Anaejua grade za kahawa na masoko yake, aje hapa tuongee

Ogo

Senior Member
Aug 26, 2013
132
43
Habari za mishughuliko wana JF, hivi unajua wapi wananunua kahawa? Na mbinu gani huwa wanatumia kupanga viwango vyake. Kuna sehemu niliambiwa iko kwa wingi ila kwavile sikuwa na idea yoyote kuhusu ili zao sikuhitaji hata kujua aina gani inayopatikana maeneo hayo.
Je wew unaweza kunipa uzoefu wako kama utafaa nitaanza kuifikira biashara hii.
Karibuni waheshimiwa.
 
Biashara ya Kahawa si kama biashara ya mahindi na mchele. Kwenye Kahawa ubora unatokana na ukubwa wa punje na radha ya punje( baada ya kuonjwa kiutaalamu).

Masoko wa kahawa ni mengi;
1. Walanguzi ambao utawauzia moja kwa moja kwa makubaliano na hasa hununua kwa debe kutokana na bei ya kilanguzi ya kipindi hicho.
2. Pia waweza kuuzia kahawa yako kwenye vyama vya msingi(Amcos) ambao wao huuza kwenye soko la mnada pale Moshi au wanafanya Direct export wakipata mteja.
3. Waweza kupeleka kahawa yako katika viwanda vya kukoboa ambavyo ni vingi pale Moshi na kama una Kahawa nyingi unaweza kuiuzia mnadani kutoka kwenye Kiwanda ulichokobolea.
4. Pia unaweza kutafuta wakulima wakubwa ukawaomba nao wakakuuzia kahawa yako mnadani, au unaweza ukatafuta wenzako wenye kahawa na mkaiuzia kwenye mnada moshi kwa vibali maalumu vya kusafirishia hiyo kahawa kutoka sehemu mnakaitoa.
5. Kama una kahawa nzuri (muonjo kuanzia 85% na kuendele) na ukubwa ambao unafikia A, AA, AAA na haina harufu yoyote kama ni nyingi waweza kupata makampuni ya nje pale Moshi kwa makubaliano ya bei ukawauzia.

Nafikiri kidogo umepata picha ya soko la kahawa.
 
Back
Top Bottom