Aliyesababisha kifo cha Salome Mbatia akamatwa

Hivi hapa nchini mwetu, ni muda upi hupita mpaka topsecrete na confidential files (simaanishi mikataba) nyingine zina kuwa legally released to public?!

SteveD.
 
Acheni kuzunguka zunguka. Mnataka kusema huyo dereva alikuwa amepewa task ya kuondoa roho ya zitto?? Mnaanza kuhukumu hata uchunguzi haujafanyika. Mmoja hapo juu anasema eti hilo fusso lilifuata moja kwa moja gari la marehemu. Naomba kumuuliza, ajali huwa zinatokea vipi?? is it not the case kwamba magari inabidi yakutane uso kwa uso ili ajali iweze kutokea??? Sasa ajali ingetokeaje kama kila dereva angeendelea kubaki kwenye lane yake???

MAMBO HAYA NDIO NINAYOPIGIA KELELE HAPA NA SITONYAMAZA DEFINITELY SO BAD LUCK KWA HAO WANAODHANI NITANYAMAZA !

SIASA WANA-APPLY KATIKA KILA KITU !

BINADAMU WALIVYOKUWA WAZITO !
 
ha ha a ha ha ha ha

somebody kaanza kujihisi hapa! ameanzisha kampeni za chuki dhidi ya JF na ameshangaa ndio memba wanazidi kuongozeka day after day na sasa ameanza kukimbia kivuli chake kuwa kuna watu wanataka anyamaze!

ha ha ha ha ah.... endelea kuexplode. JF is here to stay so kunywa sumu or something
 
Mungu ni mkuu na mwema sana!!! naamini ataendelea kumlinda mh. Zitto na kila aina ya hila na ubaya unaolengwa kwake!!

It looks as if he was the target!!

Acheni POROJO na SIASA hadi kwenye mambo ya ajali. Hiyo ni ajali kama ajali nyingine tu. Bongo hatujafikia hatua hiyo ya kutaka kujitoa mhanga. Hizo ni Hadithi za kuuza magazeti tu. Kwanza gazeti lenyewe ............
 
Sijui ni kwanini watu wanapenda sana kukuza na kuandika mambo ambayo hayapo.

PHP:
Labda wangetaka tuamini kuwa Zito ndio alikuwa target basi wangetuambia how they think the whole plan was executed and what went wrong.

From my simple understanding and from what the madia has reported hii inaonekana ni ajali ya kawaida tu ambayo ingeweza kumpata mtu yoyote.

Kama Zito alikuwa target basi dereva wa lori lazima alijua Zito anatumia gari gani. Unless gari lake na la Marehemu yalikuwa sawa then jiulize kwanini alikosea na kuligonga gari la Marehemu?

Pili mwandishi anataka tuamini kuwa Marehemu, Zito, Sumaye na Mathayo walikuwa wanaongozana barabarani kiasi kwamba kama dereva wa lori angeikosa gari ya Marehemu basi angeligonga gari la Zito. Zito mwenyewe kasema kuwa alifika sehemu ya tukio baada ya dakika tano hivi. Kwa wale wenye uzoefu wa kusafiri safari ndefu, dakika tano kwa gari linaloenda Km 80 kwa saa ni sawasawa na umbali wa Km 6 hivi. Sasa kwa umbali huo utaona kuwa hata kama angeikosa gari ya Marehemu basi angeweza kuanguka mwenyewe tu unless mwandishi anataka tuamini kuwa hiyo error kama isingetokea kwa Marehemu basi ingetokea kwa Zito.

Pia mwandishi anakuwa na mashaka juu ya maelezo ya polisi kuwa dereve wa lori alitoroka au "kutoroshwa" baada ya ajali. Kwa kumbukumbu zangu mara nyingi madereva wasababishapo ajali hukimbia kuhofia maisha yao na wengine wakiogopa kushitakiwa. 

Mimi naona hii ilikuwa ni ajali ya kawaida tu kama ajali nyingine.

Ukitaka kukataa kitu wakati mwingine usitafute theory ili kufanya proof.Sema tu kuwa hiyo ilikuwa ajali ya kawaida.
tembelea mikoa ya Kigoma na Rukwa ili ujue mambo.
Uliza habari za Marehemu TEDI Magayane na Mama Lukandamira (wote hao marehemu)ndo uijue hii dunia
 
Hii ni assassination attempt that went wrong, I said it, yes I said it!

IVI WATANZANIA WAMESHAFIKIA HATUA YA KUJITOA MUHANGA? SIAMINI NA SITAAMINI NAAMINI HIYO NI AJALI YA KAWAIDA NA TUSIANZE KUITAFTIA SABABU,ZITO KAFANYA NINI CHAKUMTISHIA AMANI NANI ADI WATAKE KUMZURU? NAAMINI SIASA NDIVYO ZILIVYO, MALUMBANO KATIKA SIASA NI VITU VYA KAWAIDA.KAMA NI HIVYO AKINA MREMA,MTIKILA, GEN ULIMWENGU TUSINGEKUWA NAO ADI LEO. WAZO BINAFSI NAWAKILISHA
 
Araway,

ni vizuri pia nawewe umesema kila unachofikiri. Ndio maana niliweka emphasis kwenye neno conspiracy. I dont know why BUT mimi the whole thing hapa iko fishy kama vile vifo vya Kolimba, mkemia mkuu wa serikali, Kombe, nk vilivyo na maswali mengi zaidi ya majibu.

Nimesema pia kuwa naweza kuwa wrong (I hope that I am wrong).
 
Sitaki kuamini nini kinasemwa hapa!!Lakini nilipata kufanya kazi na mtu makini sana.Nae alinipa maneno ambayo ni key kwenye mambo yangu mengi,Mzee yule aliwahi kuniambia "Be suspicious with Everything" Baada ya Uchunguzi uliochukua karibu miezi 12, Report ilimbana Mkuu wa kitengo kwa uizi,ambaye ndie alikuwa muelekezaji wa kila kitu ili kurahisisha Uchunguzi!,Kwa mazingira ya kawaida mtu huyo usingeweza kumfikiria kuwa ndiye mwizi Mwenyewe!!!

Sasa Waungwana tuwe waangalifu na tupime kila kitu kwa uzito wake."Sio kila aendae kanisani ni mcha Mungu".Tusiyakanushe yasemwayo sasa na wala tusiyakubali moja kwa moja ,lakini lazima tuweke (?) na kusubiri Uchunguzi.
 
Ha ha eti Assassination Attempt, duh!! jamaa alimiss darasa la planning.Inabidi apelekwe kwenye training ya Blackwater USA awe polished.
Ila this is funny it has made my day.
 
Actally kuna maswali aya kujiuliza. Pahala ilipotokea ajali na dereva kutoweka. Kauli ya kamanda wa polisi ndiyo ina mluweluwe. DEREVA KATOROSHWA na nani? ndiyo maana watu wanahoji kuwa kuna mkono wa mtu.
 
Sitaki kuamini nini kinasemwa hapa!!Lakini nilipata kufanya kazi na mtu makini sana.Nae alinipa maneno ambayo ni key kwenye mambo yangu mengi,Mzee yule aliwahi kuniambia "Be suspicious with Everything" Baada ya Uchunguzi uliochukua karibu miezi 12, Report ilimbana Mkuu wa kitengo kwa uizi,ambaye ndie alikuwa muelekezaji wa kila kitu ili kurahisisha Uchunguzi!,Kwa mazingira ya kawaida mtu huyo usingeweza kumfikiria kuwa ndiye mwizi Mwenyewe!!!

Sasa Waungwana tuwe waangalifu na tupime kila kitu kwa uzito wake."Sio kila aendae kanisani ni mcha Mungu".Tusiyakanushe yasemwayo sasa na wala tusiyakubali moja kwa moja ,lakini lazima tuweke (?) na kusubiri Uchunguzi.

Lisemwalo lipo na kama halipo linakuja. Maneno mazito hayo mkuu kama unakumbuka vizuri wakati tetesi za jaribio la kumuua Moringe Sokoine alipokuwa anatoka kusali kanisani na baadaye kwenda kutibiwa nje na aliporudi Mwalimu alikuwa safarini Mozambique, nafahamu kuna watu wana picha zile zilizotoka Daily News wakati ule na alihamisha kambi ya kusali ikawa ST. Joseph, pia mauza uza yaliyojitokeza baada ya kifo chake baada ya yule rubani kwenda na hamsini zake. Tusubiri tutaona mengi.

Je, huyo dereva alitokomelea wapi? Hivi sasa yuko wapi?
 
Ha ha eti Assassination Attempt, duh!! jamaa alimiss darasa la planning.Inabidi apelekwe kwenye training ya Blackwater USA awe polished.
Ila this is funny it has made my day.

teh teh teh,

Inabidi tena training iwe two extra years than normal
 
Lisemwalo lipo na kama halipo linakuja. Maneno mazito hayo mkuu kama unakumbuka vizuri wakati tetesi za jaribio la kumuua Moringe Sokoine alipokuwa anatoka kusali kanisani na baadaye kwenda kutibiwa nje na aliporudi Mwalimu alikuwa safarini Mozambique, nafahamu kuna watu wana picha zile zilizotoka Daily News wakati ule na alihamisha kambi ya kusali ikawa ST. Joseph, pia mauza uza yaliyojitokeza baada ya kifo chake baada ya yule rubani kwenda na hamsini zake. Tusubiri tutaona mengi.

Je, huyo dereva alitokomelea wapi? Hivi sasa yuko wapi?

Hili swali la huyu dereva hata mimi najiuliza right now
 
Kwa hali ya dunia ya leo siwezi kuweka dhamana yangu kwa maelezo yoyote yale....
Ila nachosema hiyo ajali ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba nashindwa hata kifikiria zaidi nje ya ile ya marehemu Sokoine!
hadi sasa hivi tunasema ni ajali na itabakia hivyo hadi ushahidi upatikane lakini hii haina maana dhana haziwezi kuwepo. Hata Polisi kabla hawaja mwangushia mtu mashtaka huwa na tuhuma za kile kilichotokea. Hujenga conspiracy theory ya kile kilichotokea kisha kuitafutia motives kuwa crime kulingana na vielelezo vichache vilivyopo. Ukweli huja patikana mahakamani lakini haizuii hata kidogo Polisi (Prosecution side) kuwa na theory yao.
Tuchukulie Mwafrika wa kike ni mmoja wa wataalam wa maswala haya hapa JF na katoa ushauri wake kisha nasi tusiokubaliana tuwe ya vielelezo vinavyo ashiria kuwa hii ni ajali sio zaidi. Hapo tunaweza pima habari zote badala ya kutoa hukumu zetu kwa sababu tu aliyetajwa hapa ni Zitto. Je, vipi kama ilikuwa crime na huyo mama marehemu waziri wetu ndiye alikuwa target?...bado hatuwezi kusema hii ni crime?... na kama sio mbona dereva kaingia mitini na Polisi wanamtafuta. kwa nini wamtafute mtu asokuwa na hatia..
So far kutokana na habari hizi hii inachukuliwa kama crime.. hit and run.. motive bado tunasubiri kwa hiyo jengeni lolote linalowezekana.
 
Juzi juzi kuna dereva kakamatwa . Dereva huyu alisababisha ajali iliyoua watu kadhaa miaka kama mitatu iliyopita...
Sioni ajabu huyu dereva kukimbia.
Kila stori tunayopata tunajaribu kuiexploit politically. Hivi tutafika kwa mwendo huu wa kuzua kila inapowezekana?
 
Insurgent,
U'r signature says it all! even on this case.
Have an open mind kwani kama unaamini:-
The fact that a believer is happier than a skeptic is no more than the fact that a drunken man is happier than a sober one.

Then anything is possible!
 
ANYTHING is possible kwa vitu vingi hata wewe ukiwa unatembea barabarani ukijikwaa unaweza kusema nimetegeshewa. Inategemea na state of your mind. Kuna watu ambao wako so negative in thinking to the extent CHOCHOTE kitokeacho basi LAZIMA kihusishwe na serikali. Tujaribu kuwa na open mind.
 
Mimi naomba kuuliza hivi:
Hivi kuna mtu hapa anaamini kabisa kuwa sirikali au niseme CCM ina nia ya kumtoa roho Mheshimiwa Zitto?
I don't think so! Hii ni ajali mbaya tu iliyotokea mpaka sasa, nukta!
 
Back
Top Bottom