salisalum
JF-Expert Member
- Oct 27, 2010
- 418
- 136
Maneno tupu hayavunji mfupa. Kuduwaa kwa chura na kukodoa macho hakumzuii ng'ombe kunywa maji. Ndege apigaye biribiri nyingi hawezi kusuka kiota, kumbuka mdomo wake ndio mikono ya kufanyia kazi.
Tendwa ni sawa na upatu uvumao. na asifuye mvua imemnyea. Lakini mwisho Tendwa ni kama la kuvunda lishakosa ubani tena. Au kimsahafu Tendwa ni kama chumvi iliyoharibika, haifai tena ni heri kutupwa barabarani ikanyagwe na wapita njia.
Ukubwa ni dawa lakini kwake ukubwa ni uchuro. Basi ukiona hivo sie watu Tanga twasema keshaliwa huyo.
Ni hadithi iliyokwisha hata ukimghania mwana haimkuni masikio. Laleni salama