Anatamani turudiane, lakini hataki kukiri wala kuongelea kosa alilofanya..NIMFANYEJE?

Mbarikiwe wote Wana JF! Leo nakuja kwenu kuomba ushauri, natumaini kwa kutumia uzoefu,ujuzi na Upendo mtanipa suruhisho! Nimienzi kama mitatu hivi tulitofautiana na msichana niliyetegemea angekuja kuwa mama wa watoto wangu siku za usoni! Tulidumu takribani miaka mitano kwani tulianza mahusiano tukiwa bado A'level! Kisa cha kutofautiana,mara nyingi nilifuma chatings za mahaba na mwanaume mwingine! Lakin pamoja na hayo hakuacha kuniheshimu! Kilichoniumiza mpaka tukanuniana ni siku moja kabla ya kuachana nilimuomba tutoke out akakubali,lakini cha ajabu mda ulipofika hakupokea simu zangu wala kujibu sms zangu mpaka ilipofika jioni akaniambia alikuwa na mama yake...lakini baada ya kufanya uchunguzi jioni hiyo hiyo(kwani baadae tulionana) niligumdua alitoka na huyo jamaa yake. Hii ni kutokana na sms za siku hiyo tangu wanapanga pa kukutania na msg aliyomshukuru kwa "campani"ya siku hiyo!! Nilipomuuliza hizo sms ni za nani na kwanini aliamua kunidanganya,hakuwa na usemi zaidi ya kutetemeka(nilichukua simu yake ghafla). Mpaka leo anasema nilimsingizia na hataki tuliongelee hilo ila ananilaum tu kuwa nimemuacha kwa sababu nimepata mwingine! Bado nampenda na anaonyesha nia ya kuwa na mimi, ila nahofia atakosa uaminifu ndani ya ndoa! MSAADA WENU PLZ..!

Ndugu usimrudie huyo Binti kwa Lengo la kumsaidia Elewa kuwa uchumba sio Ndoa usijejuta hapo baadaye kama ameonyesha kutokuwa mwamifu na hana moyo wa toba nakushauri mwache
 
Kama unampenda bado mrudie, halafu mambo ya kuangalia simu yake ACHA. Amini tu anachokwambia la sivyo hutaweza kuishi na msichana yeyote wa sasa. Hata wewe akiangalia simu yako kila siku hamtakaa pamoja.
Ndio maisha ya sasa ndugu yangu.
 
NI KWELI UNAMPENDA NDO MAANA PAMOJA NA KUMLAUMU, BADO UNAMSIFIA ETI "HAKUACHA KUKUHESHIMU", ETI "ANAONESHA NIA YA KURUDIANA NAMI".UNASAHAU KWAMBA HAKUHESHIMU NDO MAANA HAKUTOKEA KTK MTOKO WA SIKU ILE, HAACHI KUCHATI NA HUYO ALIYEINGILIA MAHUSIANO YENU LICHA YA KUONA NAMNA UNAVYOKERWA NA MASEJI HIZO ZA MAHABA KTK SIMU YAKE NA KULE KUTOKUWA TAYARI KULIONGELEA KOSA LAKE.HUO WOTE NI USHAIDI WA MOJA KWA MOJA KWAMBA HUYO DEMU ANAKUDHARAU SANA.SUALA LA KUONESHA NIA YA KURUDIANA NALO LINAKUANIAKA KWAMBA HUJIEKLEWI.HEBU JIULIZE AMEONESHA NIA YA KURUDIANA KWANI NANI ALIMWACHA MWENZAKE KATI YAKO NAYE.KUMBE ULIPOMWACHA HUKUMAANISHA, SIYO!.KAMA ULIKUWA UNAMWOMBA MUNGU AKUPE MKE MWEMA BASI KAKUSAIDIA KWAMBA HUYO SI MWEMA.NA YEYE KUTOKUWA TAYARI KUJADIRI KOSA LAKE NA KUOMBA RADHI, NI WAZI SANA KWaMABA YUKO TAYARI KWA UAMUZI UTAKAOCHUKUA.

tafakari.................
 
Anaogopa kuzungumzia kwasababu anajua ni kweli na anaona vibaya kukiri kuwa alifanya hayo.. Kwa uzoefu wangu, huyo binti anaona unampenda na uko kwa ajili yake kila mara so kakugeuza tulizo lake pale anapoumia. Mkirudiana na akapata mshefa mwingine atakukimbia tena.

Haya nilokwambia changanya na yako upate uamuzi. Maneno yangu si sheria

Hakufai huyo kaka utakuja juta chapa mwendo fasta.maneno haya pia sio sheria
 
ushathibitisha so unahitaji nn sasa
mi kwa jibu rahs tu naona upo tayari kushea.
big up kwa mdada aendelee kukudanganya hivohivo

Hapo umenena mwanawane. watu wengine ni kama akili zao zinahama kwenye masuala ya mapenzi. After all inakuwaje for 5 years mnakandamizana kizenji tu bila kuoana, why? Hilo pia linaweza kuwa moja ya sababu ya yeye kukuona huna committment naye.

Wewe fahamu kwamba hata iweje huyo hataweza kuwa wako peke yako, utaendelea kuchukuliwa mpaka utie akili, kudadadeki wewe!
 
mbona mtu mwenyewe kama vile mimi ndo nilikuwa nae siku iyo vile! kiufupi achana nae, atakuumiza zaidi ya hapo. leo anarudi kwa msamaha, lakini baadae atasahau na hapo ndo utalia na kusaga meno
 
Back
Top Bottom