Amekataa Shule Mpaka Malengo yake Yatimiee

RGforever

JF-Expert Member
Apr 3, 2011
6,878
5,424
Kwa wale wanaopenda kuangalia Kipindi cha CLOUDS TV Kiitwacho TAKE ONE. Nadhani Mtakumbuka wiki iliyopita Kuna Binti alienda Clouds TV akatoa Matatizo yake lukuki Mpaka Na Machozi Juu mpaka Nikamwonea huruma na Kutoa Laana kwa Waliomtendea Uchafu Ule...kubakwa,yeye ni yatima na mengneyo

NYUMA YA PAZIA

Kumbe Binti Yule katoroka Nyumbani hajaaga kaenda Dar kutafuta Maisha ya Uigizaji ili Atoke na kuwa Super-star...huyo mtoto Analelewa na Baba Mdogo wake.

Sasa baada ya Mtoto yule kwenda kwenye Luninga ndo Ndugu zake wakamwona ndo Kuja Kusema Ukweli wote na Kufichua Maovu yake Yote.. Story ni Ndefu

BUT SIKILIZA REKODI HII

Inauma sana kumsomesha
Mtoto halaf anakuwa hivi...Anatukna hadi Familia
 
Anataka ku ekti, shule hapana, yule mtoto ana matatizo sana!
 
au wewe ndugu yake unataka kufunika hayo?

hahahaha! Mi siyo ndugu yake mkuu Wala hata simjui..... Nimetoa tu taarifa maana huyo binti alikuwa anaomba Msaada CLOUDS TV kama Wanavyoomba Wengine kumbe ni Uwongo Mtupu. Ndugu zake ndo Wamemuumbua
 
Kumbe wako wengi wa hivyo, mimi nami kuna mtoto wa uncle yangu naye kaishia form three hataki kusoma tena anachotaka ni kuigiza tu shule baadaye, du! kazi ipo, hizi TV naona na vyombo vya habari kuutangaza msiba wa Kanumba kama vile alikuwa kiongozi mkuu wa nchi ndo kunakosababisha watoto waone maisha ni kuigiza.
 
Niliangalia hicho kipindi yule binti kwa kiasi fulani ni muongo. Ila ana kipaji cha hali ya juu sana ningeweza ningemsaidia afikie lengo lake. Maana alikuwa composed sana, uwezo wa kusikiliza wa hali juu, hana interruptions, hawi provoked na alikuwa ametulia sana. Kila mzungumzaji alipo mu interrupt yeye alikuwa ananyamaza na kumpa nafasi yeye ndio aseme....hii ni adimu sana kwa watu wengi. Yule binti ana kipaji cha kuigiza...she is a natural actress akipewa nafasi atafika mbali sana kwenye sanaa ya kuigiza........ nilipenda alisema kusoma ni kipaji
 
Back
Top Bottom