uzio ni sawa na kuzuia nuru hiyo isienee zaidi.
(sisemi moja kwa moja MMM asiingie katika siasa,la hasha huo ni utashi wake mwenyewe,mimi nimeshauri kama mkereketwa wa mawazo yake hapa jamvini na kwenye media nyingine).
Article ipo very confusing (almost a reflection of our political system).
It's the philosophy that creates an avenue for ideology.
Article ipo very confusing (almost a reflection of our political system).
It's the philosophy that creates an avenue for ideology.
Ideology shapes the policy . (Ideology is reflected in policies).
Philosophy = falsafa, hii huelezea kwanini kitu fulani kipo kama kilivyo, na njia mbali mbali za kuboresha hicho kitu (kimawazo). ni msingi wa knowledge.
Ideology ni doctrines mbalimbali ambazo kundi la watu fulani wanaona kama ndiyo zitawafikisha wanapotaka kwenda.
Policy ni sera.... jinsi ya kuincorporate ideolgy(ies) ili kuleta results (materially).
CDM lacks concrete ideology, chama chochote kinachosema kina mlengo wa kati ni lazima tukiogope ... huwezi kukiwajibisha kwa sababu centrism by itself is a lazy man's ideology. It's so irresponsible, .. knowing that "Socialism" is the preffered policy when it comes to the poor and powerless (which is the majority in Tanzania). But is the enemy of the rich and powerful (A group that most politicians either aspire to be or to please).
CDM's philosophy is bogus from the begining. People's power can only be achieved throgh socialism, period. Their shadow budgets are not socialistic at all, so that tells you what kind of a party CDM is ...... A mere political party. They are just there to have something to do.
Policies?...... well, that's self explanatory.
Mlengo wa kati ni nini?Fanya home work yako vizuri utagundua kuwa ''Mlengo wa kati'' ndio nchi nyingi zimeamua kufuata hasa zinazoendelea. Nchi kama China inajulikana ni nchi ya kisoshalisti lakini inafuata sera za kati, hali kama hii pia utaiona Russia na nchi nyingine ambazo hapo mwanzo zilikuwa za kisoshalisti.
Katika nchi maskini kama zetu ukikumbatia ubepari moja kwa moja wakati watu ndo kwanza wameingizwa ghafla kwenye bahari wasiyo jua kina chake ni lazima wengi nchi ididimie. Katika hali kama hii ndipo wachache wenye madaraka hujilimbikizia mali kama ilivyo sasa hapa kwetu na pia kama ilivyotokea huko Russia baada ya kuanguka kwa USSR.
Baada ya kupambana na kufanikiwa kudhibiti ''walafi'' sasa mambo yao yanazidi kuboreka ingawa bado wanayo safari ndefu lakini angalau wanayo matumaini sio kama sisi.
Nchi kama China inafanikiwa pia kwa njia hiyo hiyo kukuza uzalishaji lakini bila kuwasahau maskini na pia kupambana na ''walafi'' kwa nguvu zote.
Mlengo wa kati kwa sasa ndio njia, nawapongeza wote wenye mtazamo huo
Philosophy ni nini basi na inahusiana vipi na "fikra" (ideas) za tu mmoja mmoja?