Jakubumba
JF-Expert Member
- Mar 5, 2011
- 1,624
- 500
Nilikuwa na girl friend tangu 2002 hadi 2006. Tulipendana sana ingawa hatukuwa na kipato chochote maana tulikuwa wanafunzi, tulipohitimu form six mwenzangu alianza kubadilika kitabia na nilipomuuliza akawa anakana kabisa,ila mwisho wa siku mambo yakawa hadhalani ana uhusiano na mwanajeshi na ana mpango wa kumuoa! Nilimsihi nampenda tuvumilie tutakuwa na maisha yetu ila akakataa na akaniambia amisha mpenda mtu mwingine. Kwa kuwa huwa naamini mapenzi hayalazimishwi nikajipa moyo na kusonga mbele! Mungu si athumani akanijalia nikapata chuo USA nikawa nimeondoka tz hivo machungu sikuyapata sana maana nikawa niko mbali hata simuoni anavyofurahia penzi lake jipya! Ni miaka minne sasa imepita, nilishtuka sana juzi baada ya kuona sms yake kwenye simu yangu ikinisihi kumpigia! Sikusita nikampigia: kikubwa zaidi akawa ananiomba msamaha turudiane aliko hafurahii maisha! Wanajf! Mie huwa nina msimamo sana ktk maisha yangu, jibu nililompa ni kuwa asijisumbue kuomba msamaha maana sitamkubalia kabisa! Je nina kosa? Ukweli ni kuwa ninatafuta mchumba ila siko tayari kurudi nyuma kwa mtu alienitenda nataka kusonga mbele!!!