Anatamani turudiane, lakini hataki kukiri wala kuongelea kosa alilofanya..NIMFANYEJE?

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Mbarikiwe wote Wana JF! Leo nakuja kwenu kuomba ushauri, natumaini kwa kutumia uzoefu,ujuzi na Upendo mtanipa suruhisho! Nimienzi kama mitatu hivi tulitofautiana na msichana niliyetegemea angekuja kuwa mama wa watoto wangu siku za usoni! Tulidumu takribani miaka mitano kwani tulianza mahusiano tukiwa bado A'level! Kisa cha kutofautiana,mara nyingi nilifuma chatings za mahaba na mwanaume mwingine! Lakin pamoja na hayo hakuacha kuniheshimu! Kilichoniumiza mpaka tukanuniana ni siku moja kabla ya kuachana nilimuomba tutoke out akakubali,lakini cha ajabu mda ulipofika hakupokea simu zangu wala kujibu sms zangu mpaka ilipofika jioni akaniambia alikuwa na mama yake...lakini baada ya kufanya uchunguzi jioni hiyo hiyo(kwani baadae tulionana) niligumdua alitoka na huyo jamaa yake. Hii ni kutokana na sms za siku hiyo tangu wanapanga pa kukutania na msg aliyomshukuru kwa "campani"ya siku hiyo!! Nilipomuuliza hizo sms ni za nani na kwanini aliamua kunidanganya,hakuwa na usemi zaidi ya kutetemeka(nilichukua simu yake ghafla). Mpaka leo anasema nilimsingizia na hataki tuliongelee hilo ila ananilaum tu kuwa nimemuacha kwa sababu nimepata mwingine! Bado nampenda na anaonyesha nia ya kuwa na mimi, ila nahofia atakosa uaminifu ndani ya ndoa! MSAADA WENU PLZ..!
 
Kweli mapenzi ni upofu...afanye nini ujue hataacha kukuchanganya na wenzio? wake up
 
umekuwa naye kwa miaka mitano halafu kwa miezi mitatu zinatokea mizengwe!
Jichunguze isije kuwa na wewe una mapungufu, labda kuna kitu kakosa kwako
Je, mapenzi yenu yapo kama mlivyo anza zamani?

Mwanamke kutongozwa kupo hata kama umemweka ndani, ila chakuangalia ni reaction yake
Mrudiane tu!
 
Kama unampenda mwite kaa naye muulize sbb zipi zilimfanya yy kukusaliti na kutoka na mwanamume mwingine,huwezi jua lbd kn usichomridhisha, na akueleze msimamo/ malengo yk juu ya mapenzi yn
 
Uchumba wa muda mrefu kama huo (miaka 5) sio mzuri, humsisimui tena - amekuzoea, ndio maana anakuoana wa kawaida na kuanza kutafuta mwingine anayemsisimua. Kama unampenda mrudie, maana hata kama utamwacha na kumtafuta mwingine mambo yatakuwa hivyo hivyo. Ni afadhali uendelee na huyo uliyemzoea.
 
Uchumba wa muda mrefu kama huo (miaka 5) sio mzuri, humsisimui tena - amekuzoea, ndio maana anakuoana wa kawaida na kuanza kutafuta mwingine anayemsisimua. Kama unampenda mrudie, maana hata kama utamwacha na kumtafuta mwingine mambo yatakuwa hivyo hivyo. Ni afadhali uendelee na huyo uliyemzoea.
kinadharia watapinga lakn kiuhalisia ndio ukweli mkuu
 
ushathibitisha so unahitaji nn sasa
mi kwa jibu rahs tu naona upo tayari kushea.
big up kwa mdada aendelee kukudanganya hivohivo
 
ushathibitisha so unahitaji nn sasa
mi kwa jibu rahs tu naona upo tayari kushea.
big up kwa mdada aendelee kukudanganya hivohivo
nafikiri ni katika kutimiza ile nadaharia yenu ya kutest kama jamaa yupi anaweza,......
 
Anaogopa kuzungumzia kwasababu anajua ni kweli na anaona vibaya kukiri kuwa alifanya hayo.. Kwa uzoefu wangu, huyo binti anaona unampenda na uko kwa ajili yake kila mara so kakugeuza tulizo lake pale anapoumia. Mkirudiana na akapata mshefa mwingine atakukimbia tena.

Haya nilokwambia changanya na yako upate uamuzi. Maneno yangu si sheria
 
yaelekea bado mnapendana, rudianeni tu kwani hakuna alie msafi hasa ktk mahusiano, kosa moja haliachi mke
 
Kama unampenda mrudie tu,ni bora kichaa uliyemzoea,hujui utakayempata atakuwa na ukichaa wa aina gani,sie wanawake hatuishi vituko japo vinazidiana!
 
yaelekea bado mnapendana, rudianeni tu kwani hakuna alie msafi hasa ktk mahusiano, kosa moja haliachi mke

MAKOSA MANGAPI NDO YANAACHA?????tutakufa sana na hili gonjwa kwa mitazamo hii
Kaka hapo hupendwi unazugwa tu so shituka mapema
 
Back
Top Bottom