Anayejua namna ya kutengeneza bagia za kunde

Mahitaji
Kunde zisizo na maganda nusu kilo
Vitunguu maji 3
Vitunguu saumu 2
Chumvi
Mafuta
Pilipili 1

Maelekezo
Weka maji kwenye sufuria, beseni au chombo chochote.
Weka kunde kwenye hayo maji uziloweke, mimi huwa napendelea kuziloweka usiku mzima ili zilainike vizuri.
Andaa viungo, kata vitunguu maji vipande vidogo sana, vitunguu saumu menya weka kwenye chombo na pilipili ikatekate.
Chukua blenda, toa kunde kwenye maji, ziweke kwenye blenda.
Weka vitunguu maji, vitunguu saumu, pilipili na chumvi humo ulipoweka kunde
Ongeza maji kidogo sana,upate urahisi wa kusaga. Hakikisha unaposaga kunde zimelainika na viungo ulivyoweka vimesagika vizuri.
Hakikisha pia mchanganyiko hauwi mwepesi, bandika sufuri jikoni, weka mafuta yakipata moto, chukua kijiko chota ule mchanganyiko, weka kwenye mafuta.
Usigeuze mpaka uone chini imeiva vizuri geuza upande wa pilipili, ukiona imeiva epua, chuja mafuta hapo ni tayari kuliwa.
mkuu umeshapika nije kuonja?
 
kwa hiyo huweki hamira
 
Mimi pia ni mpenzi wa hizo bagia ila kwa kuzitengeneza mwenyewe si kwa kuzinunua mtaani au kula hotel coz maandaliz yake sijui wanafanyaje zinakuwaga na mchanga sana.Karibu!!!!
Bajia Za Kunde

Bajia%20Za%20Kunde.jpg

VIPIMO

Kunde za kupaaza 1 ½ Vikombe (hizi kunde kwetu tunaziita (njoombo)

Vitungu vya kijani iliyokatwa katwa ½ Kikombe

Baking soda ¼ Kijiko cha chai

*Bizari mchanganyiko 1 Kijiko cha chai

Maziwa 2 Vijiko vya supu

Chumvi 1 ¼ Vijiko vya chai

Unga wa ngano 2 Vijiko vya supu

Mafuta ya kukaangia

* Unaweza kutumia bizari ya pilau (cummin) ukipenda

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA

  1. Osha na kuroweka kunde kwenye bakuli la maji ya baridi usiku mpaka asubuhi.
  2. Saga kwenye mashine (food processor) kisha mimina kwenye bakuli.
  3. Ongeza vitungu, baking soda, masala, maziwa, na chumvi.
  4. Koroga vizuri halafu tia unga kisha uchanganye pamoja.
  5. Fanya vidonge kama nchi moja kisha ukipenda bana katikati ya mikono na kidole katikati ya bajia.
  6. Kaanga kwenye mafuta ya moto mpaka ziive.
  7. Andaa bajia kwenye sahani na chatini uipendayo.
Kwa hapo unaweza kuserve kwa chai, maziwa,juice au chochote unachopenda wewe!!
Asante nilikuwa natafuta hii recipe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom