Mohamedi Sekiet
New Member
- Jun 11, 2011
- 3
- 0
Mohamedi: muacheni naona anataka kuendeleza kuiua nchi yetu.TULIO BAKI TUKAZE BUTI.
Hongera mwanangu wee hongera nasi tuhongeree wee hongera!
Jama lina uma mno wee!
Asante m-coconut, msukuma mikokoteninilisema , huwezi kuwa member wa ccm ukawa timamu ! Haiwezekani,kielelezo cha fikra lojo.Kwani kazi za serikali wanauliza kadi za chama ! Ni juha anaeweza kufikiri sawa na wewe.Kazi zenye kuhitaji kadi ni zile za chama chenu .Kazi za umma , hazina vyama. Punguza ujuha kidngo uwe timamu.
unalo nanilako hilo zigo la misumariNa Chadema walingoja nini mpaka uchaguzi uishe ndio walete hii habari au hao kina makanja washahama Chadema?
Mkuu huo ndiyo ukweli nami nillitaka kuweka bayana hilo, na kwa taarifa tu hiyo nafasi ya katibu aliyosimamishwa bawaba Nyanza bado haijajazwa baada ya kutemwa kwa usaliti wake. Kisha anasema ana mapya ama kweli CCM hapo wamelamba galasa na ndiyo mwisho wake kisiasa.MBUNGE mteule wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ameingia katika kashfa ya rushwa ya uchaguzi na huenda akapoteza ubunge, MwanaHALISI limeezwa.
Mkono ametajwa kutoa mlungula kwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika jimbo hilo, Michael Makanja ili ampe nafasi ya kupita bila kupingwa.
Taarifa zinasema Makanja amewaeleza viongozi wa Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA, kwamba alishawishiwa na Mkono kupokea kiasi cha Euro 1,000 ( karibu Sh. 2 milioni) ili kujitoa katika kinyanganyiro cha ubunge.
Fedha hizo ni sehemu ya mamilioni ya shilingi ambayo Mkono inasemekana aliahidi kumlipa mgombea huyo wa Chadema.
Baada ya Makanja kufika hapa, wanachama walimvamia wakitaka kujua nini kimemsibu. Hapo ndipo mchezo ulipobumburuka, alisema afisa mwandamizi wa ulinzi na usalama wa Chadema, Hemed Sabula.
Alisema Makanja aliwasili katika ofisi za makao makuu ya chama hicho kwa lengo la kukutana na viongozi wakuu wa chama, lakini kabla hajaingia ndani alikutana na kundi la wanachama waliombana aeleze ukweli wa kilichotokea hata akajitoa.
Makanja alijitoa kugombea ubunge katika jimbo hilo, siku mbili baada ya kuteuliwa kuwa mgombea kwa kumuandikia barua msimamizi wa uchaguzi wa jimbo.
Aidha, Makanja aliwataja viongozi wawili katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Sibitari Nyanza na mwenyekiti wa vijana wa mkoa, David Katikiro kwamba ni wabia katika mpango huo.
Kwa mfano, ujumbe wa simu ya mkononi uliotumwa kwa kigogo huyo kutoka kwa simu ya Makanja (namba tunaihifadhi) unasema, Mzee ameshanikatia tiketi ya kwenda Dar. Sasa mhimize amalize kiasi kilichobaki, maana hali yangu kiuchumi si nzuri .
Mwingine ulisema, Tumeshamaliza kama tulivyokubaliana. Ujumbe huo ulitumwa tarehe 21 saa 8:21 mchana.
Ujumbe mwingine uliotumwa juzi Jumatatu, mara baada ya Makanja kuingia mtegoni ulisema, Niko makao makuu ya chama. Nimewekwa chini ya ulinzi....
Akijibu katika namna ya kushtuka, kigogo huyo alijibu, Wewe nani kakwambia uende huko Watakuua. Siwezi kuja huko kukutetea....
Taarifa zilizofikia MwanaHALISI zinathibitisha kuwa tayari Chadema kinaandaa malalamiko rasmi kwa Msajili wa vyama vya siasa dhidi ya hatua hiyo ya Mkono.
Umeyaona majibu yako, acha ushabiki utaheshimika kuliko kuwa kama FaizaFoxy.Breaking News: PIGO CHADEMA MARA
Katibu wa CHADEMA wa Mara Nyanza Sibitari amerejesha kadi rasmi jioni hii katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na aliyekuwa mbunge wa Musoma Mjini Vedasto Manyinyi.
Sibitari aliyeongozana na vijana wengine 126 na bendera na Kadi za CHADEMA anadai kuwa kajiengua CHADEMA kwa sababu zifuatazo:
- CHADEMA Kuendeshwa kama Taasisi na si chama
- Kushamiri kwa makundi ndani ya Chama hicho
- Mgogoro ulioanza toka nyakati za uteuzi wa viti maalumu hadi Ubunge
Anadai alipotea na sasa karudi nyumbani
More UP DATE to follow
Breaking News: PIGO CHADEMA MARA
Katibu wa CHADEMA wa Mara Nyanza Sibitari amerejesha kadi rasmi jioni hii katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na aliyekuwa mbunge wa Musoma Mjini Vedasto Manyinyi.
Sibitari aliyeongozana na vijana wengine 126 na bendera na Kadi za CHADEMA anadai kuwa kajiengua CHADEMA kwa sababu zifuatazo:
- CHADEMA Kuendeshwa kama Taasisi na si chama
- Kushamiri kwa makundi ndani ya Chama hicho
- Mgogoro ulioanza toka nyakati za uteuzi wa viti maalumu hadi Ubunge
Anadai alipotea na sasa karudi nyumbani
More UP DATE to follow
Naomba usipotoshe umma,hii si breaking news kwani mtu huyu alisha fukuzwa kwenye chama siku nyingi.yawezekana kwa kuwa alikuwa katibu atakuwa alikuwa na masalia ya kadi.
we faiza ni nilisikia umekufa sorry umepigwa ban bado upo, au ni ghost.Hongera mwanangu wee hongera nasi tuhongeree wee hongera! Jama lina uma mno wee!