All about Edward Hosea, Mwanyika

Taarifa zilizopatika hivi punde mjini Dodoma,ingawa bado hazijathibitishwa rasmi, zinaeleza kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya kuzuia na kupambambana na Rushwa,Bw.Hosea pichani juu amejiuzulu,aidha taarifa hizo zinaeleza kuwa Mkurugenzi huyu alijiuzulu jana usiku na kwamba anasubiri ridhaa ya Rais.Mpaka sasa Bw Hosea anakuwa mtu wa nne kujiuzulu kufuatia sakata zima la Richmond.

Source: http://www.michuzijr.blogspot.com/

Habari za Hosea kujiuzulu zimeshathibitishwa?
 
Mtanzania,

Mwanakijiji anaitangaza HKL News hapa JF- well huwa tunaenda pia kule sema JF wengi ndo tulipopazoea zaidi!

Ingewezekana kuunganisha nguvu pamoja isije kuwa kama kuna competition!

Na habari ishapatikana hapa kwamba Mizengo Pinda kapitishwa! Tuendelee na maoni!
 
Kama Hosea anasema anaenda kanisani Jumamosi, tuseme ni msabato? Kama haya niliyosoma hapa ni kweli si yale yanayofundishwa kwa Wasabato wala dhehebu lingine, sidhani kama huenda kuabudu bali kutembea au kusocialize tu kama walivyo waumini bandia wengi. Mcha Mungu awaye yote yule ni muadilifu maana ameongoka, anayependa binadamu mwenzie. Kumbukeni Zakayo alitangaza kuwarudishia mara dufu wale aliokuwa kawadhulumu. These corrupt figures wanatumia vivuri yva makanis/misikiti kuficha maovu yao. SHAME-------------
 
Sio JF tena?

two independent entities but yet very connected. Uhusiano wetu ni symbiotic in nature and complimentary. My point ya kule ni "Jinsi" klh inavyobreak... hiyo habari... lengo lilikuwa ni kuiweka to the standard ya major news media and we did that... na ukiendelea kuangalia pale and follow up the story you'll get details only KLH can confidently and boldly carry.

Like right now...
 
Ndugu Wana Jf,,napenda Kuwapongeza Katika Jitihada Zenu Za Kusafisha Na Kufumbua Maovu,,niwakati Wa Kushangilia Ushindi Baada Ya Kuona Mafisadi Wakitamka Hadharani wanajiuzulu,,nimeuishwa Kuandika Haya Baada Ya Kuona Na Kusoma Yaliyomo Lwenye Kamati Na Mapendekezo Yake Sasa Yanaanza Kufanya Kazi Likiwemo Kuwaadabisha Wote Wahusika Walioshirki Katika Msiba Wa Ndugu Yetu""tanesco""....katika Hili Ningefurahi Tu Kama
Ningeona Waliotajwa Kwa Majina Kufwata Nyayo Za Aliekuwa Waziri Mkuu,,je Baada Ya Aho Wote Mwanyika ,,hosea,,mama Kejo Wa Wizara Ya Nishati Na Madini Wewe Pamoja Na Wenzako Wote Tunaomba Muachie Nagazi Ama Kutangaza Hadharani Ama Kwa Kuandika Barua ////tafadhalini Muwahi Mapema Kabla Aibu Aijawakumba...huyu Moto Alieingia Hana Mapenzi Na Mtu Nawashauri Hilo Mapema Nduguzanguni......

Tukiwa Hapa" kufundisha Na Kusafisha Uozo"" Tunawaomba Mkisoma Taarifahizi Mfanye Hima Mara Moja Na Kujua Democracy Ci Kungangania Madarka Bi Kukubali Kuachia Ngazi Pale Unapoaribu....

wenu

mafish
 
BAADA ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kulaumiwa na Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza utaratibu wa zabuni ulioipa ushindi kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond Development LLC kuwa iliisafisha wakati imeonekana ina uozo, Mkurugenzi wake Mkuu Edward Hosea ameitetea taasisi hiyo na kuisafisha kuwa ilifanya kazi yake kwa mujibu wa sheria inayoiongoza taasisi hiyo.

Hosea alisema kazi ya taasisi hiyo ni kupambana na rushwa na si kupambana na mikataba mibovu kama ilivyoonekana kwenye ripoti hiyo kuwa kulikuwa na tatizo la mikataba mibovu.

Mkurugenzi huyo ambaye amekuwa kimya tangu kutolewa kwa ripoti hiyo wiki iliyopita, alisema kuwa taasisi yake inafanya kazi kwa kufuata sheria ya rushwa ya mwaka 1971.

“…Kuna watu wakubwa wenye madaraka, vitendea kazi, uwezo, wenye fedha na wenye magazeti wanayoyatumia kujifanya vipofu wa sheria kwa sababu wangeisoma sheria wasingenihusisha na suala la Richmond,” alisema Hosea.

Mkurugenzi huyo ambaye alikuwa anahudhuria mkutano wa kawaida wa wakuu wa taasisi za kupambana na rushwa kwa Afrika Mashariki unaofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, alipoulizwa juu ya uvumi uliozagaa kuwa amejiuzulu alisema, “ningejiuzulu nisingesimama hapa”.

“…Mimi namuamini Rais, nikiwa kama mteule wa Rais nipo tayari kwa shughuli ya uamuzi wowote dhidi yangu ili sheria ichukue mkondo wake…la msingi the rule of law must be observed”.

Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita na Mwenyekiti wake Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, ilisema kuwa Takukuru katika taarifa yake kwamba Taifa halikupata hasara kutokana na Richmond ililenga kuficha ukweli.

“…Hivyo iliishia kujikanganya kwa kukiri kuwapo kwa mapungufu lakini yasiyokuwa na athari. Taarifa hiyo imeng’oa hadhi na heshima ya chombo hiki muhimu cha kitaifa kurejesha heshima ya umma mabadiliko ya haraka ya uongozi wa taasisi hiyo yafanyike,” alisema Mwakyembe katika ripoti yake.

Source: Habari Leo, Feb 16, 2008.
 
Kama Hosea akibaki , basi ujue ule Mkataba unahusu Mamlaka ya Juu ya Nchi.
Hivyo Lowasa watakuwa wamemtoa Kafara.
 
Dr Hosea Must GO Now!!!!

Dr Hosea has failed the most powerful and most dependable institution in the nation.

TAKUKURU is, in part, the equivalent of FBI in the US, which never leaves any stone unturned in the interest of the Nation. Why does he (Hosea) leave some stones unturned and thereby undermining the power of TAKUKUKURU? Yet he maintains that he will never resign; why? who gives him the steam?
 
"Hosea alisema kazi ya taasisi hiyo ni kupambana na rushwa na si kupambana na mikataba mibovu kama ilivyoonekana kwenye ripoti hiyo kuwa kulikuwa na tatizo la mikataba mibovu."

Napendekeza huyu akapimwe akili, inawezekana si mzima kwa sasa. Hivi mikataba mibovu inachochewa na nini kama si rushwa? Au, matokeo ya rushwa kwenye biashara za kimataifa huwa nini kama si mikataba mibovu? Hii kweli inahitaji mtu mwenye PhD kui analyse? Hivi mbona tunafanywa wajinga kiasi hiki jamani?
 
.......Hosea alisema kazi ya taasisi hiyo ni kupambana na rushwa na si kupambana na mikataba mibovu kama ilivyoonekana kwenye ripoti hiyo kuwa kulikuwa na tatizo la mikataba mibovu........Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita na Mwenyekiti wake Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, ilisema kuwa Takukuru katika taarifa yake kwamba Taifa halikupata hasara kutokana na Richmond ililenga kuficha ukweli.

“…Hivyo(TAKUKURU) iliishia kujikanganya kwa kukiri kuwapo kwa mapungufu lakini yasiyokuwa na athari. Taarifa hiyo imeng’oa hadhi na heshima ya chombo hiki muhimu cha kitaifa kurejesha heshima ya umma mabadiliko ya haraka ya uongozi wa taasisi hiyo yafanyike,” alisema Mwakyembe katika ripoti yake.

...Give me my gun....
 
Huyu Bw Hosea ni PHd kweli??
Mimi nadhani ana matatizo makubwa sana vinginevyo statement yake ni pure and simple BLACKMAIL. Huyu bwana ana guts za kumtisha Rais JK!!

Kwa nanmna yeyote mpira umechezwa kwa JK, atauchezaje??
 
Hiyo ni kauli mbaya sana kutoka kwa mkuu huyo. Kama kweli kasema akiamini hivyo, basi hajui anachokifanya, na wajibishwe kwa kutokujua wajibu wake. The whole issue is UFISADI..Corruption..Rushwa yeye anasema nini?!!!!!!!.Jamani huyo mtu na Permanent head Damage(PhD) yake vipi!. I used to like this guy very much..mmh..traitor! Kitendo cha kusema nchi haijapata hasara kwa mkataba huo wakati anajua ni mbovu maana yake nini? Ubovu wa mkataba ni nini kwa Hosea? Au umeandikwa kwenye used toilet paper ndo maana unaitwa mbovu, na si wenye kutia nchi hasara?.

I'm disappointed in Hosea and I think I hate him now. Please JK do us a favour, expel this stinking idiot.Period!.
 
Hiyo ni kauli mbaya sana kutoka kwa mkuu huyo. Kama kweli kasema akiamini hivyo, basi hajui anachokifanya, na wajibishwe kwa kutokujua wajibu wake. The whole issue is UFISADI..Corruption..Rushwa yeye anasema nini?!!!!!!!.Jamani huyo mtu na Permanent head Damage(PhD) yake vipi!. I used to like this guy very much..mmh..traitor! Kitendo cha kusema nchi haijapata hasara kwa mkataba huo wakati anajua ni mbovu maana yake nini? Ubovu wa mkataba ni nini kwa Hosea? Au umeandikwa kwenye used toilet paper ndo maana unaitwa mbovu, na si wenye kutia nchi hasara?.

I'm disappointed in Hosea and I think I hate him now. Please JK do us a favour, expel this stinking idiot.Period!.


Hosea sote tunajua hakupewa nafasi kwamba anaweza bali kukomoa na kwa vile alimsaidia JK kuupata Urais basi alipewa fadhila kama wengine walivyo pewa.Ndiyo maana anadiriki kusema haya kwa kuwa anawajua wachafu wengi na labda hata uchafu wa Ikulu .A big test to you Mr.Prezidenti .Tuna angalia na mapendekezo nadhani yamesha fika Ikulu .Yaani hadi Hosea hajajiondoa tu ? Yuko kama Mwanyika ?
 
Guys, I think the man is right!

Mwanakijiji kumbukeni sana nilipiga sana makelele kuhusu matumizi ya neno RUSHWA na tukalitungia sheria bila kufahamu maana na mapana ya neno hilo. Muswada ulisukumwa haraka haraka ukapitishwa ukiwa umeacha mabo mengi sana muhimu. Nakumbuka hata wewe ktk mada mojawapo uliwahi kusema kuwa sii lazima tunapozungumzia Rushwa basi iwe, lazima mtu kachukua/katoa hongo hali tumesahau kuwa CCM waliukubali muswada huu kwa sababu haukuwagusa wao kama viongozi wanao Hujumu uchumi wakitumia wadhifa wao na Azimio la Zanzibar linalowaruhusu kufanya Biashara.
Sasa wataweza vipi kufanya biashara hizo ikiwa hawana ruksa ya kutumia nafasi zao kupata connection?...How will it work halikutazamwa hili..
As a fact hata Rostam Aziz hana makosa ikiwa Richmond ni kampuni yake na hatuwezi mshtaki kwa sababu anakuwa protected na Azimio la Arusha pili, Richmond ni incorporated yaani entity inayojiendesha kama kampuni na tatu hakupokea wala kutoa rushwa kupata Tender hiyo..

Mkorogo wote wa sheria tumefungashiwa sisi na ndio maana Taasisi hiyo ya Dr. Hosea imeitwa - Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Kwa ufinyu wake haiweki hujuma za uchumi wa taifa letu..Deal la Richmond halina ushahidi wowote wa Rushwa lutumika.

Kutumia madaraka yako kupata Tender ya serikali sio kosa wala Rushwa hata kidogo na sheria za Azimio zinawa protect zaidi...

Ni mawazo yangu mnaweza nielemisha zaidi kama nimekosea.
 
Ninapata mashaka yale yale ya siku zote! Kwamba huwa hatusomi vizuri mambo hata ikibidi btn the lines...


Chombo kilichoshindwa kuchunguza ile rushwa ya Richmond kilikuwa ni PCB au TAKURU...

Naomba mukumbuke kwamba PCB/TAKURU ilianzishwa na sheria dhaifu sana... hiyo sheria haikuweza kupambana na rushwa hata kidogo... Na sio PCCB/TAKUKURU.
Ndio maana sheria ikapelekwa kubadilisha hiki chombo kile na sasa ni PCCB/TAKUKURU...

Nina pata mashaka kwamba Tume ya Mwakyembe iliihukumu PCB/TAKURU kwa sheria ya PCCB/TAKUKURU. (Ni kwa bahati mbaya hii misleading ni rahisi sana kwa kuwa aliyekuwa mkurugenzi wa PCB/TAKURU ndiye huyo huyo aliendelea kuwa mkurugenzi wa PCCB/TAKUKURU... Hivyo jamii imeshindwa kujua mwanzo na ukomo wa vyombo hivyo viwili.

Bila kumtetea Hosea... lakini najua hajiuzulu kwa sababu hii tu na si nyingine...

PCB/TAKURU ilikuwa ina zungumzia bribing tu! ambayo sio Tume ya Mwakyembe wala PCB/TAKURU walioweza ku-establish kwamba rushwa (bribing and not corruption) ilikuwepo....

Ni kwa sababu hii bado Hosea ana confidence maana ripoti yake imefanya kazi kwa kufuata sheria ile ya 1971 ya Rushwa

Mwisho:

Kwa sheria za PCCB/TAKUKURU nadhani wangetoka na ripoti tofauti maana sheria inawapa upana mkubwa zaidi!!!

Nasikitika Watanzania tu wavivu wa kusoma na kusikiliza watu kwa makini!!!!
 
Amechemsha huyo, kiwewe as he fully knows he's gone.


Zomba unaweza kushangaa kuona JK anamwacha anaenelea kupeta mkuu .Wacha tuone maana Pinda ni serious na nadhai hataacha kumpa Rais ushauri wa uhakika .Hope Hosea will be ditched
 
Back
Top Bottom