All about Edward Hosea, Mwanyika

Ogah,
Labda hujanielewa vizuri na pengine unachanganya sheria zetu na huko nje..

WHEN, WHERE, WHAT, WHO, WHY and HOW ni kazi aliyoifanya isipokuwa hakuona charges zozote zinazohusiana na Rushwa hata kama kulikuwa na utata wa mkataba wenyewe. Kama vile tunavyoona Mkataba wa Buzwagi hata waziri mkuu wa Canada ameshindwa kutusaidia kwa sababu anafungwa na sheria za nchi yake.

Kifupi ni hivi deal lote la Richmond kupelekwa Takuru ilikuwa kuficha ukweli na kama sikosei Lowassa alikuwa mbele sana kujibu hoja na kusema tusubiri. Hivyo basi JK, Lowassa na viongozi wengi ngazi za juu wote walifahamu kilichotendeka bila hata uchunguzi wa Hosea.
Kitu ambacho hawakuelewa ni kwamba wananchi na hasa wagazeti yetu pamoja na hapa JF ndio tulioshinikiza uchunguzi zaidi na pengine hata Mzee Six kukosa boya la kuelea bungeni ikabidi kamati nyingine iundwe.
Hawa walipewa madaraka zaidi nje ya sheria ziizokwisha pitishwa ikiwa ni pamoja na access ya upana wa hujuma hizi. Nitashangaa sana ikiwa kweli tunaamini Hosea ajiuzuru hali yeye aliambiwa atafute kile alichotakiwa kukitafuta... Rushwa, mengine yote ni matokeo ya nguvu zenu wananchi kumshikia bango JK hadi kakubali swala hili.

Kama alivyosema mwenyewe nia yake ilikuwa kubadilisha baraza la Mawaziri toka November 2007 hii ina maana alijua kuna maovu yanatendeka. Huwezi badili baraza la mawaziri bila sababu na imekiri kuwa sakata la Richmond ndilo limemlazimu kuharakisha.
So he knew about Meghji, Karamagi na scandal nyinginezo zote kabla kabisa ya uchunguzi wa kamati teule ya bunge.
Still he could have stopped kupelekwa bungeni kabla ya Bush kuingia nchini...
Jamani tusiwe wajinga Hosea ni mlinzi mlangoni ambaye anajua kila kinachoendelea ndani ya nyumba ya bwana.
 
Bob
Hosea kazi imemshinda..................kama angekuwa anajua kinachoendelea ndani kwa bwana Mkubwa asingetoa zile statements za ku-clear Richmond...............msomi kama yeye angetambua kuwa hili ni bomu in the making
 
Mwandishi Wetu, Zanzibar
Daily News; Friday,February 15, 2008 @07:15

BAADA ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kulaumiwa na Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza utaratibu wa zabuni ulioipa ushindi kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond Development LLC kuwa iliisafisha wakati imeonekana ina uozo, Mkurugenzi wake Mkuu Edward Hosea ameitetea taasisi hiyo na kuisafisha kuwa ilifanya kazi yake kwa mujibu wa sheria inayoiongoza taasisi hiyo.

Hosea alisema kazi ya taasisi hiyo ni kupambana na rushwa na si kupambana na mikataba mibovu kama ilivyoonekana kwenye ripoti hiyo kuwa kulikuwa na tatizo la mikataba mibovu.

Mkurugenzi huyo ambaye amekuwa kimya tangu kutolewa kwa ripoti hiyo wiki iliyopita, alisema kuwa taasisi yake inafanya kazi kwa kufuata sheria ya rushwa ya mwaka 1971.

“…Kuna watu wakubwa wenye madaraka, vitendea kazi, uwezo, wenye fedha na wenye magazeti wanayoyatumia kujifanya vipofu wa sheria kwa sababu wangeisoma sheria wasingenihusisha na suala la Richmond,” alisema Hosea.

Mkurugenzi huyo ambaye alikuwa anahudhuria mkutano wa kawaida wa wakuu wa taasisi za kupambana na rushwa kwa Afrika Mashariki unaofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, alipoulizwa juu ya uvumi uliozagaa kuwa amejiuzulu alisema, “ningejiuzulu nisingesimama hapa”.

“…Mimi namuamini Rais, nikiwa kama mteule wa Rais nipo tayari kwa shughuli ya uamuzi wowote dhidi yangu ili sheria ichukue mkondo wake…la msingi the rule of law must be observed”.

Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita na Mwenyekiti wake Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, ilisema kuwa Takukuru katika taarifa yake kwamba Taifa halikupata hasara kutokana na Richmond ililenga kuficha ukweli.

“…Hivyo iliishia kujikanganya kwa kukiri kuwapo kwa mapungufu lakini yasiyokuwa na athari. Taarifa hiyo imeng’oa hadhi na heshima ya chombo hiki muhimu cha kitaifa kurejesha heshima ya umma mabadiliko ya haraka ya uongozi wa taasisi hiyo yafanyike,” alisema Mwakyembe katika ripoti yake.
 
Mitomingi, hiyo post ipo mwanzo kabisa wa thread hii, nahisi umeona uvivu kusoma toka mwanzo...
 
Mkandara, Ogah;

Nadhani tunaelekea kuelewana vizuri, yafuatayo ni muhimu sana.

1. Sheria mpya ya PCCB ilisainiwa na Mh. Rais lini? na Ilitangazwa kwenye Gazeti la Serikali lini? Kwa ajili ya Kuanza kutumika?

2. Dr. Hosea atafutwe na aulizwe, uchunguzi wake Uli-base kwenye Taasisi ipi PCB au PCCB?

3. Nakubaliana kwamba kuna maneno kwenye ile riport ambayo Dr. Hosea yuko responsible nayo,,, nayo ni yale ya kusema hapakuwa na adhari yoyote kwa nchi!!! haya hakuulizwa na anahitajika kujibu kwa nini alisema hivyo, nani kamtuma na vigezo gani alitumia kusema hivyo.
4. Aidha kwenye issue ya Hongo kweli hakuna sehemu ilipatikana hapo tume-close.

5. Ninavyofahamu mimi sheria mpya ya PCCB kama ndiyo ilitumika... then Dr. Hosea anastahili kupelekwa kule kwenye yale majengo yaliyokaribu na Airport aliposhukia George W. Bush. Sheria mpya inafuatilia corrupion na sio tu bribing kama ilivyokuwa ya Kwanza... Kwa mfano sheria mpya ina uwezo wa kuhoji utajiri unaokuja kiajabu kiajabu!!!
 
1. Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita na Mwenyekiti wake Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, ilisema kuwa Takukuru katika taarifa yake kwamba Taifa halikupata hasara kutokana na Richmond ililenga kuficha ukweli. “…Hivyo iliishia kujikanganya kwa kukiri kuwapo kwa mapungufu lakini yasiyokuwa na athari. Taarifa hiyo imeng’oa hadhi na heshima ya chombo hiki muhimu cha kitaifa kurejesha heshima ya umma mabadiliko ya haraka ya uongozi wa taasisi hiyo yafanyike,” alisema Mwakyembe katika ripoti yake.

2.
Hosea alisema kazi ya taasisi hiyo ni kupambana na rushwa na si kupambana na mikataba mibovu kama ilivyoonekana kwenye ripoti hiyo kuwa kulikuwa na tatizo la mikataba mibovu.
“…Kuna watu wakubwa wenye madaraka, vitendea kazi, uwezo, wenye fedha na wenye magazeti wanayoyatumia kujifanya vipofu wa sheria kwa sababu wangeisoma sheria wasingenihusisha na suala la Richmond,” alisema Hosea. “…Mimi namuamini Rais, nikiwa kama mteule wa Rais nipo tayari kwa shughuli ya uamuzi wowote dhidi yangu ili sheria ichukue mkondo wake…la msingi the rule of law must be observed”. [/U
]

Hosea tulimwambia toka alipotoa ripoti yake mbuzi, kuwa kama kuna mapungufu ya sheria kwenye taassisi yake katika kupambana na rushwa au viongozi wezi, basi angeliomba bunge letu limpe anachohitaji, yaaani ammendment ya sheria ya 1971 ili aweze kuwashughulikia hao wezi, wewe huwezi kupoteza hela zote alizotumia Hosea, kufanya uchunguzi wa Richimonduli, halafu mwishoni ukaishia kutumabia taifa kuwa huna sheria za kulishughulikia tatizo, ila tu uanangalia mikataba, that is pure nonesense,

Hivi mkataba gani hapa duniani leo unaweza kuwa na mapungufu? kinachotakiwa kutafutwa ni nia na madhumuni ya waliouleta mkataba, kama sisi bongo kama taifa tulimuomba Hosea, afanye uchunguzi wa mkataba tu basi na sisi as a nation something is wrong with us, na siamini it to be the truth of the matter, kwa sababu ukiangalia hapo juu Mwakyembe anaweka wazi, tatizo la Hosea, kuwa kwa yeye kusema kuwa taifa halikupata hasara kwenye Richmonduli ni nonesense, sasa this has nothing to do na mapungufu ya sheria anayoizungumzia Hosea, anachosema Mwakyembe, ni kwamba haiwezekani a man wa calliber ya Hosea, afanye utafiti kama alioufanya, halafu aishie kusema kuwa kuwa hakukuwa na hasara kwa taifa kwenye mkataba wa Richmonduli, wakati taifa letu lilikuwa likilipa dola $ 145,000 kwa siku kwa kampuni ambayo haipo,

Hosea aondoke tu, tunajua kuwa alitakla kujiuzulu akakataliwa na rais, ndio maana sasa ana ubavu, lakini aondoke tu maana hili sooo bado linaunguruma bungeni kwa hiyo linakuja mzee Hosea, huja-save bado!
 
2.]

... kwa sababu ukiangalia hapo juu Mwakyembe anaweka wazi, tatizo la Hosea, kuwa kwa yeye kusema kuwa taifa halikupata hasara kwenye Richmonduli ni nonesense, sasa this has nothing to do na mapungufu ya sheria anayoizungumzia Hosea, anachosema Mwakyembe, ni kwamba haiwezekani a man wa calliber ya Hosea, afanye utafiti kama alioufanya, halafu aishie kusema kuwa kuwa hakukuwa na hasara kwa taifa kwenye mkataba wa Richmonduli, wakati taifa letu lilikuwa likilipa dola $ 145,000 kwa siku kwa kampuni ambayo haipo,

Mkuu Field Marshall ES,

Huu ushabiki wa Hosea kwenye hiyo sentensi ndio utamwondoa kwenye kiti kile, ieleweke wazi hakuna aliyemuuliza kwamba hasara ni kiasi gani? hiyo tungeuliza wengine na wala sio PCCB...
 
Mkuu huyu Hosea, alitakiwa kuondoka, nilisikia majuzi kuwa ameomba kuondoka, sasa nafikiri alipewa grace na muungwana, ndio maana anajikakamua sasa, aende tu kama tulivyosema Mama Meghji, aondoke, na akaondoka!
 
If ours is not a "lame duck" president I do not know who is.

Huyu mpumbavu hajui hata kukaa kimya baada ya kuharibu, na sasa anataka kuleta arrogance itakayo fuel moto upya?

Mazingaombwe, bangusilo, mauzauza na mengine yanayotia kinyaa kama hayo.
 
Ogah,
Labda hujanielewa vizuri na pengine unachanganya sheria zetu na huko nje..

WHEN, WHERE, WHAT, WHO, WHY and HOW ni kazi aliyoifanya isipokuwa hakuona charges zozote zinazohusiana na Rushwa hata kama kulikuwa na utata wa mkataba wenyewe. Kama vile tunavyoona Mkataba wa Buzwagi hata waziri mkuu wa Canada ameshindwa kutusaidia kwa sababu anafungwa na sheria za nchi yake.

Kifupi ni hivi deal lote la Richmond kupelekwa Takuru ilikuwa kuficha ukweli na kama sikosei Lowassa alikuwa mbele sana kujibu hoja na kusema tusubiri. Hivyo basi JK, Lowassa na viongozi wengi ngazi za juu wote walifahamu kilichotendeka bila hata uchunguzi wa Hosea.
Kitu ambacho hawakuelewa ni kwamba wananchi na hasa wagazeti yetu pamoja na hapa JF ndio tulioshinikiza uchunguzi zaidi na pengine hata Mzee Six kukosa boya la kuelea bungeni ikabidi kamati nyingine iundwe.
Hawa walipewa madaraka zaidi nje ya sheria ziizokwisha pitishwa ikiwa ni pamoja na access ya upana wa hujuma hizi. Nitashangaa sana ikiwa kweli tunaamini Hosea ajiuzuru hali yeye aliambiwa atafute kile alichotakiwa kukitafuta... Rushwa, mengine yote ni matokeo ya nguvu zenu wananchi kumshikia bango JK hadi kakubali swala hili.

Kama alivyosema mwenyewe nia yake ilikuwa kubadilisha baraza la Mawaziri toka November 2007 hii ina maana alijua kuna maovu yanatendeka. Huwezi badili baraza la mawaziri bila sababu na imekiri kuwa sakata la Richmond ndilo limemlazimu kuharakisha.
So he knew about Meghji, Karamagi na scandal nyinginezo zote kabla kabisa ya uchunguzi wa kamati teule ya bunge.
Still he could have stopped kupelekwa bungeni kabla ya Bush kuingia nchini...
Jamani tusiwe wajinga Hosea ni mlinzi mlangoni ambaye anajua kila kinachoendelea ndani ya nyumba ya bwana.

Mkuu, naona tuna'split hairs' hapa katika kujiingiza kwenye mjadala wa semantics. Ninachoshandwa kuelewa ni kuwa pale Mkuu alipoona kuna matatizo katika mkataba, alifanya nini kutafuta kwa nini pamoja na hayo matatizo hawa jamaa waliendelea kubebwa? Amefanya uchunguzi au utafiti gani kuhakikisha kuwa hapakuwa na kitendo cha rushwa? Au mpaka ionekana cheque aliyoandikiwa mhusika? Kama mimi nikitumia nafasi yangu kupindisha sheria ili swahiba wangu apate kandarasi, hiyo si personal profit (profit si lazima iwe benjamins)inayozungumziwa? Mimi nadhani Mkuu aweke wazi walichokifanya mpaka wakahakikisha kuwa hakuna rushwa katika dili nzima. Hii itamuondolea kiwingu. Pamoja na hao ambao pengine jamii inawahukumu vibaya.
 
Jamani ehhhee! Msing'oane meno bure hapa, Hosea anajua kila kitu tangua A to Z. na anajua alichoongea sio anachokiamini. Na MP ametoa tamko jana kwamba yote yaliyopo kwenye ripoti ya HM yatafanyiwa kazi. Na kama ni kweli alitaka kujiuzulu akaambiwa na Jk atulie basi kaingizwa mkenge huyo. Yatamkuta ya makubwa zaidi ya Balali huyo.

Ingekuwa bora kama angefunga mdomo kwanza! kwa sababu alichokiongea hapa ni matusi. hata kama sheria ya 1971 ilimzuia angeonyesha hivyo kwenye ripoti yake ya uchunguzi, sio kuja kutoa pumba sasa.

Anyway, time will tell. Siku inakuja atakataa kuongea na waandishi juu ya kauli yake hii ya kitoto.
 
MZAMIVU HOSEA KAKA YANGU NAKUPONGEZA KWA MAJIBU MAFUPI YANAYOONYESHA UKAKAMAVU WA KITAALUMA NA PROTOKALI ZA KIDOLA,MEDIA ZA TANZANIA ZIMEKUWA ZIKIPEPERUSHA HABARI KWA SHINIKIZO LA MATAJIRI WALIO KTK KITI CHA ENZI CHA WAKUBWA WALIOSHIKA MPINI KWA WAKATI HUO NA KUSAHAU WAJIBU WA KUTUFUNDISHA KUWA TAARIFA NI SHULE KWA JAMII NA SIYO HUKUMU. HILI NI TATIZO KUBWA SANA KWA WAPASHAJI WETU WA HABARI,NIMEANGALIA PRESS CONFERENCE YA BUSH NA JK LAKINI TUTAKACHOSOMA KESHO NI AIBU NA BLABLA ZA KILA SIKU .

HITIMISHO LA MZAMIVU MWAKYEMBE JUU YA LOWASSA LIKO WAZI KUWA SERIKALI NA HATA BUNGE HALINA LA KUMFANYA LOWASSA LAKINI HAWA JAMAA WANACHO RIPOTI WANA HABARI WETU NI JAZBA ZA WABUNGE AMBAO HATA WAO SIKUONA SHABAHA YAO HALISI JUU MICHANGO YAO,TANGU IMESOMWA BUNGENI NA HUMU JF NI WAZI, LAKINI BADO MBUNGE ANASIMAMA KUPIGA KELELE ZA LOWASA LOWASA LOWASA NA WENGINE WANASEMA ASIPEWE HAKI YA USTAAFU,NINA MASAHAKA NA UWEZO WA WABUNGE WETU KTK KUCHAMBUA MAMBO ,NILICHOJIFUNZA HAWA JAMAA WALIINGIA PALE WAKIWAWAMELISHWA NA KUKARIRISHWA HILO ILI KUTUPUMBAZA WATZ, NAKIRI RICHMOND NI AIBU KWA TAIFA LAKINI MICHANGO YA WABUNGE YETU 90% ILIKUWA NI AIBU YA WAKURUPUKAJI NA NDIYO MAANA NAWAANGALIA HAWA WAZAMIVU WAWILI KAMA NI MFANO WA KITAFITI KABLA YA KUKURUPUKA KTK MIC NA RUNINGA ZETU ,MWAKYEMBE ANASOMA" KAMATI HAINA UTHIBITISHO WOWOTE DHIDI YA LOWASSA NA HATA PALE ANAPOTAJWA KTK MAWASILIANO YA KIUTENDAJI HUENDA NI AINA YAKE YA UFANYAJI KAZI NA SIYO UFISADI AU RUSHWA" MEDIA NA WABUNGE HAMKUONA JANJA HII YA MZAMIVU MWAKYEMBE? KWANINI TUMSHANGAE MZAMIVU HOSEA? LAKINI KALI ZAIDI NI PALE LOWASSA ALIPOBAINISHA KUWA TATIZO NI UPM WAKE,A WISH WHICH I'M GOING TO GRANT" JF tusiingizwe mkenge na game hii lakini tuiangalie in positive way kwa vizazi vijavyo kujiepusha na saga za namna hii.
Ahsanteni
 
Mkandara
nilipokusoma jana niliamua kujipa muda wa kufikiria maana ya neno rushwa. na kama Hosea anasema anapambana na rushwa na si mikataba mibovu basi kuna mchezo wa kijinga anaufanya na kutufanya sisi wote wajinga.
Katika tafsiri anayotaka tuiamini kuwa corruption maana yake ni rushwa basi amechemsha kwani rushwa ni bribery na corruption ni uozo sasa hapo anatutega tena na bomu la mkononi. Inafaa akamatwe, aminywe korodani aeleze ukweli kwa nin anaudanganya umma kwa taarifa potof??

Hosea ni mzembe na mwongo wa karne.
 
Msanii,
Sijui mkuu kati yetu nani kakosea lakini nijuavyo mimi Rushwa ni Corruption na Bribery ni Hongo!..
Kama alivyosema Kasheshe, mimi najaribu kutazama jinsi scandal hili lilivyojaribiwa kuzimwa kisheria lna makusudi kabisa..
Kwa maana hiyo sina maana Hosea yuko safi lakini yawezekana akawa sawa kisheria. Huku mkuu wakati mwingine katika timutimu za Mjini watu hukamatwa na Polisi na wakakutwa hawana visa ama sheria ya kuishi nchi hii. Polisi hulazimika kumwachia huyo mtuhumiwa ikiwa hana kosa linalohusiana na kazi ya huyo Polisi..sheria haimruhusu kujihusisha na maswala ya Uhamiaji.
Hivyo basi Hosea anachosema ni makusudi na kiburi akitumia sheria na yale yaliyokuwa yamepangwa toka mwanzoni yaani kuficha kilichokuwemo. Sasa basi kinachotakiwa toka sasa hivo ni kuelewa huyo Hosea alichukua ngapi ama ni nani aliyemwabia asifanye kazi yake bila kujali mipaka ya sheria kwani Tanzania hatuna mipaka kama hiyo ktk Upelelezi. Isipokuwa tuna mipaka kwa wahusika yaani huwezi kumvamia kiongozi na hasa waziri mkuu na kumtaka ajisaliishe.
Kwa hiyo utetezi wake ni ujinga kweli lakini kisheria nadhani alifungwa na hilo neno Rushwa. Hilo swala la nchi kupata hasara huwezi kulijadili kwa mapana ikiwa ras mwenyewe alisema tuwape muda hao Richmond hali ni wakati huo huo Hosea alikuwa akifanya Upelelezi... Hii ni cover up ya hali ya juu sana lakini imeshindikana kwani pakacha lilivuja vibaya sana. Na ndio maana kamati ya CC walimwomba rais kujiuzuru kwa PM na uchunguzi ufanyike. Ni rais aliyemkubalia mzee six kupokea ombi la kuundwa kwa kamati teule kuchunguza swala la Richmond kwani EL na RA walikuwa tayari sumu kubwa kwa chama na baadhi wazee wa chama. This was after uchunguzi wa Hosea..usidanganywe na mtu kuwa mzee Six ndiye aliyetoa amri... hakuwa na ubavu huo hata kidogo mbele ya EL ama RA.
Kwa hiyo ni lazima ajiuzuru kwani yumo ktk scandal hiyo ambayo kama kweli tunatafuta haki basi sidhani kama kuna mtu atabakia ikifikishwa mahakamani.
 
Mkandara,

Tafsiri ya Corruption kama uliyotoa, imetolewa kwa ufasaha kwenye sheria ya PCCB ya sasa.

Tafsiri ya Corruption ya 1971 (PCB) ilitafsiriwa kama hongo... Nakukumbusha ahadi ya CCM na TANU (sitatoa au kupokea rushwa) walikuwa na maana hongo.

Naomba niwakumbushe kwamba kilio kikubwa cha watu wa PCB wakati ule ilikuwa ni sheria ambayo ilikuwa ina wigo mdogo sana... ikiwa maana ilikuwa ikitamke hongo tu!!!
 
Nashindwa kumuelewa HOSEA
Jamani wanajf humu ndani inaonesha kuna wanasheria wengi sana tena waliobobea ikibidi zaidi ya mwakyembe na Hosea,ndio maana hii mijadala labda haiishi,lakini pamoja na hayo siasa na misukumo binafsi nayo imetuelemea mno kiasi saa nyingine tunashindwa kutoa hoja na badala yake tunang'ang'ania misimamo yetu. Aliyemwanazuoni atakubaliana nami kuwa lazima akubali kupingwa na katika kufanya hivyo hoja yoyote anayoitoa anaitoa akiwa na open mind huku akielewa kuwa wapo watakaompinga wapo watakaomkubali na pia wapo watakaotaka kuelimishwa zaidi.Lakini katu hatowachukia wanaompinga kwani nao wanahoja zao shindani.

Baada ya kusema hayo,sasa narudi kwa HOSEA.Mhe. HOSEA wakati anachunguza sakata la Richmond alikuwa akitumia sheria namba 16 ya mwaka 1971 kadiri ilivyofanyiwa marekebisho kwa vipindi toauti.Vilevile wakati HOSEA nachunguza kuhusu sakata la balozi Mahalu vilevile alikuwa akitumia sheria hii hii. Makosa yote haya mawili yalihusisha viongozi wa serikali kwa upande mmoja na watu binafsi au makampuni yaliyoko nje ya nchi. Na katika makosa yote hayo mawili yaliyoiingoza hasara nchi yetu hakuna aliyewahi kushikwa red handed akiomba,au kupokea rushwa. Yote yanahusisha ushahidi wa kimazingira tu. Makosa yote mawili pia hayahusishi rushwa tu bali pia uhujumu uchumi.

Hivi karibuni Hosea amesikika kwenye vyombo vya habari akisema,yeye kazi yake ni rushwa na kwamba alifanya kazi kwa mujibu wa sheria ya rushwa ya mwaka 1971 ilivyokuwa,hivyo kazi yake si miktaba wala uhujumu uchumi. Jibu hili linafanana sana na alilolitoa mwanyika wakati anahojiwa na kamati ya mwakyembe. Swali hapa je,uhujumu uchumi na mikataba ni kazi ya nani? si makusudi yangu kujibu swali hili leo hapa,bali kuangalia uhalali wa kauli za HOSEA kuhusu wajibu wake kwa masuala yote hayo mawili hapo juu.
TAKURU ya zamani iliundwa kwa mujibu wa kifungu cha tatu cha sheria ya rushwa mwaka 1971 ikiwa na majukumbu yafuatayo,hapa nitanukuu
1.TO take necessary measures for the prevention of corruption in the public,parastatals and private sector.
2.To investigate and prosecute offences under the Act and other offences involving corrupt transactions.
3.Advise the governement and other parastatals organization on the ways and means to prevent corruption.
Sheria pia inaendelea kusema kuwa wakati wakitekeleza majukumu yao,watakuwa na mamlaka ya kipolisi sawa na askari mwenye cheo cha ASP.Hivyo kwa ufupi hizo ndizo kazi zao. Ukiangalia kwa haraka haraka tu utakuta kwa kauli za hosea,haguswi na richmondi kwani labda alishafanya kila jinsi kuzuia rushwa,pili alishachunguza akakuta hakuna rushwa ya moja kwa moja na tatu aliishauri serikali kwamba iendelee tu na richmond kwani hakua rushwa na haipati hasara yoyote.
Hivi kusema serikali inapata hasara au haipati ilikuwa ni kazi yake? hiyo kazi inafall wapi kati ya hizo kazi tatu kuu hapo juu? naam labda alisema kwakuwa hizo zilikuwa hadidu za rejea za uchunguzi wake. Lakini mimi naenda mbali zaidi.

Ukisoma kifungu cha 6 cha sheria hiyo ya zamani kinasema kwamba
mtu yeyote ambaye kwa kujua atampa wakala, au wakala yeyote kwa kujua atatumia kwa lengo la kumdanganya mkuu wake, risiti,akaunti au hati au nyaraka yoyote inayohusiana na mambo au shughuli yoyote ya mkuu wake wa kazi na ambayo ina taarifa feki,za kughushi au zilizopotoshwa na kwa jinsi yoyote ile zina lengo la kumdanganya mkuu,atakuwa ametenda kosa.mwisho wa kunukuu.

Sawa Hosea hakuona rushwa,je hakuona pia kipengele hiki cha sheria? je katika mkatba wa richmond hakukuwa na nyaraka feki zenye lengo la kumpotosha mkuu,je kusema kwamba richmond ina ubia na kampuni ile waliyoitaja na kuthbitisha hilo kwa business kadi hakukuwa na lengo la kumpotosha mkuu?je,ukweli kwamba richmond haikuwa mtu kisheria yaani sio kapuni halali kwa kuwa inakosa usajili tanzania na huko USA haipo na kwamba hata kama ilisajiliwa hapa nchini usajili wake haukuwa halali kwa kuwa hatuna one man company kwa mujibu wa kifungu cha tatu,moja cha sheria ya makampuni.je,waliohusika hawakuwa na lengo la kumpotosha mkuu?
Watu wote waliokuwa wakideal na richmond walikuwa wanajua nini kinachoendelea toka mwanzo hadi mwisho,na ukweli wote hapo juu walikuwa wanaujua je,hakuwa na nia ya dhati ya kumpotosha mkuu? ili aingie mkataba na mtu asiyekuwepo(yaani fictitious person?) Hosea hili hakuliona kabisa? Kama hakuliona anatofautiana vipi na sisi walei(laymen) wa taaluma ya kuchunguza rushwa? basi ameprove incomptence kwenye taasisi yake iwapo atashindwa kuthibitisha hili.Basi uchunguzi wake ulijikita kwenye nini? yaani ni vitu gani alivyoviangalia hadi akaandika ripoti?
Je,kama vigezo hivyo hapo juu havikwepo kwa maana kwamba kampuni ilitoa nyaraka feki juu ya uwepo wake kisheria na maafisa wetu wakavipokea na kumwaminisha mkuu ili anendelee kuingia mkataba je,hakukuwa na harufu ya rushwa iliyowapofusha maafisa wetu wasiweze kuchunguza zaidi juu ya uwezo wa richmond kisheria na kama je,imetimiza masharti yote ya sheria za tanzania?Mbona ukisoma mkataba wa richmodn maafisa wetu wanasaini kabisa kauli zao kwamba wameridhika richmondi ni kampuni halali kisheria na haijavunja sheria yoyote ya tanzania,wakati kwa hakika imevunja sheria ya makampuni na sheria ya mikataba ya mwaka 1961.

Sawa Hosea atasema yote haya si kazi yake na hayakuwamo Richmondi. Ok,si kazi yake ndiyo lakini jaji mmoja kwenye kesi ya Donoghue v,stevenson[1932]QB aliwahi kusema "....iwapo tutakwenda hatua moja kwanini isiwe hamsini?" HOSEA alifikiaje uamuzi wa kumshitaki balozi mahalu? alijuaje kuwa pale kuna mkono wa rushwa wakti mazingira yake yalikuwa swa na richmond? Ni kwanini HOSEA alitumia kifungu cha sita katika suala la mahalu kumtia mahalu hatiani wakti kwenye richmond hakukitumia?ilikuwaje katika mashtaka ya mahalu Hosea huyohuyo akamchaji pia balozi mahalu na uhujumu uchumi pamoja na wizi kama mtumishi wa umma kwa mujibu wa sheria ya kanuni ya adhabu(pena code cap16) na pia sheria ya rushwa 1971,wakati kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1971 hakuwa na mamlaka ya kuestablish makosa hayo?

Mamlaka ya kuchaji mahalu kwa kutumia penal code na Economic and organised crimes control Act aliyapata wapi.Hivyo basi kama aliweza kwenye hili la mahalu tultegemea aweze pia kwenye richmond kwani kanuni za haki zinasema "justice must not only be done but must be seen to be done" na katiba yetu intambua equality before the law. Ni kutokana na mashaka haya niliyoataja hapo juu ndio maana mhe. Hosea anatuhumiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine kwenye sakata la richmond kwa kuufumbia macho uovu wa wazi.
Na kama mwanazuoni? utafiti wowote unasehemu ya hitimisho na mapendekezo,ambayo tulitegemea hosea aseme,pamoja na kuwa kazi yangu si kuangaliwa mikataba na masuala ya uhujumu uchumi,lakini katika utafiti wangu au uchunguzi nimegundua mapungufu yafutayo kwenye mkataba wenyewe na kwenye uhalali wa kampuni ya richmond kisheria ambao napendekeza ziundwe tume maalumu zenye mamlka ya kuchunguza uhalali wa mkataba huu nk.ili kujiridhisha zaidi. Hapa angekuwa safe,lakini yeye alikana kabisa na kusema mchakato wote ulizingatia sheria na ulienda kwa kufuata vipengele vyote wala hakuna harufu ya rushwa na wala hatupati hasara.mmh HOSEA ulienda mbali mno uliposema vipengele vyote vya sheria vilifuatwa je,na kanuni za manunuzi zinazosema tenda itangazwe siku 45 na wao wakatangaza siku kumi je,huko kulikuwa ni kufuata sheria? au ripoti ya PPRA hakuiona?

Kwa mantiki hii mimi na wadau wengine ndio maana tunashawishika kukubali kuwa Mhe.HOSE anawajibika katika sakata hili la Richmond unless aje na maelezo ya kuridhisha zaidi lakini sio kujibu wadau kwa jazba.
 
Samahani wadau kwa makala ndefu lakini,imebidi niiandike hivyo ili kujiridhisha na majibu ya hosea.Naomba tu tusameheane,muisome na kutoa mawazo yenu.
 
Augustoons,
Mkuu wangu wala hujakosea kabisa. Kifupi umenifunga mdomo!..haya ndio maneno.
Sina zaidi Hosea GUILTY as charged!
 
Sijui na sielewi nini kinampa kiburi Hosea, Hivi anacheza na nguvu za Wananchi, kama wananchi hawana imani na chombo anachokiongoza ina maana hata ushirikiana hatapewa... asitake kujificha na sheria. Sheria zenyewe za Tanzania za Kocopy na Kupest sometimes wanacopy wrongly. Asitake kujificha kwenye mgongo wa sheria... Akikwepa hili najua la BOT atakimbia mwenyewe kwani anajua kila kitu na yeye amekaa kimya muda wote...
 
Samahani wadau kwa makala ndefu lakini,imebidi niiandike hivyo ili kujiridhisha na majibu ya hosea.Naomba tu tusameheane,muisome na kutoa mawazo yenu.

Mkuu haujakosea katu na wala haichoshi kuisoma ila ninashauri watu wa media wangeitumia ktk makala zao ili kuibua mjadala wa hoja.
 
Back
Top Bottom