Anahitajika mfanyakazi wa kuuza duka la vifaa vya TEHAMA Arusha Mjini

siz

Senior Member
Jan 26, 2015
135
25
Nafasi ya kazi kuuza duka la vifaa vya TEHAMA:

Kituo cha kazi:
Arusha mjini

Mwisho wa kupokea maombi: 14 May 2021

Taarifa kuhusu kazi:
Anahitajika mfanyakazi wa kuuza duka la vifaa vya TEHAMA (Computer networking accessories).

Kazi za kufanya:
• Kuuza vifaa vya data kwa wateja watakaofika dukani,
• Kutunza nyaraka na kumbukumbu za mauzo na manunuzi yote ya duka,
• Kutoa ushauri wa kitaalam ambao utawashawishi wateja ili kuongeza mapato ya taasisi.
• Kutoa huduma ya kiufundi kwa wateja.
• Kutanua wigo wa biashara kwa kutangaza bidhaa kwenye mitandao ya kijamii.

Kufanya kazi nyingine zitakazojitokeza au kupangiwa muda wowote.

Sifa:
Waombaji wawe ni watanzania wakazi wa Arusha wenye umri kuanzia miaka 23 mpaka 35 wenye kiwango cha elimu kuanzia astashahada ya uhadisi wa kompyuta ,sayansi ya kompyuta, teknolojia ya mawasiliano, na mawasiliano ya simu.

Uzoefu
Mwombaji awe na uzeofu wa vifaa vinavyotumika katika TEHAMA (computer networking accessories) kiasi kwamba aweze kutoa ushauri kwa wateja na msaada wa kifundi.

Mawasiliano

Barua pepe:najat025@gmail.com

Simu ya mkononi:0763497413

Tahadhari: usitoe fedha kwa mtu yeyote kupata nafasi hii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom