Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 03 April, 2024 jijini Dar Es Salaam, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na masuala mengine, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, imefanya mabadiliko madogo ya Sekreteriet ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kuwachagua wajumbe kama ifuatavyo:
  • Ndugu John Mongella kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, akichukua nafasi ya Anamringi Macha ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga,
  • Ndugu Amos Gabriel Makalla kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, akichukua nafasi ya Ndugu Paul Makonda ambaye ameteulia kuwa Mkuu wa Mkoa Arusha.
  • Ndugu Ally Salum Hapi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania, akichukua nafasi ya Ndugu Gilbert Kalima ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga,
  • Ndugu Jokate Urban Mwegelo kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM akichukua nafasi ya Ndugu Fakii Raphael Lulandala ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
Aidha katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imezipongeza Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya Rais Dkt. Hussein Mwinyi, ambaye pia ni Mwenye kiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025.

IMETOLEWA NA IDARA YA ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO 03 APRIL, 2024
Sentensi ya mwisho ni kwa Marais wote wa wili wanatekeleza ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-25.kwa Maana hiyo Rais Dr SSH anatumikia awamu ya Tano maana ndiyo ikoyotengeneza ilani hii ya mwaka 2020-2025.Au nakosea ndugu zangu??
 
Back
Top Bottom