Ziara ya Makonda mikoani inamjenga sana yeye kuliko Chama

Bromensa

Member
Jan 3, 2024
22
21
Habari,

Nimeona Ziara ya Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Paul Makonda mikoani ni kama inamjenga sana yeye kuliko chama na huenda ikamfanya kuwa na ushawishi mkubwa sana ndani ya CCM na nje ya CCM.
Mara nyingi amekuwa akitumia jukwaa kujielezea yeye zaidi kuliko chama.

Nilitegemea kwenye ziara hii angejikita zaidi katika kutoa mwelekeo wa kisiasa kwa wanachama na umma. Hii ni pamoja na kuelezea sera za chama, kutoa mwelekeo wa maendeleo ya kisiasa, na kueleza msimamo wa chama katika masuala mbalimbali.

Vilevile angetumia fursa hii kusikiliza moja kwa moja mahitaji, maoni, na matarajio ya wanachama wa chama. Hii inaweza kusaidia kuunda sera na mikakati inayojibu mahitaji halisi ya wanachama na jamii kwa ujumla.

Take it or leave it
 
Acha chuki zako na hofu zako kwa Mheshimiwa Makonda.usitake kumkatisha tamaa na kuleta uzushi wako hapa.hayo uliyoyaandika kuwa unataka afanye ni kuwa Mheshimiwa Makonda amefanya zaidi ya hayo unayoyataka wewe.

Mheshimiwa Makonda anasikiliza kero za wananchi,anatoa suluhisho kwa kuwahoji watendaji wa serikali na wahusika wote,anaelezea kwa undani sera za chama, utekelezaji wa ilani, mambo ambayo serikali imefanya na inatarajia kufanya,msimamo wa chama katika mambo mbalimbali na mengine mengi sanaaa .

Sasa wewe unataka afanyeje? Hata hivyo ningependa kukwambia kuwa jina la Mheshimiwa Makonda ni kubwa sana katika Taifa letu.hata kabla ya uteuzi huo Mheshimiwa Makonda alikuwa ni mkubwa sana na mwenye jina kubwa sana kitumishi ,kuichapa kazi ,kiuzalendo, kijasiri,kiupeo,kiubunifu n.k.

Ndio maana uteuzi wake katika nafasi aliyopo kwa sasa ilipokelewa kwa shangwe, nderemo na vifijo vikubwa sana mitaani.ndio maana aliteka habari zote hapa nchini na ndio maana Anaendelea Kuitetemesha nchi kila siku huku macho na masikio ya watanzania yakiwa katika ziara zake.
 
Anaitumia fursa vizuri. Ana malengo yake pia binafsi tofauti na ya taasisi. Kwahiyo anajijenga kote kote. Angeweza ku balance ingekuwa heri ila hizi mimi mimi sijui mimi ningekuwa mwenezi kipindi cha fulani hazimsaidii. Yeye ni Mwenezi chini ya Mwenyekiti Mh. Samia na aende kwa style ya uongozi ya Mwenyekiti wetu sasa.
 
Ziara zote zinabidi ziwe kusikiliza wananchi, kutatua changamoto zao, kuwawajibisha watendaji, kujenga taifa zaidi ya mtu, kikundi, chama.
 
Sawa
 
Ziara zote zinabidi ziwe kusikiliza wananchi, kutatua changamoto zao, kuwawajibisha watendaji, kujenga taifa zaidi ya mtu, kikundi, chama.

..wananchi wana changamoto nyingi mno.

..mikutano ya Makonda haichukui zaidi ya masaa mawili kwa wilaya moja.

..huo sio muda wa kutosha kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyapatia ufumbuzi.

..wananchi wanakuwa na hamasa kuhusu ujio wa Makonda ktk maeneo yao lakini nina hakika baada ya muda mfupi watagundua wako palepale na matatizo yaleyale kama alivyowakuta Makonda.
 
Habari,

Nimeona Ziara ya Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa Paul Makonda mikoani ni kama inamjenga sana yeye kuliko chama na huenda ikamfanya kuwa na ushawishi mkubwa sana ndani ya CCM na nje ya CCM.
Mara nyingi amekuwa akitumia jukwaa kujielezea yeye zaidi kuliko chama.

Nilitegemea kwenye ziara hii angejikita zaidi katika kutoa mwelekeo wa kisiasa kwa wanachama na umma. Hii ni pamoja na kuelezea sera za chama, kutoa mwelekeo wa maendeleo ya kisiasa, na kueleza msimamo wa chama katika masuala mbalimbali.

Vilevile angetumia fursa hii kusikiliza moja kwa moja mahitaji, maoni, na matarajio ya wanachama wa chama. Hii inaweza kusaidia kuunda sera na mikakati inayojibu mahitaji halisi ya wanachama na jamii kwa ujumla.

Take it or leave it
Na anajijenga hasa. CCM wampatie uenyekiti kabisa
 
Saiv Makonda ndo mwenye CCM tangu kiongozi wa juu Hadi wa chini wanamwangalia yeye! Jambo ambalo SI zuri sana kwenye Chama Cha siasa.
Pia Makonda inatakiwa awe makini sana na kauri zake kunawakati anaongea vitu vitakuja kumgalimu kama kauli yake wakati akiwa Moshi anatumia muda mwingi kuattach personality ya wapinzani kuliko sera za Chama chake.
Makonda anajijenga sana, baadaye anaweza kuwa mtu mkubwa sana ndani ya Chama jambo ambalo litakuja kiwaletea shida sana CCM.Utafika muda atakuwa haambiliki,haguswi, yupo juu ya kila mtu.Nawaza TU kwa sauti saiv Nappe Nnauye anajiskiaje au anawaza Nini Makonda kuwa na upepo alionao?!
 
Chuki zako na hofu zako.........nimecheka sana ......sijaona sehemu ameonyesha chuki wala hofu.....yeye katoa mtazamoa wake tu......ilibidi na wewe ujenge hoja....:D :D:D
Nilitaka kuandika nikakuta Ukimgusa makonda kwa namna tofauti na kumsifia na kumkweza Lucas anamwaga adrenaline kama ndugu wa mume. So sad
 
Nilitaka kuandika nikakuta Ukimgusa makonda kwa namna tofauti na kumsifia na kumkweza Lucas anamwaga adrenaline kama ndugu wa mume. So sad
Jamaa anasifia mpaka anapitiliza....ndio maana anaweka namba ya simu kabisa...anasubiri uteuzi. :D :D :D
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom