Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,264
KUMBUKUMBU YA MFUNGO WA RAMADHANI 3: FUTARI YA ALLY SYKES NA NA SINIA LA KUNDE ZA BIBI TITI
Binti yangu kaanda meza katuwekea futari.
Tumetoka msikitini tukakaa mezani tunafuturu.
Kipindi kimepita ghafla mwandaaji katutokea anakagua meza.
"Mbona hii mihogo haijaguswa?"
Mwandazi anauliza.
Kimya.
Kasimama jicho linapitia sahani moja moja.
Kimya.
Sasa sioni dalili ya mwanangu kuondoka nasi tuendelee na mikono yetu iendelee kule moyo unakopenda iende.
Kimya.
Mimi nikajibu, "Tumetembelea kote."
Mwanangu hakujibu akanyanyua sahani moja kuelekea jikoni.
Ukweli ni kuwa tumechota muhogo lakini kiduchu sana kiasi unaonekana kama vile haukuguswa.
Hili hakupenda.
Walaji tumefanya khiyana.
Mpishi hakupenda.
Huu muhogo toka jana Chungu Mosi tulitengewa lakini tukadonyoa.
Leo tumewekewa tumedonyoa.
Binti yangu kaghadhibika kidogo bila ya kuonyesha hamaki.
Lakini ujumbe umetufikia walaji sawia.
Nikakumbuka futari ya Ally Sykes na sinia la kunde la Bibi Titi Mohamed.
Bwana Ally katualika futari kwenye nyumba yake Ursino Estate.
Katambua akitualika futari nyumbani kwake Mbezi Beach atatutaabisha.
Yapata saa miaka 40 imefika.
Miaka hiyo Mbezi Beach kulikuwa mbali sana hakuna usafiri wa umma unaofika huko.
Baraza imejaa watu wa Gerezani rafiki zake Bwana Ally toka utoto wao.
Halikadhalika watu wakubwa wapo wanajichanganya na wananchi wapiga kura.
Enzi hizo chama kimoja siasa ni Ujamaa Vijijini na Kujitegemea.
Tuko kwenye shughuli ya Ally Sykes anafuturisha.
Kamata kitu kimoja kutoka kwangu.
Hapa ni Who is Who.
Nani ni nani Dar-es-Salaam.
Jua limetua.
Pameadhiniwa tumefungua kwa kahawa, tende juisi baridi na maji baridi.
Pamekimiwa.
Tumesali.
Sahani zimetandazwa kote mazuliani.
Kila mtu na sahani yake na mbele yake vyombo vilivyojaa vyakula kuanzia kuku, samaki, hadi sambusa, katlesi, chapati maamri, njegere, mbaazi...
Waswahili tuna msemo hukuweko malaika wako alikuwako.
Tumeziinamia sahani tunazungumzanazo.
Mungu atupe nini sisi waja wake.
Mfungo unakaribia kukatika futari yetu makwetu ni muhogo, kunde na maharage.
Enzi hizo tunapanga foleni kupata kilo ya unga wa njano.
Leo Bwana Ally anatumwagia kuku, mchone, sambusa, katlesi...
Sisi wana wa nchi hatuzungumzi na mtu tunazungumza na changu na nguru.
Ghafla Bwana Ally kasimama na sinia kubwa kainyanyua juu anatunadia, "Jamani Bibi Titi katuletea kunde, kunde za Bibi Titi."
Bwana Ally anapita ananadi, "Kunde za Bibi Titi, kunde za Bibi Titi."
Anapita anawapakulia watu kwenye sahani zao.
Ikawa sasa anaitwa kila mahali watu wanataka kula kunde za Bibi Titi.
Mimi nimekaa na Juma Mwapachu tumeelekezana.
Kaka Juma ananiuliza, "Mohamed vipi niite kunde za Bibi Titi?"
"Kaka Juma kunde za Bibi Titi zitaniwia radhi.
Mimi hapa mkono kwenye chapati mkono kwenye kuku samaki."
Juma Mwapachu akaangua kicheko.
"Kaka Juma kunde hiyo ndiyo futari yangu kila siku itaniwia radhi leo naipumzisha."
Allah warehemu wazee wetu hawa kwa baraka za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani."