Anatamani turudiane, lakini hataki kukiri wala kuongelea kosa alilofanya..NIMFANYEJE?

Pole ..msamehe ila usikimbilie ndoa haraka jipi na mpe muda wa kua-nalize kwanza ili uje kufurahia ndoa badae ila ni vizuri angekueleza yaliyomsibu kuchanganya ujue kama anajutia au ni hobby yake..wakati mwingine Mungu anakuonyesha huyu siye mwanangu na ww unang'ang'ania ..ni mawazo yangu
 
Anaogopa kuzungumzia kwasababu anajua ni kweli na anaona vibaya kukiri kuwa alifanya hayo.. Kwa uzoefu wangu, huyo binti anaona unampenda na uko kwa ajili yake kila mara so kakugeuza tulizo lake pale anapoumia. Mkirudiana na akapata mshefa mwingine atakukimbia tena.

Haya nilokwambia changanya na yako upate uamuzi. Maneno yangu si sheria

Aksante kwa ushauri wako! Ngoja niendelee kuchekecha na ya Wadau wengine!
 
silence means yes,tokea hapo ushajua ukweli,hata akikiri haitabadili kitu,fata moyo wako unavyokwambia
 
Mwambie abadilishe line halafu uchunguze kwanza kama anaendelea kuchati na vinjemba vyake.
 
Pole ..msamehe ila usikimbilie ndoa haraka jipi na mpe muda wa kua-nalize kwanza ili uje kufurahia ndoa badae ila ni vizuri angekueleza yaliyomsibu kuchanganya ujue kama anajutia au ni hobby yake..wakati mwingine Mungu anakuonyesha huyu siye mwanangu na ww unang'ang'ania ..ni mawazo yangu

nashukuru kwa mawazo yako! Ila wakati mwingine nahisi umbali ulichangia, kwani mda mwingi nilikuwa chuoni mkoa mwingine yeye alikuwa na mishemishe mingine nyumbani! Nazidi kumuomba MUNGU anitie nguvu ktk hili,nilimuamini sana!
 
Inavyoonekana una wivu bro! nashauri kwa kuwa ushatia wasiwasi na huyo girlfriend wako basi tafuta mwingine maana utateseka maisha yako yote
iwapo utafunga ndoa na kila utakapokuwa unafikiria hilo jambo.Bro usisikie bwana kumegewa unaweza kuua mtu bora achana nae kabisaaaaaaaaaaaa.
 
"...WIVU UNAHUSIKA PENYE MAPENZI YA KWELI..."by the way thanks for your advise!
 
Kuna wimbo flan hvi umeimbwa na banana zoro unaitwa 'ZOBA' naupendaga.
 
Mkuu pole kwa yaliyokukuta,lakini napenda nikupe angalizo hapa katika maamuzi yako,mchumba ukishakuwa na mashaka nae kabla ya ndoa hautokuja enjoy hayo maisha yako ya ndoa,labda kama una uwezo wa kusamehe na kusahau bila kuwepo na nguvu nyingine yoyote toka nje na wewe itakayokushawishi kusamehe,vinginevyo utakuwa unajitafutia stress na ulcers mbele ya safari.....Uliloamua ndilo la msingi zaidi ni bora uliheshimu mwachie apate nafasi ya kuwa na mtu anayemsisimua,anaonyesha wazi umemuacha ukiwa unampenda kaza moyo songa mbele utakuja juta wakati umeshachelewa.NI USHAURI TU KIONGOZI.
 
Mapenzi hayana formula hakuna anayeweza kukushauri njia sahii ya kuenenda na mpenzi wako kama vile ambavyo wakati mnaazana hakuna aliyekuambia mwambie neno hili au lile ndio atakusikiliza au kukubali. Kuleta mada kwenye jamvi ili ijadiliwe ni kama ada lakini mwisho wa siku uamuzi sahii wa nini kifanyike unabaki nao wewe.

Kama ukitoa nafasi ya kila mtu kueleza yake yalokwisha msibu mapenzini utashangaa kuona kwanini hii kitu mapenzi na mahusiano bado kipo duniani! kwani hakuna anayewezasema kuwa ameogelea bahari ya mahusiano hadi ufukweni bila kukumbana na misukosuko.
 
Nashukuru sana kwa maoni yenu kwa ujumla! Mpaka sasa nimepata kitu tena kikubwa! Naamini maoni yenu yatanisaidia kufanya maamuzi mazuri! Nasema tena thanks a lot!
 
Nashukuru sana kwa maoni yenu kwa ujumla! Mpaka sasa nimepata kitu tena kikubwa! Naamini maoni yenu yatanisaidia kufanya maamuzi mazuri! Nasema tena thanks a lot!
 
yaani kama ningekuwa mimi kwa hali niliyonayo sasa na nikigundua hivyo kwa kweli namuacha maana anaonekana hawezi kubadilika, angekuwa mtu wa kubadilika ungemkamata mara moja ama mbili tena na watu tofauti na angeacha, lakini mtu yule yule na umemkamata mara kadhaa, hawezi kuacha na akiingia ndani ndio utaona dunia chungu maana kutoka kwenye ndoa inakuja kuwa ngumu zaidi. kwanza angejutia aliyoyafanya na kama hataki kukiri basi hana nia ya kuacha huyo. lakini mwisho wa siku hii ni akili ya kuambiwa tu sasa jaribu kuwa mbayuwayu
 
Nashukuru sana kwa maoni yenu kwa ujumla! Mpaka sasa nimepata kitu tena kikubwa! Naamini maoni yenu yatanisaidia kufanya maamuzi mazuri! Nasema tena thanks a lot!
 
Back
Top Bottom