Anataka kuwa mke bora baada ya kunidharau

Mkuu embu tumia muda wako vizuri kuchakata mbususu lukuki zilizotapakaa kila kona acha kupoteza mda na na wazee mlioachana miaka 10 iliyopita.

Watu tunashangaa mbona mbususu zinatuzidi kumbe wengine mnategea.
Kuna za kuchakata na za kuoa mkuu
 
Dah hapo nilikwama,
Anzeni upya, kuna wanandoa niliwahi waona wao waliahidiana kuoana wakiwa shule, lakini haikuwa hivyo walipokuja kukutana kila mtu ana mwenza wake, huwezi amini kila mtu alimwacha mwenzie na wao wakaoana na wapo vizuri mpaka sasa.
 
Anzeni upya, kuna wanandoa niliwahi waona wao waliahidiana kuoana wakiwa shule, lakini haikuwa hivyo walipokuja kukutana kila mtu ana mwenza wake, huwezi amini kila mtu alimwacha mwenzie na wao wakaoana na wapo vizuri mpaka sasa.
Ana mtoto
 
Tulidumu karibu miaka 10, nia yangu ilikiwa ni kumuoa ila baada ya kukamilisha mipango niliyojiwekea, ilipobaki miezi michache tuoane akanikalisha chini akaniambia kuwa hawezi kuendelea kuwa na mimi.

Ikabidi niheshimu mawazo yake japo roho iliniuma mpaka kufikia hatua nikawa napata maumivu kwenye moyo.

Nakumbuka kuna siku nilikuwa namfuatilia kwenye facebook nikitamani kujua aliyenipiku ananini kunizidi, nikakuta kamposti jamaa fulani mfupi kapiga picha mbele ya rav 4, roho iliniuma sana na ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kukosa usingizi mpaka asubuhi, na kiherehere cha kumfuatia kikaishia palepale.

Baada ya kupita miaka mitano, Mwaka jana siku moja napeleka mzigo wa mteja mara simu ikaita kuchek namba ya airtel, kupokea anasema mimi I, nikamuambia mimi siongeagi na wake za watu akasema hajaolewa.

Akasema amenimiss anatamani kuniona tukapanga tukakutana, nilikuwa na hamu ya kuona maisha anayoishi,
Tukaenda anapoishi ni chumba kimoja kidogo kina kitanda tu na jiko la mkaa, amepauka amekonda. Akawa anampa mtoto kipande cha tikiti maji.

Hana kazi anategemea elfu 50 ya malezi ya mtoto anayopata kila mwezi kutoka kwa baba wa mtoto. Yenyewe aliipata kwa mbinde kupitia ustawi wa jamii.

Akanielezea kuwa yule mwanaume alikuwa ameoa ana watoto wa 3 na amezalisha wanawake kibao.

Akaniomba numpe nafasi awe mke bora mi nikawa namcheki tu alivyopauka.

Hivi kweli nipambanie maisha mpaka hapa nilipo alafu nioe mwanamke mwenye mtoto tena aliyenidhau.

Hakikisheni mkiacha mtu mnaenda kwa aliye bora zaidi. Ni hesabu rahisi tu.
we ndio umemuharibia mwenzako maisha, unadate na mtu miaka 10 ulitegemea nini
 
Back
Top Bottom