Aliyoyafanya January Makamba Bumbuli

Mambo ya jimboni Bumbuli waachiani wanabumbuli, wewe jimbo lako la Ubungo kero kibao
 
Nimepitia website ya january makamba sijaona orodha ya mambo aliyoyafanya Bumbuli katika kutekeleza ahadi alizozitoa

website ya Bumbuli hii hapa

Bumbuli Development Corporation... Coming Soon!

ukiingia unaambiwa utatumiwa e-mail ya maendeleo lakini so far ni mwaka mzima hakuna kitu chochote

Sasa kwa mbunge ambaye anapatikana kwenye mitandao hatupatii ripoti ya maendeleo kama alivyofanya Marehem Regia Mtema au Mbunge wa Singida ndugu Mo Dewji

January tunaomba uje utuambie umeshafanya nini Bumbuli toka uchaguliwe?

Kinachofanyika ndani ya CCM ni hatari inayopikika. Kuchafuana kumeanza, kila mtu anaiangalia nyota yake na kujaribu kumfanya yule aneyemonwa tishio aonekane mchafu ndani ya Jamii. Hizi siasa za makundi ni mibaraka ya CHADEMA. Vita kati ya

JK na Ikulu, Lowassa, Membe, Ngeleja, Samwel Sita, Mwakyembe, Mwandosya, Nyalandu, Rostam na wafuasi wao kama kina january zinakuja kulipasua chama tawala. Subirini kidogo waanze kuuwana. Hiyo ndo iliyobakia, kuuwana kwa maana wanaelekea kubaya. Huyu january ni swala lingine kwa maana kila kitu kapewa hadi vyeo 7 alivonavo. Kwa nini awe mzungumzaji mkuu wa EWURA, na TANESCO? anapinga kupanda kwa umeme wakati umeme umeshapandishwa, mbona hakufanya hivyo kabla ya umeme kupandishwa au ndo tumuone mchapkazi? hatudanganyiki tena watanzania. Anayataka mwenyewe ndo maana anamalizwa kwenye mitandao. Hauwezi kuwarushiwa wengine mawe ukiwa kwenye nyumba ya vioo. january anasemekana bingwa sana kuchafua viongozi kwenye mitandao. ale dosi yake mwenyewe. Heri angenyamaza kuliko kuwa kama NAPE. Mafisadi wanaolipwa hela za umeme watammaliza. Hakuna lingine hapa. Wanaommaliza ni hao hao anajaribu kuwapinga wakati mwenyewe ni fisadi kinara. Siasa ni mchezo mchafu kweli
 
1..Amesaidia kuimarika kwa migogoro ya wakulima wa chai(smallholders) vs wenye viwanda vya kusindika(processors) na vyama vya wakulima wa chai vs processors..Kwa hilo nampa pongezi yaani amekata mguu kabisa kutokana na kushindwa kutimiza ahadi zake za utatuzi:
-Ikiwamo kuwasaidia wakulima wadogo kumiliki hisa zaidi ya 50% ya Mponde Tea Factory ili waweze kuwa na sauti katika upangaji wa bei ya Green Leaf.
-Kuwawezesha wamiliki mini-processing, facilities,packing & blending factories ili waweze kupata faida zaidi kukamilisha the whole value chain.

2..Ukija kwenye upande wa barabara unaweza kulia machozi kwani terrain ya kule ni milima kwenda mbele sasa usiombe mvua ikukute kule juu Bumbuli wakati wewe una mpango wa kurudi kulala Soni au Lushoto mjini.Lazima uombe hifadhi kwani barabara hazipitiki unless you have a death wish..

3..Amesaidia kuwepo na bendera,khanga,kofia na scarf nyingi za CCM.Yaani evergreen ya Chama imetapakaa kule juu na chombezo la njano kwa mbali.Bendera zapepea kwenye mashina na nyumba za wabunge wengi wakiwa wamejenga vile vigorofa vya jadi.People are in smiles waiting to line up for the next election.

It leaves a lot to be desired.
 
Nimepitia website ya january makamba sijaona orodha ya mambo aliyoyafanya Bumbuli katika kutekeleza ahadi alizozitoa

website ya Bumbuli hii hapa

Bumbuli Development Corporation... Coming Soon!

ukiingia unaambiwa utatumiwa e-mail ya maendeleo lakini so far ni mwaka mzima hakuna kitu chochote

Sasa kwa mbunge ambaye anapatikana kwenye mitandao hatupatii ripoti ya maendeleo kama alivyofanya Marehem Regia Mtema au Mbunge wa Singida ndugu Mo Dewji

January tunaomba uje utuambie umeshafanya nini Bumbuli toka uchaguliwe?

Mkuu napenda nikwambie mambo mawili;
1. Kipindi cha ubunge ni miaka 5, hivyo kuhukumu January sasa hivi kwamba hajafanya lolote si sahihi
2. Udhaifu wa website updates haimaanishi kwamba hakuna kilichofanyika. Ukitaka kujua kama kuna mabadiliko basi nenda Bumbuli
 
Nimepitia website ya january makamba sijaona orodha ya mambo aliyoyafanya Bumbuli katika kutekeleza ahadi alizozitoa

website ya Bumbuli hii hapa

Bumbuli Development Corporation... Coming Soon!

ukiingia unaambiwa utatumiwa e-mail ya maendeleo lakini so far ni mwaka mzima hakuna kitu chochote

Sasa kwa mbunge ambaye anapatikana kwenye mitandao hatupatii ripoti ya maendeleo kama alivyofanya Marehem Regia Mtema au Mbunge wa Singida ndugu Mo Dewji

January tunaomba uje utuambie umeshafanya nini Bumbuli toka uchaguliwe?

Ulianza vizuri ku adress mada lakini umechanganya kulinganisha Regia na Mo. Month anataka biashara zake ziende ziwe kwenye utaratibu au la. Ndo maana yuko kwenye siasa lakini marehemu regia aliwasaidia wananchi wake akiwa hana pesa
 
hivi huju january anauhusiano na yule makamba mbwatukaji?na je siku hz kikowapi hicho kizee jamani au kime r.i.p.mpeni salamu zangu kama bado anapumua.
 
Wakuu hii thread imechakachuliwa, ule utamu wa Mwammy wameungo'oa!
Ule utamu wa Mwammy ndio ulikuwa unaonyesha ni jinsi gani Januari aliweza kumngoa mzee Shelukindo.
Na kama ule utamu wa Mwammy ni kweli, haina ubishi kwamba januari hafai kabisa kwenye any public office.
Mkuu, tuwekee tena ule utamu, ila angalia WASIKUPELEKE INDIA.
 
Nikipenda hiki kijiwe. January anaonekana ni nyota inayong'aa. Mgogoro wa wakulima wa chai, suala la Bumbuli kuwa Halmashauri na kuanzishwa kwa shirika la kuharakisha maendeleo ya jimbo lake. Yote in such a short span.

Acha aendelee kutuumiza kichwa wabeba box.
 
Hii mods wataiondoa muda si mrefu i guess maana januari sijui ana ushawishi gani humu,tusubiri tuone kama wataniprove wrong..
 
Nilitaka kusema waacheni wananchi wa Bumbuli waamue.

Nikakumbuka.

January Makamba ni mbunge wa CCM, si mbunge wa Bumbuli, hakuna mwananchi wa Bumbuli hata mmoja aliyempigia kura, atakuwaje mbunge wa Bumbuli?

Na kuna wananchi wengine tunaweza kusema January hata si mbunge kikatiba, kwani hakuainishwa katika katiba.
 
January Makamba ni member wa JF? Na kama siyo, basi ndiyo muda muafaka kuyaleta hapa hayo mafanikio yake ili achangiwe na Great thinkers kwa ajili ya manufaa ya kwake na wapiga kura wake!
 
January Makamba ni member wa JF? Na kama siyo, basi ndiyo muda muafaka kuyaleta hapa hayo mafanikio yake ili achangiwe na Great thinkers kwa ajili ya manufaa ya kwake na wapiga kura wake!

Kusema kweli mimi bila kuficha na kwa moyo mkunjufu kabisa nakiri kuwa nilimpigia kura Bw. J.J. Mnyika ili awe Mbunge wangu wa Ubungo na akawa. Nilifadhaika sana baada ya kuona Regia Mtema (RIP) amekuja na kutuambia ni nini amewafanyia wananchi wake (japo yeye hakuwa Mbunge wa Kilombero) lakini Mbunge wangu wa kuchaguliwa tena nami nikiwa nimechangia kura ati hajajitokeza na kutuambia katufanyia nini! Namuamini Mnyika lakini naomba ajitokeze hapa JF (huwa namuona mara kadhaa) atuambie ni nini katufanyia wana ubungo. Najua yapo mengi lakini ingependeza yeye mwenyewe akayanena kwa kinywa chake.

Pia kwa kuwa ni Mkurugenzi wa Uenezi (Propaganda) basi awahamasishe wabunge (hasa wa majimbo) wa CDM wajitokeze humu na kumuunga mkono Regia (RIP) kwa kutuambia wamewafanyia nini wananchi wao kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
 
Kwa majaribio madogo tu jana nilituma mada kuhusiana na wapi rais Jakaya Kikwete anapata muda kwenda misibani lakini siyo kuhimiza maendeleo. Mada hiyo iliuawa pamoja na kuituma zaidi ya mara tatu. Kwa mchezo huu si JF itangaze wazi kuwa imeingia ubia na serikali kufanya kazi ya ushushu na PR? Si hilo tu kwanini mtu atoe dukuduku lake watu au kikundi cha watu kiliondoe kwenye matandao hata bila kumtaarifu? Hizi ni tabia za magazeti ya chama na asasi nyingine za kifisadi za propaganda za serikali. Heri kutangaza wazi kuwa JF imeingiliwa.
 
Hii mods wataiondoa muda si mrefu i guess maana januari sijui ana ushawishi gani humu,tusubiri tuone kama wataniprove wrong..

Mkuu umechelewa, kulikuwa na dossier moja kutoka kwa Mwammy wazeee waitoa!
Ni kweli, influence yake sio mchezo, maana za Mzee wa Kaya, RA, Dr. Pombe, EL na wengine zinakaa hadi wana JF wanazichoka.
 
Nilitaka kusema waacheni wananchi wa Bumbuli waamue.

Nikakumbuka.

January Makamba ni mbunge wa CCM, si mbunge wa Bumbuli, hakuna mwananchi wa Bumbuli hata mmoja aliyempigia kura, atakuwaje mbunge wa Bumbuli?

Na kuna wananchi wengine tunaweza kusema January hata si mbunge kikatiba, kwani hakuainishwa katika katiba.

Alipita bila kupingwa?
 
lol naona kama jk alivyokuwa mdogo,ni picha yake ya utotoni?

22.JPG
 
Januari Makamba si Mbunge wa wananchi ya Bumbuli ni mbunge wa genge la wanasisiemi wa Bumbuli, tunahitaji wabunge wanaochaguliwa na "Majority" si "Minority"...Wakati tunajiandaa kuelekea mchakato hai wa kuandika katiba Mpya lazima tuweke sheria ya mwakilishi "Mbunge" itakayofuta ubunge wa kutopita bila kupingwa, hata kama mgombea ni mmoja lazima apigiwe kura za "NDIYO" au "HAPANA", kwani bila hivyo tunazalisha wabunge wanunuzi wa wagombea Ubunge na si Wabunge. Hatuhitaji nguvu za pesa zitupatie Wabunge bali nguvu za hoja na mipango zizalishe wabunge wanokubalika kwa njia zisizo na mizengwe.
 
Back
Top Bottom